Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,797
- 11,959
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa Faragha (Retreat) wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha leo tarehe 02 Machi, 2023
RAIS SAMIA
“Kutofanyika kwa mikutano yenye lengo la kutoa maelekezo ya kiuongozi kumesababisha athari katika utendaji kazi wa Serikalini.
“Hii ni moja ya sababu ya kubadilishwa kwa viongozi mara kwa mara ili kuiepusha Serikali na fedheha ya kuwa na viongozi wanazifanya Wizara kuwa sehemu za marumbano na migawanyiko isiyo na tija.
“Nafahamu madhara ya kubadilisha viongozi mara kwa mara na huwa sipendi kufanya hivyo kwa kuwa kunawafanya watu wafanye kazi kwa hofu na viongozi kutokuwa na mipango ya muda mrefu kwa kuhofia teuzi zao kutenguliwa.
“Kiongozi anapoondoshwa kazini ni fedheha kwa familia yake, watoto na vijana ambao walikuwa wanamuona kama mtu wa mfano, kwangu pia si lengo langu kubadilisha viongozi kwa kuwa inachukua muda mrefu kuwajenga lakini wakati mwingine nafanya hivyo kuepusha madhara Serikalini na kwa Wananchi.”