Rais Samia simamia hili, chakula kisitoke nje ya mipaka ya Tanzania. Wananchi wanauza hadi akiba zao

Semahengere

JF-Expert Member
Nov 29, 2020
1,186
1,955
Habari Wana Jukuwaa.

Mimi nataka kusema, Kwa kasi hii ya usafirishaji wa mazao nje ya nchi hadi magari ya Kenya yanaingia vijijini kukusanya Ni dhahiri kwamba hakuna Serikali imara.

Kwa ukame huu tungepaswa kusimamisha biashara ya mazao nje ya nchi kwa muda hali itengamae. Hawa wakulima wanadanganyiwa pesa hadi wanauza chakula cha akiba. Ukifika kwenye border zetu za Namanga na Tarakea ndio utajua jamaa wanasomba mzigo

Nasema hivi Serikali simamieni jambo hili. Chakula kisitoke nje ya nchi Tena Hadi mwaka ujao kama mvua zitanyesha.

Wacheni urafiki kwenye tumbo hamtaweza kuwalisha Hawa wananchi mambo yakiharibika wasimamieni wananchi wenu kabisa

Fanyeni kama Yusufu kipindi kile Cha njaa kule Misri wacheni mchezo na life za watu

Kwa hili Magu Namkumbuka. Nasema kwa hili.

Asanteni
 
Tutalaumu wakenya kwa upumbav wetu. Subirini kuna mtu anaupiga mwingi
 
Nimepata gunia 80 za mahindi kila gunia kilo 100. Nahifadhi gunia 10 kwa chakula na dharura.

Sasa anatokea mtu anataka nisiuze nnakotaka hata kama bei ni nzuri kisa kuna wengine hawana.

Hilo ni jukumu la nani? Ni vipi ukunikatisha tamaa mwakani nisilime utanilazimisha? Kwanini serikali isinunue mahindi na kuhifadhi au kuwagaia wasio nayo.

Ila mimi kwa sulubu nilizo pata ninyimwe bei nzuri. Mipango yangu ni kuhusu kaya yangu. Hizo kaya nyingine ni uratibu wa serikali lakini nisiviziwe nivune kisha niporwe kwa ngongo wa nyuma kupitia bei ndogo.

Hatukuwekeana mkataba.
Ikibidi serikali ngazi za chini watukague tunao uza kama hatujaweka akiba.

Hii habari ya kuzuia mazao yanayo zalishwa yasiuzwe nje siyo sahihi.

Yaani wakulima wafanye juhudi na bidii halafu watawala katika madawati wapitishe kuwa wakulima wasiuze watakako.

Kuna wasemao eti mahindi hayazalishwi na wanaovusha mipakani, sawa lakini wakulima wanajua kutofautisha nini Tshs 400 au 500 kwa kilo na nini Tshs 800 au 1000 kwa kilo.

Msituonee wakulima. Kulima sio shughuli ya kitoto.
 
Habari Wana Jukuwaa.
Mimi nataka kusema, Kwa kasi hii ya usafirishaji wa mazao nje ya nchi hadi magari ya Kenya yanaingia vijijini kukusanya Ni dhahiri kwamba hakuna Serikali imara. Kwa ukame huu tungepaswa kusimamisha biashara ya mazao nje ya nchi kwa muda hali itengamae. Hawa wakulima wanadanganyiwa pesa hadi wanauza chakula cha akiba. Ukifika kwenye border zetu za Namanga na Tarakea ndio utajua jamaa wanasomba mzigo
Nasema hivi Serikali simamieni jambo hili
Chakula kisitoke nje ya nchi Tena Hadi mwaka ujao kama mvua zitanyesha.
Wacheni urafiki kwenye tumbo hamtaweza kuwalisha Hawa wananchi mambo yakiharibika wasimamieni wananchi wenu kabisa

Fanyeni kama Yusufu kipindi kile Cha njaa kule Misri wacheni mchezo na life za watu

Kwa hili Magu Namkumbuka. Nasema kwa hili.
Asanteni
Tuna chakula cha kutosha kwenye maghala na bado watu Wana Mazao ya kuzidi kwenye mastoo maana tulipata ziada..

