Rais Samia Suluhu Hassan ampa onyo Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo

Mh. Rais amesema Wizara ya Tamisemi ina matumizi ya ovyo ya pesa za Serikali, yenyewe haikusanyi ni mwendo wa matumizi kwa kwenda mbele hivyo kamwagiza Waziri Jafo afuatilie vizuri matumizi ya wizara yake na kama akishindwa Basi asaidiwe(atumbuliwe)


Ushauri.

Mh Seleman Jafo jipange; Halmashauri, Hospitali,miradi ya ujenzi wa shule n.k hela zinapigwa sana, vituo vya afya EFD mashine hazitumiki vilivyo. Fuatilia Mama Samia hatakuhurumia atakutumbua shauri yako.
Yaani, kampa kavu!
Na kasema asipotosha , watamsaidia(Sack)!
 
Huyu Jaffo si ndo yule alimjambisha mkandarasi hadi akadondoka....!! Sasa ni zamu yake kujambishwa...!!
 
Sisi tunataka Mh Samia Suluhu arudishe maduka ya kubadili fedha maana mabenki yanatupiga sana hakuna ushindani.

Lile takataka la kisukuma hayati lishaondoka lazima mfumo ubadilike.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Apambane sasa atafute barabara, madaraja na majengo ya kuyapa majina ya mama Kama alivyokua akifanya kwa jpm.

Ule mda wa kufanya kazi ili kumfuraisha flan ushapita na kwa bahati mbaya tiari jofo alishazoe sasa sijui Kama ataweza kufanya kazi bila mapambio.
 
Tuwe tunaangalia na uwezo wa mtu kichwani sio ktk kelele nyuma ya mic au utanashati wake, pengine jafo kweli anastahili kusaidiwa kwakuwa huenda uwezo wake wa kiutendaji ktk fikra umeishia hapo, tusilazimishe aweze wakati hawezi. Jaffo jiuzulu kulinda heshima yako.
 
Kiukweli waziri wa tamisemi inafaa awe engineer wa kusomea kabisa maana ujenzi ni mwingi tizama mbezi stand BOQ ikasukwa kupigwa bil 15 sasa wamepiga ngapi nani anajua?? huyu bitozi masuti itamtesa apewe kawizara ka mazingira na usafi
Yaa hii wizara ipewe wahandisi kama ujenzi na maji maana Kazi kubwa ni ujenzi
 
jafo ni hardworking,tuseme tu ukweli .sema there's something wrong kwa watu wake,Wanampa ripoti za matango pori.Na ikitokea waka m curl,ameyataka mwenyewe,kwa kukubali kumeza ripoti za matango pori za watu wake.
 
Huyo Jaffo aliwahi kumpiga mkwara yule Mhandisi wa watu wa barabara kule Arusha na kutaka ahamishwe mara moja, kisa tu hakuleta wananchi wengi kuja kushuhudia uzinduzi wa barabara!

Na kwa mtazamo wake, akaona huyo Mhandisi anamhujumu Rais wake eti kwa Wananchi! Maana yeye Jaffo angehutubia watu wachache! Hatari sana.
Noma sana.tusubiri,Tamisemi dudu litakalo malizana na jaffo.
 
Hii ni mara ya pili huyu waziri wa TAMISEMI anahonywa mbele ya hadhara kwamba abadilike katika utendaji wake

Kwa kauli ya leo kutoka kwa Rais Samia Suluhu, Jaffo anatakiwa kujizuru nyazifa zake

Kakini pia huyu Jaffo ana nini cha mno mpaka aendelee kupewa maonyo kila siku juu ya utendaji wake na usimamizi wa mali za umma?
Katika hili Jaffo unatakiwa utumie hekima na busara kuiacha TAMISEMI, kiuhalisia wizara hii kubwa imekushinda

