Rais Samia Suluhu ametoa moja ya hotuba bora sana, nina matumaini ataziba nyufa nyingi za utawala uliopita

Nina moja tu: Kuinamisha kichwa siyo udhaifu. Kuinamisha kichwa ni alama ya unyeyekevu ambayo anatakiwa awe nayo kila kiongozi.

Inasikitisha wabongo tumezoea viongozi wenye viburi na kujikweza kiasi ambacho ukimwona anayenyenyekea unamwona kama ni mjinga. Hili la kuinama ni zuri sana na aliendeleze.
Ahsante sana mkuu.
Sijui hawa jamaa wamepata wapi hili wazo na kulifanya kana kwamba ni jambo muhimu sana.

Afanye kazi yake vizuri tu, na kila kiongozi na watu wataheshimu kazi zake.
 
Let Samia be Samia, do not try and recreate her into something she is not.

She was not a President then ; now she has to reinvent herself, she has no choice! Huyu sio Samia wa zamani , huyu ni Rais Samia Hassan kwahiyo kuna tofauti kubwa sana!!
 
She was not a President then ; now she has to reinvent herself, she has no choice! Huyu sio Samia wa zamani , huyu ni Rais Samia Hassan kwahiyo kuna tofauti kubwa sana!!
Re-inventing herself does not mean wearing makeup.
Whether she is President or not, she is intrinsically a person with characteristics that make her who she is.

Next time you're going to suggest she changes her voice tone, because now she is president!
 
Umesema kweli, hata hivo urafiki wa Kenya na Tanzania haujawahi kutokuwa wa mashaka tangu enzi.

Labda mama atabadili huu upepo. Ngoja tuone
Ni makosa makubwa kuitegemea Kenya kama mshirika muhimu kwetu.
Mwingiliano nao unaonyeshwa na njia kuu za kuingilia kati ya nchi hizi mbili - zipo kama nne hivi: Sirari, Namanga, Holili, Holoholo; na barabara zetu kuu kwenda nje zinaelekea huko zaidi ya kwingine kokote. Na bado kuna barabara zinajengwa, kama ile ya kuambaa pwani tokea Kilifi hadi Bagamoyo!

Tunazo barabara ngapi kati ya Uganda na sisi; au Zambia na sisi; Burundi na DRC ,je, hawa sio majirani zetu tunaotaka tushirikiane na kufanya nao biashara?

Ni wakati sasa tuweke mkazo kwa majirani zetu wengine.

Ni juzi tu tumeona tatizo kubwa la kutegemea nchi moja kwa biashara ya mahindi ya wakulima wetu.
 
Umesema kweli, hata hivo urafiki wa Kenya na Tanzania haujawahi kutokuwa wa mashaka tangu enzi.
Inawezekana una maana nisiyoielewa kuhusu "urafiki kutokuwa wa mashaka tangu enzi."

Hili linaweza kuwa mjadala mwingine kabisa nje ya hii mada yako uliyoianzisha hapa.

N.B. Nadhani nimekusoma sivyo: Umeandika "KUTOKUWA"; samahani, sikuliona neno hilo nilipojibu.
"....haujawahi kutokuwa..." Ninakubaliana nawe.
 
Next time you're going to suggest she changes her voice tone, because now she is president!

Don't you know that when people ascend to certain positions ,they undergo certain rituals including the art of PUBLIC SPEAKING? Give her time you will notice the changes she will undergo by virtue of her Presidential position. Ndio maana nimewaambia Rais Samia wa leo sio yule wa jana kwani anabadilika kufuatana na uzito wa majukumu anayobeba sasa. SHE IS ALSO THE COMMADER OF OUR ARMED FORCES NOW!
 
Nahifadhi comment Hii Ili nione Kama utabadilisha kauli yako miezi mitano kuanzia Sasa....hahahaha
Mimi nipo straight na tayari kwenda na beat yeyote inayopigwa.. akizengua lazima nimkosea tena nimkosoe vikali sana
 
Inawezekana una maana nisiyoielewa kuhusu "urafiki kutokuwa wa mashaka tangu enzi."

Hili linaweza kuwa mjadala mwingine kabisa nje ya hii mada yako uliyoianzisha hapa.

N.B. Nadhani nimekusoma sivyo: Umeandika "KUTOKUWA"; samahani, sikuliona neno hilo nilipojibu.
"....haujawahi kutokuwa..." Ninakubaliana nawe.
Tanzania na Kenya tuna upinzani wa asili... ila hiyo pia haizui kuwa na uhusiano mzuri.. Kikubwa ni kwamba tuwe tumefungua macho kila wakati ndo tutaweza kwenda sawa na wakenya.
 
Don't you know that when people ascend to certain positions ,they undergo certain rituals including the art of PUBLIC SPEAKING? Give her time you will notice the changes she will undergo by virtue of her Presidential position. Ndio maana nimewaambia Rais Samia wa leo sio yule wa jana kwani anabadilika kufuatana na uzito wa majukumu anayobeba sasa.
Nakubaliana na wewe... uongozi utamshape baadhi ya tabia.. hata alivoapa wiki iliyopita na leo.. unaona tofauti kubwa sana..

