Rais Samia Suluhu aweka rekodi ya kudumu Mikoa ya Kigoma na Katavi

===
Wakati Taifa likielekea kupokea Jumla ya Mega Watt 2,115 kutoka kwenye bwawa la JNHPP kwenda kwenye gridi ya Taifa ya Umeme Kigoma na Katavi bado walikuwa wanaongelea habari za umeme wa sola na majenereta,
==
Watu Wakigoma na Katavi ilikuwa ni hadithi ngeni kuwaambia watapokea mwekezaji yoyote toka nje au ndani wa kuanzisha kiwanda kwani Duniani kote sina hakika kama kuna kiwanda kinaweza kuendeshwa kwa Umeme wa Genereta au sola kwa ufanisi,
==
Wakati flani watu wa Kigoma na Katavi walipata mashaka kama na wao ni wana wa Tanzania kwani kwa kukosa kwao umeme wa gridi miaka 60 ya Uhuru kuliwatoa imani kwamba na wao ni Watanzania kama wenzao hoja ambayo leo Rais Samia anaijibu kwa vitendo,
==
Kwa mujibu wa meneja mkuu wa Shirika tanzu la TANESCO yaani Electrical Transmission and Distribution Construction Service Provider (ETDCO), Maclean Mbonile tayari Rais Samia anatekeleza mradi wa kupeleka umeme Kigoma na Katavi wenye Jumla ya Kilometa 776,
==
Umeme huu utatoka Tabora kwenda Mpanda na Tabora kwenda Kigoma kwa kilometa 383 na 393 kilometa kila moja kwa thamani ya TZS 15.9BL,
==
Mtakumbuka mradi huu ni miongoni mwamiradi 15 ya Mama Samia inayogharimu Jumla ya TZS151.48BL zilizokwisha kutolewa,

#Kigoma & Katavi hamkupata Umeme wa gridi tangu Uhuru,Kwani leo mnasemaje kuhusu Rais Samia ?

View attachment 2025434
Kigoma kama kunamtu wa kumshukuru basi ni huyu mama,
 
Apongezwe kwa kitu gani wakati ni wajibu wake.Hizo fedha ni kodi za Watanzania na wala hastahili pongezi yoyote.Watu wengine humu ni wanafiki watupu.Ona unakatwa makodi lukuki halafu unapeleka kwenye shughuli za maendeleo halafu unasema aliyepokea fedha hizo apongezwe.Wa kupongezwa ni yule aliyelipa kodi ambaye ni mwananchi.Ukweli ndo huo.
Mkuu kwani waliomtangulia huu haukuwa wajibu wao?
 
Kulikuwa na Mradi wa Malagarasi nadhani unazungumzia huo,

Huu ni Mradi wa Rais Samia Chief Mwenyewe chief
Mkuu huu mradi umeanza 2017, kuanzia Tabora, kwenda kigoma kupitia urambo tabora, na mwaka jana mwishoni nilikuwa kaliua, hata sub station ilishakamilika, na wa kwenda katavi unapitia sikonge, ipole, inyonga hadi mpanda,
 
Aisee Kigoma walio wengi hawamuelewi huyo hangaya na wanamchukia kweli kweli,,maana huku 98% ni wakulima na wanategemea kilimo kama mkomboz wao.Kilo 50 ya mbolea ni kuanzia 100k-120k,kwa hali hiyo wampende kisa umeme wa gridi ya taifa na wakati jenereta zao zinawapa umeme wa uhakika usio wa mgao
Sins hakika wewe pungu1 unaishi kgm au dunia gani naona hujui matumizi ya umeme unafikiri ni kuwasha taa nakuona tv kwamtu mwenye uwelewa hawezi tenganisha kilimo ,umeme na usafirishaji pia faham umeme ndio utaleta kiwanda cha mbolea ili ishuke kgm umeme utapandisha thamani yamazao yetu yote sikunyingine usiandike ujinga umeelewa?
 
Mkuu hakukua na haja ya kunitukana ungenielewesha tu ila shukrani sana
 
Ulicho kiandika hakiendani na maisha ya watu wa kigoma, 98%ya watu wa kigoma wanategemea kilimo kutoka pori moja linaitwa Kagera nkanda, huo ndio mgodi wao wa dhahabu but pori hilo limepigwa pin, na huwaambii kitu kuhusu pori hilo,
 
Mkuu kwani waliomtangulia huu haukuwa wajibu wao?
Umemjibu jibu fupi lakini lilioenda degrees. Kwa sababu, watu wanaisifu awamu ya 5 kama vile miradi yote kaianza yeye na kuitekeleza. Kwa mfano, SGR, fly over ya TAZARA na Ubungo viliasisiwa awamu ya 4. Lakini ibada zote Ni kwa awamu ya 5 kama vile mtangulizi wake hakufanya kitu. Tukumbuke hizi awamu zinategemeana as if a chain. Juhudi za kila awamu zitambuliwe na tuache ushabiki wenye chuki binafsi
 
Hivi hawa wanaojipendekeza kutoa sifa kwa viongozi kwa kufanya mambo fulani, wakati ni wajibu wao kufanya wanayoyafnaya; Je, wanatumwa au wanajituma wenyewe?
Cc: Aliye anzisha uzi huu.
 
Wakati Taifa likielekea kupokea Jumla ya Mega Watt 2,115 kutoka kwenye bwawa la JNHPP kwenda kwenye gridi ya Taifa ya Umeme Kigoma na Katavi bado walikuwa wanaongelea habari za umeme wa sola na majenereta,

Watu Wakigoma na Katavi ilikuwa ni hadithi ngeni kuwaambia watapokea mwekezaji yoyote toka nje au ndani wa kuanzisha kiwanda kwani Duniani kote sina hakika kama kuna kiwanda kinaweza kuendeshwa kwa Umeme wa Genereta au sola kwa ufanisi,

Wakati flani watu wa Kigoma na Katavi walipata mashaka kama na wao ni wana wa Tanzania kwani kwa kukosa kwao umeme wa gridi miaka 60 ya Uhuru kuliwatoa imani kwamba na wao ni Watanzania kama wenzao hoja ambayo leo Rais Samia anaijibu kwa vitendo,

Kwa mujibu wa meneja mkuu wa Shirika tanzu la TANESCO yaani Electrical Transmission and Distribution Construction Service Provider (ETDCO), Maclean Mbonile tayari Rais Samia anatekeleza mradi wa kupeleka umeme Kigoma na Katavi wenye Jumla ya Kilometa 776.

Umeme huu utatoka Tabora kwenda Mpanda na Tabora kwenda Kigoma kwa kilometa 383 na 393 kilometa kila moja kwa thamani ya TZS 15.9BL.

Mtakumbuka mradi huu ni miongoni mwamiradi 15 ya Mama Samia inayogharimu Jumla ya TZS151.48BL zilizokwisha kutolewa,

#Kigoma & Katavi hamkupata Umeme wa gridi tangu Uhuru,Kwani leo mnasemaje kuhusu Rais Samia ?

View attachment 2025434
Samia sio wa Nchi hii ni WA viwango vya mbele huko.

Sio tuu Katavi na Kigoma bali hata kwenye sekta ya Afya Nchi nzima..Soma utekelezaji wa ujenzi vituo vya afya 221 kwa mpiga kwa mwaka huu tuu 👇

Screenshot_20211127-185918.png
 
Back
Top Bottom