Hata wewe ungekuwa malaika usingeweza tamisemi kwani wizara ilikuwa chini ya ofisi ya bosi wake na wote mnamjua alivyokuwa kwenye matumizi ya serikali
 
Aisee ni kweli Tamisemi ni wizara iliyo sheheni mambo mengi na miradi na programu nyingi napendekeza baadhi ya miradi na programu zitolewe Tamisemi ziwe serikali kuu
Miradi ya ujenzi wa majengo ya shule na afya kwa mfano kwa nini wasifanye TBA? Kitengo cha uhandisi kule kitoke kiende TBA
 
Jafo mbona alikuwa busy sana kukagua miradi mbali mbali iliyo kuwepo tamisemi ..binafsi nahisi shida ipo ktk halmashauri na tawala za mikoa husika
Pengine ukaguzi wa ndani unashida pia
Lakini binafsi naona bado Jaffo ana paswa awe na msaidizi mkali mwenye uzoefu zaidi kuliko wanaomsaidia sasa maa naTammisemi ni kubwa mnoooo. Pengine ipewe ma naibu mawaziri wawili
Kwenye Ubize ndipo watu wanapopiga.
Rejea ripoti 'iliyoMtumbua kiani' CAG,
Mabilioni yamepigwa na waliokuwa Bize hawakuthubutu kusema yalikoenda na sasa wameanza kupukutika mmoja baada ya mwingine.
 
Ukishindwa sema tukusaidie..
IMG-20210328-WA0007.jpg
 
Huwa nashangaa pale watu wanapo msifia jaffo kwamba ni mchapa kazi, nabaki najiuliza huo uchapa kazi anaosifiwa nao unatokana na nini na ni mambo gani hasa amefanya huyu kijana kwenye wizara ya tamisemi hadi asifiwe kwamba ni mchapa kazi?

Kwa miaka mitano mfululizo hakuna ubunifu wala cha maana alichokifanya katika wiazara yake(kama kipo mniambie). Kazi yake kubwa kwa kipindi chote ilikuwa ni kusifia na kujipendekeza (uchawa) kwa boss wake.

Hata huo umaarufu alionao ameupata kutokana na media coverage maana wizara anayoongoza inagusa sekta zote na hivyo ni rahisi kwake kuonekana na kusikika kwenye vyombo vya habari kila siku na ndio chanzo cha yeye kuonekana mchapa kazi lakini behind jaffo ni debe tupu ambalo kazi yake ni kupiga makelele tuu.

Angalia hata ziara zake utakuta anaongea maneno mengi mithili ya ndege chiriku lakini utekelezaji wake ni sifuri.

Kwenye kudhibiti matumizi mabaya ya fedha kwenye miradi inayosimamiwa na wizara yake huku ndo hovyo kabisa. Mfano, kwenye miradi ya EP4R pesa zinapigwa lakini yeye yupo anaangalia wala hakuna hatua zozote anazochukua kuhakikisha pesa hizo zinarudishwa.

Baadhi ya halmashauri zilitengewa mamilioni ya pesa na serikali kwaajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi mbaya zaidi pesa zimeisha na ujenzi umeishia kwenye msingi na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa watu waliofanya ubadhilifu. Je kuna waziri hapa?

Huyu kijana apumzishwe tuu maana hata kiutendaji na ufuatiliaji anazidiwa na naibu waziri wake(david silinde)
Rais amteue bwana Tickson Nzunda kuwa katibu mkuu Tamisemi maana aliwabana Sana wapigaji akiwa Naibu anaeshughulikia elimu ,atamsaidia.

Pia wazari Jafo kama anaona kuna watu chini yake hawafanyi vizuri si awaseme kwa boss mama wapigwe chini?
 
Jafo wanamuonea tu,wakurugenzi wengi wameingia kwa kiki za uanachama wa kijani pia ni vilaza mno hawawezi kusimamia pesa za serikali.Aanzia kwa hao DED ndo shida zipo
 
Back
Top Bottom