Mimi kwa sasa naona jambo moja tu la kubadilika kwa haraka ni kwenye kutoa salamu kwa viongozi wenzake..

' Asiinamishe tena kichwa' ... ' Leaders dont bow' .. sijui kama nimepatia..
 
Asiinamishe tena kichwa' ... ' Leaders dont bow' .. sijui kama nimepatia.

Mimi sina matatizo akifanya hivyo akiwa hapa nyumbani. Akiwa kwenye International Arena ,it is a different ball game because she will be playing on the International stage. Sijaona clips zake akiwa nje ya nchi alipokuwa anamuwakilisha marehemu, maybe her posture was different! I have every reason to be believe that she is a fast learner.
 
Don't you know that when people ascend to certain positions ,they undergo certain rituals including the art of PUBLIC SPEAKING? Give her time you will notice the changes she will undergo by virtue of her Presidential position. Ndio maana nimewaambia Rais Samia wa leo sio yule wa jana kwani anabadilika kufuatana na uzito wa majukumu anayobeba sasa.
Hakuna anayekataa kubadilika kwa mtu kutokana na majukumu.

Kwa mtu halisi habadiliki tabia yake; labda kui-'reinforce' tu basi, lakini tabia haibadiliki.
 
Tanzania na Kenya tuna upinzani wa asili... ila hiyo pia haizui kuwa na uhusiano mzuri.. Kikubwa ni kwamba tuwe tumefungua macho kila wakati ndo tutaweza kwenda sawa na wakenya.
'Credit' mpe yeyote anayeistahiri hata kama kuna baadhi ya mambo aliyoyafanya hukuyapenda.

Tanzania ya Magufuli ilianza "kwenda sawa na wakenya," na hata wao walianza kuona 'inevitability' ya kufanya hivyo.
 
Kwa mtu halisi habadiliki tabia yake; labda kui-'reinforce' tu basi, lakini tabia haibadiliki
Sikubaliani na taswila yako kuwa mtu hawezi kubadili tabia yake ! Human beings are inherently flexible .
 
1. Uhusiano na nchi majirani - Haukua mzuri, na hususani uhusiano na jirani yetu Kenya ambaye tuna muingiliano mkubwa sana wa kibiashara na kijamii kuliko majirani wetu wote. Ila kwa namna ya namna alivotoa hotuba yake, nna imani sana kwamba ataboresha na kuponya haya mahusiano na majirani. Na sio Kenya tu, hata wale ambao walibatizwa kwamba ni 'mebeberu' nadhani Madam President ni kama amefungua mkono kupitia hotuba yake kitu ambacho ni kizuri.

2. Umoja wa kitaifa - amegusia pia kwenye hotuba yake na nadhani ni jambo jema, maana taifa tulishafika mahali pabaya sana

Cha mwisho ni kumshauri tu, aache mara moja kuinamisha kichwa kwa heshima, Rais unatakiwa u express Authority kila dakika, so sijapendezwa na akisalimiwa kila saa anainamisha kichwa, awe straight kila saa hata akisalimiwa.

Namba 1 inategemea sana na kenya. JPM alikuwa aemejenga uhusiano muzuri sana na Kenya, aliwatembelea, wakamtembelea na vile vile aliwapa Tauz, wakaja kuomba kununua mahindi, na kurudisha dhahabu zetu na pesa zilizokuwa zimetoroshewa huko siku za nyuma. Zaidi ya yote, alimpeleka Palamagamba kusimamia maafikiano ya yao na akawapo uhusia mzuri sana. Sidhani kama Samia atafanya zaidi ya effort aliyofanya JPM. Mwisho wa yote, itategemea sana iwapo kenya wanareciprocate. kenya walikataza ndege za Tanzania kuingia kwao, JPM naye akfanya hivyo hivyo kuwa ndege za kenya sissingie Tanzania. Kwa hiyo kufuatia ushauri ulitoa hapo mwishoini, ni lazima na yeye aonyeshe kuwa ana authority iwapo Kenya wakileta vya kuleta, na yeye anatoa vya kutoa.

Namba-2 nina mashaka sana na unavyoweza kuwa unatafasiri maana ya umoja wa kitaifa. Wahubiri wenge wa sera za umoja wa kitaifa ni kwa kwa serikali kushirikiana na vyama vya upinzania kwa lolote lile. JPM aliwatambuwa awatu wa vyama vya upinzani kwa kulingana na maono yake, akawapa vyeo baadhi yao lakini viongozi wengine ambao hawakuepwa vyeo hivyo walikuwa na falsafa ya kupinga kila kitu, hata yale waliyokuwa wanakubali zamani, baada ya JPM kuyagusa wakayageuka na kuyapinga. Kwa falsafa hiyo ya kupinga kile kitu, au kutafuta neno la kufanyia siasa, sidhani kama Samia atakubaliana nalo iwapo atafuata ushauri ulimpa hapo mwisho kuwa ni lazima aproject authority.

