Rais Samia Suluhu awasili Kenya, aweka kidole Mkataba wa Bomba la gesi Dar-Mombasa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini leo tarehe 04 Mei, 2021 kuelekea nchini Kenya ambako anafanya Ziara Rasmi ya siku 2 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta.

#KaziIendelee
======




Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amewasili nchini Kenya na kupokelewa uwanja wa ndege na Waziri wa Mambo ya Nje ya Kenya, Balozi Amina Mohammed. Rais Samia amefika eneo la VIP uwanjani hapo na punde anaenda Ikulu ya Kenya na leo atafanya mazungumzo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Saa 11: 10 Asubuhi: Rais Samia Suluhu amefika Ikulu ya Kenya na kulakiwa na Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta kisha kumtambulisha kwa viongozi kadhaa ikiwemo wa Kijeshi na Polisi. Kinachoendelea sasa ni nyimbo za mataifa mawili.

11:16 Asubuhi: Sasa inapigwa mizinga 21 kwa Rais Samia Suluhu kama Rais mgeni aliyezuru nchi hiyo na baada ya tukio hilo atafanya mazungumzo na Rais wa Kenya.

=======

Kenyatta: Tumepata nafasi ya kuongea mambo mbalimbali, tumekubaliana ya kwamba tutare-energize ile joint commission of cooperation kati ya nchi zetu mbili na mawaziri wetu wameambiwa kwamba wawe wanakutana mara kwa mara kuhakikisha ya kwamba wanaendelea kuzingatia uhusiano wetu na kuweza kutatua shida ndogondogo ambazo zinasumbua wananchi wetu wakati wanafanya biashara kati yao, wakati wanatembeleana kati yao.

Tumepata nafasi ya kuongea mambo mengi ya muhimu pia mambo ya usalama wa nchi zetu na watu wetu na vile tutasaidiana kuhakikisha tuko na usalama kati yetu, kati ya wananchi wetu hasw tukielekeza mambo ya kupambana na ugaidi katika sehemu zetu.

Tumekubaliana pia ya kwamba na kuweka mkataba haswa ya mambo kuhusu kujenga pipeline ya gas kutoka Dar es Salaam mpaka Mombasa na hiyo itarahisisha bei ya stima katika nchi yetu na itasaidia pia kuhakikisha ya kwamba viwanda vyetu industries zetu zinapata Stima na energy ambayo ni environmental friendly.

Rais Samia Suluhu: Tumepokewa vizuri sana njiani, muda mfupi uliopita tumetoka kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta, tuemjadili mambo mengi kama alivyosema mwenyewe. Ninalotaka kuliweka msisitizo ni lile linalohusu kukuza na kuimarisha mahusiano kati ya mataifa yetu mawili na hili ndio jambo msingi.

Tanzania na Kenya sio tu ni majirani lakini ujirani wenyewe ni wa kindugu, alisema pia, ukiangalia mipaka inayozunguka Kenya, mpaka wao na Tanzania ndio mkubwa kuliko mipaka ya nchi nyingine zote lakini kwenye mpaka huo, wale wanaaoishi mipakani wako Tanzania, wako Kenya nao wote ni ndugu, kwahiyo uhusiano wetu ni wa kindugu.

Wakati wa mazungumzo yetu, nimemuarifu kaka yangu Rais Kenyatta kuwa Kenya inashika nafasi ya tano kwa uwekezaji ndani ya nchi ya Tanzania ikitanguliwa na mataifa mengi kutoka nje lakini ndani ya jumuiya ya Afrika mashariki, Kenya ni ya kwanza na kiulimwengu inashika nafasi ya tano ambapo imewekeza miradi 513 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.7 ambayo imetoa ajira zipatazo 51 elfu za watanzania.

Zipo kampuni 30 za kitanzania ambazo zimewekeza mtaji ndani ya Kenya wenye thamani ya shilingi za Kenya 19,330,000,000 na kutoa ajira kwa watu 2,640 lakini nikaweka ahadi kwamba Tanzania sasa tutakuja kwa nguvu yote Kenya kuja kuwekeza ili kukuza ujazo wa biashara.

Kwenye miaka mitano iliyopita wastani wa biashara kati ya Tanzania na Kenya ni Shs trilioni moja za kitanzania ambayo bado sio kubwa na tumeweka ahadi kuikuza hivyo katika mazungumzo yetu tumekubaliana kuhusu namna ya kukuza biashara na uwekezaji kati yetu kama mnavyofahamu nchi zetu bado zina fursa nyingi sana.

