Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,641
- 22,240
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamala D. Harris, Makamu wa Rais wa Marekani, leo Aprili 15, 2022 katika Ikulu ya Washington DC Nchini Marekani.
"Utawala wetu umedhamiria kwa dhati kuimarisha ushirkiano na Tanzania na nchi za Kiafrika kwa ujumla" - Kamala Harris
“Nashukuru sana uwepo wangu hapa, nashukuru sana Makamu wa Rais kwa kunikaribisha hapa, hii ni mara yetu ya kwanza tunakutana, hivyo natumia nafasi hii kumpongeza Rais Joe Baden na wewe pia Makamu wa Rais kwa kushinda uchaguzi mwaka 2020,” – Rais Samia
“Tanzania tilikuwa tunafuatilia uchaguzi wenu, kwa mara ya kwanza kulikuwa na mwanamke katika nafasi ya kuwa Makamu wa Rais, hilo lilituvutia.
“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania naipongeza Serikali ya Marekani kwa msaada mkubwa wa maendeleo ambao mmekuwa mkitupatia kupitia USAID kwa miaka mingi hasa katika maendeleo ya kijamii,” Rais Samia.
“Kuhusu Covid-19, Nchi yangu ipo katika hali nzuri na imekuwa ikipata msaada kutoka Marekani, kuna chanzo zaidi ya dozi milioni tano ambazo tumepata kutoka Marekani.
“Kuhusu haki za binadamu na demokrasia, Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala hayo, ambapo tumefanya juhudi kubwa kuhakikisha kuna umoja, mshikamano na heshima kwa Watanzania wote,” Rais Samia.
"Kuhusu biashara na uwekezaji, tunajua tunatakiwa kutengeneza mazingira rafiki ya biashara, Serikali yangu inashirikiana na sekta binafsi, ninachoomba ni Marekani kushawishi sekta binafsi kuja Tanzania kufanya biashara na sisis, tunawakaribisha sana," Rais Samia.
“Napenda pia kukutaarifu Makamu Rais kuwa nikiwa hapa Marekani, nitazindua The Royal Tour ambayo ni programu inayolenga kuonesha uwezo wa Tanzania katika sekta za Utalii na Uwekezaji," Rais Samia.
“Kuichagua Marekani kuwa sehemu ya kufanya Uzinduzi si bahati mbaya, tulifanya hivyo makusudi, lengo ni kuufanya mradi uonekane duniani kote, ili watu wengi wafike Tanzania kutembea,” Rais Samia.
Hana habari kuwa Marekani ilikwisha kuwa na mgombea urais mwanamke na alifanya vizuri sana.
Wazungu huwa uchaguzi ukiisha hawapongezani ushindi.