Rais Samia Suluhu anahujumiwa kwenye utawala wake?

Babe la mji

JF-Expert Member
Dec 14, 2019
983
2,053
Ukiangalia utawala wa Rais wetu kwa makini utagundua kabisa kuna nguvu nyuma ya pazia inayompa shinikizo kuhusu maamuzi anayoifanya hasa kuhusu mambo ya uchumi.

Alianza kwa kuongezea makato kwenye miamala ya simu hali iliyozua tafulani kwa Wananchi wake wakati ilitakiwa kupunguzwa kwa Sababu ya COVID 19.

Matokeo yake Wananchi ndiyo wanaumia yeye ni kama hajali,Lengo tuliambiwa ni tozo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa lakini badae serikali ikapata mkopo World Bank kwa ajili ya huo ujenzi ajabu Bado tozo zipo

Bidhaa zinapanda Bei Kila kukicha lakini mkuu wa nchi haonyeshi kujali yeye Kila siku ni kisisistiza bidhaa itendelea tu kipanda kisa na mkasa ni vita ya Ukrein na Urusi na inaonekana serikali Haina hata mpango wa kuzibiti bidhaa isipande Zaidi ya hapo .

Mafuta ya kula,ngano,sabuni ni Kaa la moto kwa maisha ya Wananchi wa kawaida.

Jana kaludisha tena sh 100 kwenye tozo ya mafuta manake ameluhusu mafuta yapande zaidi Sasa hapo anawasaidia Wananchi au anazidi kuwaumiza.

Lengo la serikali Zote Duniani ni kuwawezesha Wananchi wao waishi vizuri lakini kinyume na matalajio watawala wa Tanzania ni kama hawawajali Wananchi wao.

Je, anahujumiwa au anajihujumi mwenyewe.
 
Anajihujumu mwenyewe. Ikiwa keshajijua yeye ni raisi kwanini kuwe na watu wa nyuma ya pazia.

Tatizo anakurupuka katika kufanya mambo bila ya research za kina kupelekea kutoa na kutengua kauli zake kila kukicha. Leo anasema hiki kesho anatengua.

Pia anajaribu sana kufanya kila jambo kwa kujilinganisha na Magufuli kusahau kuwa wao ni watu wawili tofauti na kila mtu ana upeo na uwezo wake wa kufanya mambo. Akiacha kufanya maamuzi kwa kutaka 'ku prove' kwa watu kuwa yeye ni mwanamke na 'anaweza' basi kwa hakika atafika mbali.

Mwisho aangalie kauli zake sana, hizo ndizo zinazomuhujumu. Aidha kwa makusudi tu au kutokujua, huwa anatoa kauli ambazo baadae zinakuja kugharimu taifa.

Ikiwa kama raisi kuna baadhi ya kauli unapaswa kuziepuka maana zinatoa mianya kwa wazee wa fursa kuumiza wananchi. Anaporudia kila mara kuwa vitu vitapanda bei (hata kama ni kweli) na kutaja kabisa sekta kama usafiri, anatarajia nini zaidi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri vya biashara kupandisha nauli hata kama hawakuwa na dhamira hiyo. Hii ni sawa na kauli ya kusema viongozi wale kwa urefu wa kamba zao, inawekana dhamira yake ilikuwa njema lakini kupitia chaguzi duni ya maneno yake watu wametafsiri tofauti na baadhi kwenda mbali zaidi na 'kula kwa urefu wa kamba zao'.
 
Sasa anahujumiwa na nani ikiwa wale aliosema hawaendi vizuri aliwatoa.

Ukiona watu wanakueleza Jambo la kipumbavu na ukakubaliana nalo, basi jua kuwa.
 
Anajihujumu mwenyewe. Ikiwa keshajijua yeye ni raisi kwanini kuwe na watu wa nyuma ya pazia.

Tatizo anakurupuka katika kufanya mambo bila ya research za kina kupelekea kutoa na kutengua kauli zake kila kukicha. Leo anasema hiki kesho anatengua...
Subiri wazee wa mama anaupiga mwingi waje kukushukia.
 
Wakati wenzetu wanapambana kutatua changamoto za uchumi zilizosababishwa na vita ya Ukraine huku kwetu Mapaka yanatutangazia kuwa maisha yatakuwa magumu kutokana na vita hiyo.