Lengine aliliongoza mheshimiwa Rais nami nakubaliana nalo, ni kwa mawaziri wetu wa afya kukaa, kuangalia na kurahisisha mfumo wa kuingia na kuchekiwa kwenye mambo haya yaliyoingia ya Covid au Corona, watu wetu wapate huduma za haraka, Kupima na kuchekiwa ili waweze kupita na biashara ziendelee.

Tumegusia pia suala la ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa, huu ni mradi wa muda mrefu, tunashukuru leo tumeweka kidole na kilichobaki ni utekelezaji, tutakwenda kusimamia.

Mwisho ni kwa taarifa yenu waandishi wa habari, mwaka huu ifikapo mwezi December, Tanzania tunatimiza miaka 60 ya uhuru wetu na hivyo nimetoa mwaliko rasmi kwa Rais Uhuru Kenyatta awe mgeni rasmi katika maadhimisho yale ya miaka 60 ya uhuru wetu.

k0.jpg

Samia Suluhu Kenya.jpg

4.jpg

1.jpg

2.jpg
3.jpg



K1.jpg
k2.jpg


 
Naona sasa ni mwendo wa kupukuchulia rasilimali za nchi yetu angani; sasa zile harakati za kupishana angani zinanyemelea. Bi Mkubwa hasomeki, kurasa za hotuba na ahadi zake zimefutika.

#Mtanikumbuka kwa mema, na wala si kwa mabaya.
Wivu tu, Mwendazake alikuwa na Tatizo la Moyo sio kwamba alikuwa hapendi kusafiri.

Fikiria ule msafara wake wa magari zaidi mia moja na zote zina watu, zile gharama zake si ni zaidi ya ya Safari ya Ndege kwenda Kenya?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Wivu tu, Mwendazake alikuwa na Tatizo la Moyo sio kwamba alikuwa hapendi kusafiri.

Fikiria ule msafara wake wa magari zaidi mia moja na zote zina watu, zile gharama zake si ni zaidi ya ya Safari ya Ndege kwenda Kenya?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app


Wewe ni muongo sana; nadhani baada ya Profesa Muongo, anafuatia wewe.
 
Sasa raisi kurukuu imehusu nini,jamani si atoe mkono tu ule wa bye ingetosha lakini ana style ambayo ya ajabu kidogo na inawalakin.
 
Rais Samia amewasili jijini Nairobi muda huu kuanza rasmi ziara yake ya siku mbili.

Tukio liko mubashara katika local channels zote.

Kazi Iendelee!
 
Naona sasa ni mwendo wa kupukuchulia angani rasilimali za nchi yetu; sasa zile harakati za kupishana angani zinanyemelea baada ya kuzinduliwa rasmi pale kwa M7. Bi Mkubwa hasomeki, kurasa za hotuba na ahadi zake tifutifu & futefute zimefutika.

#Mtanikumbuka kwa mema, na wala si kwa mabaya.
Sogea Chato ukapalilie kaburi, acha kulialia.. Rais lazima azunguke kulitafutia taifa maendeleo.. sio kujifungia ndani kishamba na kukwapua hela za mifuko ya jamii na hela za wafanyabiashara wakubwa.
 
Wewe umeanzisha thread ya rais kuondoka, akishafika Nairobi, mwingine naye aanzishe thread? Hapo Kenya siyo mbali, ungesubiri afike halafu uweke na hiyo picha ya wakati anaondoka.
Nimekaa nikitafakari hapo kwenye andiko la huyu mtu 'kuondoka' mara paap 'kafika' nikashangaa sana 😬, hawa wapachika mada sijui ni kizazi gani na mods wanaangalia tu utadhani hawapo!.
 
Naona sasa ni mwendo wa kupukuchulia angani rasilimali za nchi yetu; sasa zile harakati za kupishana angani zinanyemelea baada ya kuzinduliwa rasmi pale kwa M7. Bi Mkubwa hasomeki, kurasa za hotuba na ahadi zake tifutifu & futefute zimefutika.

#Mtanikumbuka kwa mema, na wala si kwa mabaya.
It's true,mwacheni mwendazake apumzike,na tumwombee apite purgatory kwa amani,maana hapo ndipo pagumu kweli kupita.
*hufanikiwi kupita hapa kwa maombi ya walio hai,hapo unapita kwa wema na uzuri ulioufanya duniani.
 
Back
Top Bottom