Ushauri wako uliompa kuwa ni wa maisho, nadhani ndio ushauri wa kwanza kabisa na wa muhimu sana. Yeye sasa niye amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya Tanzaniia; ana authority kubwa sana, na ni lazima afanye hivyo kwa kuonyesha kuwa mara zote yeye ndiye anayepiga kipenga cha mwisho, na akishapuliza kusiwe na longo longo tena.
 
Mama Samia should learn to look people in the eye ; that is a sign of strength!!! Rais hutakiwi kuonekana mnyonge; kwani una dhamana ya watu million 60 na Ardhi yote ya nchi!! Rais chukua ushauri lakini Sio lazima uufuate, uamuzi ni wako kwani wewe ndio muwajibikaji.
Nakazia hapa.
 
Binafsi nilikuwa na mashaka na namna atavolimiliki jukwaa mbele ya viongozi wabobezi na malegandary wa siasa za kusini mwa Afrika. Ila ukweli kabisa nimeridhika, kwa hotuba ya leo nampa maksi 97% hizo maksi 3% nilizomnyima ni makosa madogo madogo ambayo nadhani yanachangiwa na ugeni na ukifananisha pia kwamba amekula kiapo cha urais siku tano zilizopita, ila kwa ujumla ametoa hotuba ambayo naweza sema kwa ubora imewazidi watangulizi wake na kupitia hotuba hii, nimenusa kwa mbali mwelekeo wa itikadi wa serikali ya Madam President na nimeridhika kwamba utaweza kufanikiwa sana kwenye baadhi ya maeneo ambayo utawala wa Hayati JPM uliboronga.

Kwa ufupi, mambo makubwa niliyoyaona kutoka kwenye hotuba ya leo ni haya

1. Uhusiano na nchi majirani - Haukua mzuri, na hususani uhusiano na jirani yetu Kenya ambaye tuna muingiliano mkubwa sana wa kibiashara na kijamii kuliko majirani wetu wote. Ila kwa namna ya namna alivotoa hotuba yake, nna imani sana kwamba ataboresha na kuponya haya mahusiano na majirani. Na sio Kenya tu, hata wale ambao walibatizwa kwamba ni 'mebeberu' nadhani Madam President ni kama amefungua mkono kupitia hotuba yake kitu ambacho ni kizuri.

2. Umoja wa kitaifa - amegusia pia kwenye hotuba yake na nadhani ni jambo jema, maana taifa tulishafika mahali pabaya sana

3. Moyo wa kuendeleza yale mazuri ya mtangulizi wake Hayati JPM - Hapa pia nimefurahi kuona kwamba amerithi mtizamo wa JPM kuhusu kuendeleza miundo mbinu, Hili ni jambo bora pia, kwa sababu naamini kwamba Magufuli kuna mahali alifanya vizuri na panastahili kuendelezwa, na nimefurahi kwa yeye kututhibitishia hilo.

4. Kusikiliza ushauri wa viongozi waliomtangulia - hii point nyngine ambayo naona imempa credit kubwa sana, maana technically viongozi waliopita wanaifahamu hii nchi vema na sio mbaya kuchukua ushauri kwao, japokuwa ninaamini itabidi kwanza awe ana mtizamo wake kwanza kabla ya kupokea ushauri ili asiingie kwenye hatari ya kuonekana ni kiongozi asiyeamua kwa akili yake.

Binafsi haya ni machache niliyoona kwenye hotuba ya leo, na kwa kweli nimeyafurahia kwa Madam President, na hili ni angalizo natoa. Madam President anaweza kufanya wonders kama atasimamia alichohutubia leo, na niseme tu wazi, anaweza kutawala mpaka 2030!...

Kwa hotuba ya leo, hata wale waliokuwa wanapiga ramli za ndoto za urais 2025, watakuwa wamaogopa sana. Angalia body language ya Mwinyi wakati Madam President anamaliza hotuba yake, hakika utaona kabisa ametiwa uwoga fulani. Ni kama leo viongozi wengi hawakutegemea kama Madam President angetoa speech ambayo ipo authoritative kiasi hicho.

Cha mwisho ni kumshauri tu, aache mara moja kuinamisha kichwa kwa heshima, Rais unatakiwa u express Authority kila dakika, so sijapendezwa na akisalimiwa kila saa anainamisha kichwa, awe straight kila saa hata akisalimiwa.

Nawasilisha
N.Mushi
Anainamisha kichwa kama ishara ya kutojikweza Mkuu. Kuna Mtawala na Kiongozi...
 
Ndio maana watu wanashauri amrudishe Asha Rose Mtengeti toka London aje amsaidie mambo mengí huku nyumbani.

The potential in Mama Samia's leadership is infinite and with a strong cabinet , the people of Tanzania will be surprised by what she is going to accomplish!!

Nilikuwa na wasiwasi sana kuwa mafisadi wanaweza kumyumbisha kwa kumuwekea mtu wao kama makamu wa Rais ili warudishe wizi wao wa maliasili za nchi; lakini nilifarijika baada ya Mzee Mangulla kuhakikishia kuwa watu wasiwe na wasiwasi, nikaona Kikwete na NCHIMBI wake hawana njia ya kutokea. Hizo fedha walizohonga wajumbe ziwe kama wametoa sadaka!!!
 
Back
Top Bottom