Enyi wana wema mliojirani na Rais Samia Suluhu Hassan mstueni bega ageuke nyuma aone kwa macho yake mawili, asikie kwa masikio yake mawili then atumie ile rula ya kupima mabega ya wateule alivyoahidi.
Mkurugenzi huyu amelewa chakari fedha za umma kana kwamba TAKUKURU wako likizo au wanamuogopa. Shule zote za umma Msingi/Sekondary Temeke, madarasa yamekuwa yakijengwa na wakandarasi wazawa kwa gharama ya Shilingi 20milioni kwa darasa moja.
Wakandarasi takriban 8 wazawa kwa miaka minne wamejenga madarasa wilayani humu kwa viwango standard lakini DED amegoma kuwalipa kisa wamegoma "kumhakikishia chochote" akiadhimisha malipo yao. Sasa ni "saga" Kati ya DED na Mchumi na Mamlaka za juu zisipoingilia wawili hawa wanaweza kuuana maana Mchumi amegoma kuchukua rushwa kutoka kwa kandarasi wazawa.
Ili kuonesha kuwa yeye kweli ni DED wa Hayati Magufuli asiyetishwa sasa ameamua kuchukua madarasa yote 116 za wilaya kutoka shule mbalimbali na kumpa kandarasi mmoja nje ya wale "wagumu" na kumpa "mkarimu" kwa sharti la kujenga madarasa hayo kwa Shilingi 23milioni kwa kila darasa. Piga hesabu hizo 3m mara 116. Kweli hela za umma zinachezewa. Hazina mwenyewe.
"Mimi ndiye bosi wa Temeke, kama unadhani Mchumi anaweza kuwalipa, sitoe hela hadi mjifikirie, sitishiki na utawala mpya" anamjibu kandarasi mwenye mkono wa birika.
My Take: Rais SSH, agiza vyombo vyako kumchunguza mabega ya DED huyu. Atakwamisha mwendo kasi uliyoanza nayo. Inawezekana wako wengi wa aina hii. Mbali na kiburi lakini ufisadi wa aina hii ni aibu.
#FreedomIsBack