Rais Samia Suluhu awasili Dar es Salaam akitokea Jijini Dodoma

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,156
4,510
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani amewasili Jijini Dar es Salaam kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na amepokelewa na Waziri Mkuu Mhesh Kassimu Majaliwa pamoja na Viongozi wengine wa Serikali.

s1.jpg

s2.jpg

Mama Samia atazungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam jioni ya leo katika Ukumbi wa Mlimani City.
 
Wazee ni hazina kubwa na Mama Samia Suluhu Hassan yupo sahihi kabisa kuongea nao kwa minajiri ya kuvuna busara na hekima zao.

Hongera sana Mama kwa busara na hekima zako na Mwenyezi Mungu inshalah akufanyie wepesi katika majukumu yako ya kulitumikia taifa
 
Vijana wa Dar pia tukumbwe tuna jambo letu. Pango la mageto liko juu sana hadi tunakosa pesa ya chips na miguu ya kuku mida ya jioni.
 
Anapokelewaje na Kasimu. Kwani si anatakiwa awe Dodoma huyu bwana Kasimu.
 
Mama namkubali sana, nipo attention nikisubiri hotuba zake ambazo huwezi ukachoka kuzisikiliza, i lov you my beloved president.
 
Tatizo mama anaenda kuwajibu kina

Bashir Yakub
Chige
thetallest

Na wengine. Mama hawa watu 'wapogo' tu tafadhali wasikunyime usingizi. Piga kazi na jiepushe sana kuwajibu watu wa mitandaoni. By the way, tunaokuunga mkono na tunaopenda upewe nafasi ufanye kazi kwa nafasi na kwa weledi wako tuko wengi kuliko hao wababaishaji
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom