Rais Samia Suluhu amteua Rogatus Mativila kuwa Mtendaji Mkuu TANROADS. Prof. Mgaya wa NIMR awa Mwenyekiti Bodi ya TAFICO

Taarifa imeandikwa kiusahihi kabisa. " Prof. Mgaya NI ........." na siyo "alikuwa"
Hii ndio waliyotoa mwanzo
IMG-20210730-WA0016.jpg
 
Nchi hii vyeo vingi sana ukikosa kaa kwa kutulia, leo nimejua cheo kingine tena "mkurugenzi wa barabara na mkurugenzi wa wakala wa barabara" ni watu wawili tofauti.
 
Haieleweki. Uenyekiti wa bodi sio kazi ya kiutendaji kwa hiyo Profesa anaweza kuendelea tu na nafasi yake NIMR bila shida yeyote. Tafico ni kwa kuvutia posho za vikao.

Amandla...
Tafico ni kweli kuvutia posho za vikao......maana hawana meli hata moja zaidi ni Yale maghala chakavu kule pembeni ya chuo cha chama
 
Rais Samia Suluhu amemteua Rogatus Hussein Mativila kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)

Ndugu Mativila anza kufuatilia barabara hii ya njia 8 kuanzia kimara mwisho hadi kibaha.
hii barabara ni ya hadhi ya kipekee ambayo ukiachilia mbali kuwa kiungo cha Uchumi wa Jiji la Dsm lkn pia imeboresha muonekano wa Jiji la Dsm.
sasa chonde chonde tusisahau kuweka taa za barabarani ili kuboresha kazi nzuri iliyo fanyika, naamini kazi kubwa imefanyika hatuwezi kushindwa kuweka taa za barabarani.
Maendeleo hayana chama.
Mungu Mbariki hayati JPM, Mungu mbariki Rais Samia.
 
Back
Top Bottom