Rais Samia suala la leseni kwa vijana wasio na ajira linaumiza sana. Serikali inavuna isichopanda, hili Jambo litazamwe upya!

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,903
Salaam Mama , Rais wa JMT

Awali ya yote nikupe Pole kwa majukumu ya kila siku unayokabiliana nayo!

Kwa vijana tulio wengi,, ambao hatujapata nafasi ya kuajiliwa katika serikali yako na Bado tunatozwa ada ya leseni kwa kila Mwaka kulingana na taaluma tulizosomea tunaumia sana!!

Just imagine,
a. Mtu umesoma mpaka chuo kwa gharama za mzazi wako, baada ya kuhitimu unarudi nyumbani na unaamua kutafuta kazi kulingana na taaluma yako unakosa , unaamua ujitolee bure ili kupata uzoefu na kuihandle elimu yako. Ikumbukwe kwa wakati huo wote serikali inakukata kiasi fulani kila Mwaka regardless ni jobless kama ada ya leseni na hauingizi hela yoyote!

b. Kulingana na uhaba wa nafas za kazi na ukosefu wa mitaji Kijana unaamua ufanye kazi nyinginezo Kama vile bodaboda, kukaanga chips, kuwa kibarua wa ujenzi nk, lakini Bado serikali inakukata kiasi fulani kwa Mwaka Kama Ada ya leseni regardless taaluma yako hauitumii ,na usipolipa unaandikiwa Deni.

Mh.Rais, Mama Samia hii haijakaa sawa na ni ukandamizwaji wa hali ya juu sana,, ni Kama serikali inavuna isichopanda!!

MAPENDEKEZO
Mh. Rais, Kulingana na uhaba wa ajira,, Serikali ingewatazama kwa jicho la huruma vijana wasio na ajira kulingana na taaluma walizosomea kwa habari ya malipo ya leseni;

1) Serikali isiwatoze vijana fedha ya leseni mpaka watakapoajiriwa,, ili Kijana alipe fedha ya leseni kupitia kipato chake anachoingiza!!

2) Kama plan 1, ni ngumu, Basi angalau Kijana asiye na ajira akatwe asilimia kidogo tu ya gharama nzima ya leseni

Mh. Rais na Wanabodi wote JF, naomba kuwakilisha
 
Mbona hujafunguka,hiyo leseni gani??
Kada ya afya mkuu,,, ni hatare sana,, Mimi Nina Deni la kutosha napunguza mdogo mdogo,, hata manurse na upande wa lab wote naskia ni hayo hayo
 
Ni wazo jema la kutakiwa kuangaliwa Vizuri kwa haraka iwezekanavyo
 
Kada ya afya mkuu,,, ni hatare sana,, Mimi Nina Deni la kutosha napunguza mdogo mdogo,, hata manurse na upande wa lab wote naskia ni hayo hayo
Hivi kama haupractise hamna option ya kwenda kuaitisha mpaka pale utakapoamua kufanya kazi kwa kutumia leseni?? Nauliza hivi sababu kwa mfano mawakili wanaruhusiwa kuaitisha practicing certificate kwa muda na wanakuwa wamesimamisha kabisa kudaiwa Ila wanapotaka kutumia leseni zao kufanya kazi wanahuisha jwa kulipia tu.

Kama hakuna hiyo option basi wanawaonea sana.
 
Unaongea na huyu huyu maza? Nakushauri tafuta mafanikio kwa njia nyingine na siyo hiyo maana kwasasa tupo busy na 2025
 
Hyo option hakuna,, na ndiyo maana huu uzi upo hewani
 
Unaongea na huyu huyu maza? Nakushauri tafuta mafanikio kwa njia nyingine na siyo hiyo maana kwasasa tupo busy na 2025
Mkuu,, Mimi kwa Sasa napiga inshu tofaut na medicine,, but sometimes Wananitumia Sms na email kunijuza kuwa nadaiwa huko!!

Sasa Deni limekuwa ni kubwa,, nimeona nlipe mdogo mdogo,, but this is not fair kabisaa ,,, naingiza hela kwa shughuli nyngne tofaut na medicine, but nakatwa hela ya license kila Mwaka na ajira inayohusiana na medicine sina
 
Back
Top Bottom