Rais Samia Suluhu aitaka Wizara ya Habari kuvifungulia Vyombo vya Habari vilivyofungiwa. Avitaka kufuata Sheria na Kanuni

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Rais Samia Suluhu ameiagiza Wizara ya Habari kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa, na kuhakikisha vinafuata sheria. Aidha, ameagiza sheria kanuni na adhabu ziwe wazi, ifahamike kosa fulani adhabu yake ni fulani, ili isionekane kuwa serikali inaminya uhuru wa habari.

Rais Samia amesema haya...

Wizara ya habari, mnapaswa kusimamia vyombo vya habari, nasikia kuna vyombo vya habari mmevifungia, vifungulieni lakini vifuate sheria na kanuni. Tusiwape mdomo mdomo wa kusema tunabinya uhuru wa habari na nataka kanuni ziwe wazi. Tusifungie tu kibabe

Samia.jpg
 
Hii serikali inaonekana itakuwa radhi kukosolewa na hapatakuwepo na kutishana bila sababu, muhimu watendaji wake wasije kumuangusha kama tunavyoona kwenye vifurushi vya simu.
Kuna faida kubwa sana katika kukosolewa kuliko kujiona mkamilifu na wengine wote hawajui kitu. Ukijiona mkamilifu na uhitaji kukosolewa gari likianza kwenda kombo utabakia wewe na gari lako, wale wote ambao walikuwa upande wako watakugeuka tu.

Faida moja wapo ya kukosoa ameiona juzi, kwa sababu kupitia Idara ya Vetting Mama yetu alilishwa tango pori kuwa Mwesiga mzee wa UDOSO anafaa kusimamia TPDC, lakini kupitia wakosoaji ambao kimsingi wanaitakia mema nchi hii waliona kabisa mwamba anaenda kuizamisha Taasisi.

Mama ameonesha njia na ni muungwana sana kukubali kusikia kutoka upande mwingine.
 
Wana JF

Uhuru wa vyombo vya habari taratibu unaanza kurudi. Raisi Samia leo ameagiza vyombo vyote vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe. Tusiruhusu maneno ya kwamba tunabada uhuru wa vyombo vya habari.

Aidha raisi ameagiza ya kuwa pamoja na kuvifungulia wizara ihakikishe ya kuwa vyombo vyote vya habari vinafuata sheria na adhabu bado siko pale pale.

Haki huinua Taifa
 
Hii serikali inaonekana itakuwa radhi kukosolewa na hapatakuwepo na kutishana bila sababu, muhimu watendaji wake wasije kumuangusha kama sasa tunavyoona kwenye vifurushi vya simu.
Hahahaaa hiyo ni namna ya kuanza yake tu, kwa tabia zenu si mtataka uhuru mpaka mmtoe ikuru?
 
Rais Samia Suluhu amesema vyombo vya habari ambavyo vilivyofungiwa vifunguliwe ila vifuate sheria.

Amesema mamlaka zinazohusika ziainishe kosa na kiwango cha adhabu kwa wale watakaokiuka sheria kanuni na taratibu za nchi katika kuendesha vyombo vyao vya habari na si kufungia tu kibabe.
Hapo sawa
 
Back
Top Bottom