Hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan amkumbuka Ridhiwani Kikwete baada ya kusahaulika kwa kipindi kirefu

Nawasalimu kwa Jina la JMT,

Hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi yake kwa kupeleka Vifaa tiba Hospitali ya Wilaya ya Chalinze vyenye thamani ya Shilingi Milioni 480 ikiwemo mashine ya Kupiga picha za Mionzi yaani X-Ray, Jokofu la kuhifadhia maiti, mashine za kupimia damu na vifaa mbalimbali.

Mhe Ridhiwani Kikwete mbunge wa Jimbo la Chalinze ameishukuru serikali na Rais kwa kutekeleza ahadi hii ndani ya muda wa wiki tatu toka kutolewa kwa ahadi hiyo,

Wananchi wa Kata hiyo wakiongozwa na wakina mama ambao walikuwa wakipokea vifaa hivyo wameshangilia huku wazee wakimuombea Mungu amlinde Rais wa Nchi yetu mama Samia Suluhu Hassan,

Ridhiwani Kikwete ni miongoni mwavijana very humble down the earth mwenye bashasha na furaha kwa Watanzaia wote wakati wote iwe anakujua au hakujui hakika ni mtu mzuri sana|Hongera wanachalinze,

Je? Tutarajie siku moja kijana huyu kukamilisha msemo wa kiingereza unaosema " Like father like Son "?

#Kazi iendelee

View attachment 1959269

View attachment 1959270

View attachment 1959273

View attachment 1959274
Sijapenda ulivyomalizia unataka sisi tumalizie tuonekane wachonganishi, malizia like faza, like maza, like son.
 
Hii dunia hii, yaani watu wanafurahia kuletewa jokofu la kuhifadhia maiti..mh
Unafurahia mashine ya mionzi! Ina maana duniani hakuna teknolojia nyingine ya kuangalia mifupa hadi mionzi!
Nawaonea huruma sana watu wote ambao mmepitia kwenye mashine za CTScan au MRI yaani unachomwa cell zako zote za mwili...au huambiwi unazirudishaje cell hai mpya!!
Duh, kweli kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni, naomba kuheshim hilo. Ila bila haki hio, basi ninge.....
 
Baba ake alishindwa kujenga hii,
Mtoto miaka 5 ya ubunge ameshindwa,
Baba akiwa mbunge mwenye ushawishi alishindwa kufanya hili.

Sasa kitu gani cha ziada mpaka waone ni kama hatua kubwa ya kutaka promo?
 
Ingekuwa wakati wa mtawala wa chato hivyo vifaa vingekabidhiwa ikulu tena live coverage, viongozi wa dini, vyombo vya ulinzi na usalama na wasanii wote wangealikwa.
 
Sasa vitunzeni hivyo vifaa, sio baada ya siku kadhaa tunasikia kifaa kimeharibika!!
 
Ni Ushamba na roho mbaya tu Mkuu ndio inakupa shida
Ahahahahahahaha! Roho mbaya unayo wewe unayeamini hakuna mwingine mwenye uwezo wa kuongoza zaidi ya kakikundi. I tell you, "They'll RIP!" na nchi itaongozwa na wengine na ITAKWENDA!!!
 
Hiyo hospital mbona nanayake alioacha hoi, akiumwa hata vitu vidogo anakimbilia mjini. Shame on you
 
Hii dunia hii, yaani watu wanafurahia kuletewa jokofu la kuhifadhia maiti..mh
Unafurahia mashine ya mionzi! Ina maana duniani hakuna teknolojia nyingine ya kuangalia mifupa hadi mionzi!
Nawaonea huruma sana watu wote ambao mmepitia kwenye mashine za CTScan au MRI yaani unachomwa cell zako zote za mwili...au huambiwi unazirudishaje cell hai mpya!!
Huna akili bhabha si ety....maana hizi ulizonazo ni akili za panzi... Montelukast wewe
 
Ahahahahahahaha! Roho mbaya unayo wewe unayeamini hakuna mwingine mwenye uwezo wa kuongoza zaidi ya kakikundi. I tell you, "They'll RIP!" na nchi itaongozwa na wengine na ITAKWENDA!!!
Hii comment sio mkuu,

Lazima tuombeane mema wakati wote,

#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
 
Samia amkumbuka Ridhiwani Kikwete, naona kama inarudi ile hali ya ukitaka kitu fulani muone Ridhiwani. Watu na bahati zao juu ya hii dunia.
 
Samia amkumbuka Ridhiwani Kikwete, naona kama inarudi ile hali ya ukitaka kitu fulani muone Ridhiwani. Watu na bahati zao juu ya hii dunia.

Ni mawazo yako,

Ila Habari inamuhusu Samia,

Wala hajamkumbuka riz1 amewakumbuka wana charinze. Wanacharinze semeni Asante rais wetu.
 
Back
Top Bottom