Munnahumuu
Member
- Feb 6, 2018
- 34
- 17
Muna maneno mengi mno.Yaani hadi leo ukifuattilia kila mtu alilomwambia yaani utafikiri Rais hana akili kabisaaaa.Duuuh nyie ndo mlikuwaga wasumbufu kwa Mamonita darasani nyie aaaàah.Kulingana na katiba ya JMT(1977) inaelekeza kuwa ikitokea Rais aliepo madarakani akapatwa na tatizo ambalo litamfanya kua nje ya ofisi ikiwepo na kifo basi Makamu ataapishwa kua Rais wa JMT.
Hapa basi nafasi ya makamu itakua wazi na kwa taratibu Pia katiba inamuelekeza Rais achague Makamu wake HAPA NDIPO LENGO LANGU LIPO.
Mama Samia ijulikane anachukua majukumu makubwa ya kuongoza nchi tena ambayo haijawahi kuongozwa na Mwanamke.
Kitu ambacho Mheshimiwa Rais anatakiwa afikiri zaidi ni kuhusu makamu wake akifanya kosa hapo nahisi ataona miaka4 kama10,anatakiwa achague mtu ambae ndani ya chama ana influence pia anakubalika na wazee wa chama, hapo atakua anapumua vizuri na atakua na mzigo mmoja tu wa upinzani ila akichagua ambae hakubaliki ndani ya chama ajiandae kupata wakati mgumu kwenye chama pia kutoka kwa upinzani kwa sababu upinzani wenyewe ni known hata kama akifanya hivi watakosoa tu hio ndio kazi yao.
Kwa hio Mheshimiwa akipuyanga hapa kwisha habari yake°
#ALUTA CONTINUA
Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app