Wajibu wa viongozi ni kutatua changamoto katika Taifa na siyo kutangazia uma kuwa maisha yatakuwa magumu kutokana na changamoto.Nitaendelea kuimba kuwa Tanzania inaongozwa na vibaka.
AARD4K.jpeg
 
Ukiangalia utawala wa Rais wetu kwa makini utagundua kabisa kuna nguvu nyuma ya pazia inayompa shinikizo kuhusu maamuzi anayoifanya hasa kuhusu mambo ya uchumi .

Alianza kwa kuongezea makato kwenye miamala ya simu hali iliyozua tafulani kwa Wananchi wake wakati ilitakiwa kupunguzwa kwa Sababu ya COVID 19.

Matokeo yake Wananchi ndiyo wanaumia yeye ni kama hajali,Lengo tuliambiwa ni tozo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa lakini badae serikali ikapata mkopo World Bank kwa ajili ya huo ujenzi ajabu Bado tozo zipo

Bidhaa zinapanda Bei Kila kukicha lakini mkuu wa nchi haonyeshi kujali yeye Kila siku ni kisisistiza bidhaa itendelea tu kipanda kisa na mkasa ni vita ya Ukrein na Urusi na inaonekana serikali Haina hata mpango wa kuzibiti bidhaa isipande Zaidi ya hapo .

Mafuta ya kula,ngano,sabuni ni Kaa la moto kwa maisha ya Wananchi wa kawaida .

Jana kaludisha tena sh 100 kwenye tozo ya mafuta manake ameluhusu mafuta yapande zaidi Sasa hapo anawasaidia Wananchi au anazidi kuwaumiza .

Lengo la serikali Zote Duniani ni kuwawezesha Wananchi wao waishi vizuri lakini kinyume na matalajio watawala wa Tanzania ni kama hawawajali Wananchi wao.

Je, anahujumiwa au anajihujumi mwenyewe.
Fanya kazi kijana ni muda wa kazi huu.
 
Wakati wenzetu wanapambana kutatua changamoto za uchumi zilizosababishwa na vita ya Ukraine huku kwetu Mapaka yanatutangazia kuwa maisha yatakuwa magumu kutokana na vita hiyo.

Wajibu wa viongozi ni kutatua changamoto katika Taifa na siyo kutangazia uma kuwa maisha yatakuwa magumu kutokana na changamoto.Nitaendelea kuimba kuwa Tanzania inaongozwa na vibaka.
View attachment 2170193
Inashangaza sn mafuta yakipanda bei yanapatikana kwa wingi yakishuka bei upatikanaji inakuwa shida
 
Ukiangalia utawala wa Rais wetu kwa makini utagundua kabisa kuna nguvu nyuma ya pazia inayompa shinikizo kuhusu maamuzi anayoifanya hasa kuhusu mambo ya uchumi .

Alianza kwa kuongezea makato kwenye miamala ya simu hali iliyozua tafulani kwa Wananchi wake wakati ilitakiwa kupunguzwa kwa Sababu ya COVID 19.

Matokeo yake Wananchi ndiyo wanaumia yeye ni kama hajali,Lengo tuliambiwa ni tozo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa lakini badae serikali ikapata mkopo World Bank kwa ajili ya huo ujenzi ajabu Bado tozo zipo

Bidhaa zinapanda Bei Kila kukicha lakini mkuu wa nchi haonyeshi kujali yeye Kila siku ni kisisistiza bidhaa itendelea tu kipanda kisa na mkasa ni vita ya Ukrein na Urusi na inaonekana serikali Haina hata mpango wa kuzibiti bidhaa isipande Zaidi ya hapo .

Mafuta ya kula,ngano,sabuni ni Kaa la moto kwa maisha ya Wananchi wa kawaida .

Jana kaludisha tena sh 100 kwenye tozo ya mafuta manake ameluhusu mafuta yapande zaidi Sasa hapo anawasaidia Wananchi au anazidi kuwaumiza .

Lengo la serikali Zote Duniani ni kuwawezesha Wananchi wao waishi vizuri lakini kinyume na matalajio watawala wa Tanzania ni kama hawawajali Wananchi wao.

Je, anahujumiwa au anajihujumi mwenyewe.
Huyo ndio Mama Tozo wetu.
 
Kwa ujio wa kinana na membe ni wazi anahujumiwa matokeo tutayaona kwenye 2025 mama hatoboi
 
Back
Top Bottom