Rais Samia Suluhu Hassan arejea nchini akitokea ziarani Kenya

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,206
4,696

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani amesharejea Jijini Dodoma

Alipowasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma Mheshimiwa Rais alilakiwa na Makamo wa Rais Dkt Philip Mpango, Wakuu wa Vyombo Vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali.

Mama Samia alitembelea nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili ambapo alipata fursa ya kulihutubia Bunge la nchi hiyo.

Source: DPC Gerson Msigwa
 
Mama Jembe sana huyu! Wale " washamba" wenzangu tutulie kwani Nchi imepata mtu mwenye maarifa ya kuongoza Nchi na anajua Dunia inavyo operate ! Ili ule katika Dunia hii lazima na wewe uliwe kidogo ( by JK).

Mwendazake alitaka kutuua na njaa wakati yeye na akina Makonda, tikiti maji ( Musiba) wakila na kusaza.

Karibu Nyumbani Mama! Kazi uliyofanya hapo Kenya ni A+ umepata.
 
Ningekuwa mkuu wa TSS nisingeruhusu umma kujua rais atokapo nchini na arejeapo

hata kama source ni ya serikali!
 
Back
Top Bottom