Rais Samia siyo kila Kitu cha Hayati Rais Dkt. Magufuli ni cha Kuigaiga tu, tulia nawe tengeneza 'Leadership Style' yako tafadhali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Yaani Mtangulizi wako Hayati Rais Dkt. Magufuli alianzisha tabia ya Kuvizia Wasanii wenye Majina makubwa nchini wakiwa 'on the Stage' wakitumbuiza na Kuwapigia Simu Kuwapongeza nawe Jana umeamua upite mule mule kwa Kumpigia Msanii wa Kike Nandy akiwa anatumbuiza Mkoani Dodoma na Kumpongeza pia.

Kama kweli mnapenda Kupigia Watu Simu na Kuwapongeza kwa Juhudi zao mbona hamtupigii Simu na akina GENTAMYCINE pamoja na JF Members hapa ambao 85% ya Michango ( Maudhui ) yetu yanasaidia sana nchi yako pamoja na Serikali nzima bila Kusahau na Taifa zima la Tanzania ili mtupongeze pia?

Wakati Mtangulizi wako Hayati Rais Dkt. Magufuli alipokuwa akilifanya hili sikuona Tija yake sana sana naona ni Upuuzi na Unafiki mtupu wa kutafuta 'Cheap Popularity' kwa Wasanii na Watanzania ambapo nawe tena umeliiga na najiuliza hapa huwa mnataka labda kutuma Ujumbe gani kwa Wasanii na Watanzania ambao Mimi GENTAMYCINE sijaujua bado?

Kidogo Simu yako ya Jana kwa Msanii Nandy ningeielewa na kuiona ina Umuhimu huo kama ingekuwa ni ya Kujibu Kero zao za Kimsingj ili ulipiga tu ili nawe uonekane unawajali na bahati hata Nandy mwenyewe badala ya Kutumia nafasi ile Kuwasilisha Changamoto za Wasanii Kiujumla Yeye alikuwa anafurahia tu kwa Kupigiwa Simu na Mheshimiwa Rais huku akiwa ameshikilia Simu Kiunyenyekevu na Kinidhamu utadhani Kaokota Jiwe la Dhahabu Mererani.

Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan najua katika Siku zako 100 Ofisini Ikulu jana Watanzania wengi wamekupongeza na Kukupamba ila Mimi GENTAMYCINE katika Salamu zangu za Siku 100 nimeona nizitumie katika Kukukosoa ( Kusema ) hasa juu ya Kuigaiga kila kilichokuwa kikifanywa na Hayati Rais Dkt. Magufuli na ni matumaini yangu hutoninunia bali utanielewa na kufanyia Kazi Ushauri wangu.

Tengeneza nawe Kitabu chako tukuka.
 
Yule jogoo ambaye mwendazake alipewa na yule babu naye katoroka,hapa chato siku ya nne anasakwa haonekani, legacy inabomolewa nje ndani, hajazalisha tetea hata moja
 
Mkuu, hahahah, kiuhalisia kuna vitu vingi sana ambavyo Mama asipokua makini atapotea zaidi hata ya mwendazake.

Na bahati mbaya zaidi watu wakimkosoa mama watu wanamtetea sana kwa kuangalia kuangalia kigezo cha jinsi yake na mara nyingine wanasema eti alikua hajajiandaa kua Raisi.

Kipindi cha mwendazake kulikua na MATAGA, lakini sasa kuna FEMINISTS.

But all in all, wacha tuendelee kunywa mtori nyama tutakutana nazo chini.
 
Kuna maneno Rais aliyatumia wakati anaongea na Nandy pale stejini na kubwa nililosikia toka kwake nI kutimiza kwake siku 100 akiwa Rais wa JMT, ndio akamwambia Nandy anafurahia uwepo wake Dodoma kwani umeendana na hiyo anniversary yake.

So inshort ilikuwa ni kiburudani zaidi, Samia anasherehekea siku zake 100, na Nandy akawa anawapa raha mashabiki wake, sasa kama hiyo tabia ataiendeleza mbele ya safari naona hapo ndipo patakuwa pakujiuliza kulikoni.
 
Mama hana uwezo wa kuongoza nchi rejea biblia as well as quran, wameeleza nn juu ya mwanamke kuongoza , sometimes abebwe tu ivyo ivyo
 
Kwaiyo Magufuli naye alifungua fursa za wawekezaji sio yeye aliyekuwa anawaita mabeberu na kutuaminisha sisi ni Dona Kantri? Hahahaha! Hii nchi inawatu wa ajabu sana.Mama yuko kwenye ukurasa wake na anafanya vizuri tu bottom line fursa zinakuja.
 
Back
Top Bottom