Zama za kufukarisha wakulima zilizikwa Chato,saizi Mazao yote ni pesna kilimo.ni biashara kama biashara zingine..

Bei ikiwa kubwa nenda shamba Mzee ukamatie fursa badala ya kulia lia na kuja na visingizio vya wakunya and such blaa blaa 👇
Screenshot_20221102-131244.png
Screenshot_20221102-131224.png
Screenshot_20221030-082658.png
 
Wewe umeshaanza kununua nafaka na kuweka akiba kama Huyo Yusufu?
Watanzania tuna shida sana. Kama watu hawataki chakula kiuzwe nje nunueni ninyi basi!

Yaani unataka mkulime ateseke na kilimo kwa miezi 8 shambani halafu aje akuuzie gunia shs 30,000/=?
Huo ni ufinyu wa mawazo, ukitaka kujua shulba za jembe kalime na ww!
 
Nimepata gunia 80 za mahindi kila gunia kilo 100. Nahifadhi gunia 10 kwa chakula na dharura.
Sasa anatokea mtu anataka nisiuze nnakotaka hata kama bei ni nzuri kisa kuna wengine hawana.
Hilo ni jukumu la nani? Ni vipi ukunikatisha tamaa mwakani nisilime utanilazimisha? Kwanini serikali isinunue mahindi na kuhifadhi au kuwagaia wasio nayo.
Ila mimi kwa sulubu nilizo pata ninyimwe bei nzuri. Mipango yangu ni kuhusu kaya yangu. Hizo kaya nyingine ni uratibu wa serikali lakini nisiviziwe nivune kisha niporwe kwa ngongo wa nyuma kupitia bei ndogo.
Hatukuwekeana mkataba.
Ikibidi serikali ngazi za chini watukague tunao uza kama hatujaweka akiba.
Hii habari ya kuzuia mazao yanayo zalishwa yasiuzwe nje siyo sahihi.
Yaani wakulima wafanye juhudi na bidii halafu watawala katika madawati wapitishe kuwa wakulima wasiuze watakako.
Kuna wasemao eti mahindi hayazalishwi na wanaovusha mipakani, sawa lakini wakulima wanajua kutofautisha nini Tshs 400 au 500 kwa kilo na nini Tshs 800 au 1000 kwa kilo.
Msituonee wakulima. Kulima sio shughuli ya kitoto.
Tanzania watu wote sio wakulima. Na pia hujapangiwa bei ya kuuza. Kinachotakiwa muuze bei mnayotaka ndani ya nchi Ili kukidhi mahitaji

Lingine kumbuka maisha ni kutegemeana
Wote tungelima ungemuuzia nani?

Elewa Serikalini Ina jukumu la kusimamia wananchi wake ...Kama na wewe ulivyo na jukumu la kusimamia familia yako

Hebu fikiri watu wote wangefikiri hivyo unavyofikiri kungekalika kweli hapa?

ILA MUDA UTASEMA. Na Bahati nzuri hamchelewi kuilaumu Serikalini njaa ikiingia mjini
 
Habari Wana Jukuwaa.

Mimi nataka kusema, Kwa kasi hii ya usafirishaji wa mazao nje ya nchi hadi magari ya Kenya yanaingia vijijini kukusanya Ni dhahiri kwamba hakuna Serikali imara.

Kwa ukame huu tungepaswa kusimamisha biashara ya mazao nje ya nchi kwa muda hali itengamae. Hawa wakulima wanadanganyiwa pesa hadi wanauza chakula cha akiba. Ukifika kwenye border zetu za Namanga na Tarakea ndio utajua jamaa wanasomba mzigo

Nasema hivi Serikali simamieni jambo hili. Chakula kisitoke nje ya nchi Tena Hadi mwaka ujao kama mvua zitanyesha.

Wacheni urafiki kwenye tumbo hamtaweza kuwalisha Hawa wananchi mambo yakiharibika wasimamieni wananchi wenu kabisa

Fanyeni kama Yusufu kipindi kile Cha njaa kule Misri wacheni mchezo na life za watu

Kwa hili Magu Namkumbuka. Nasema kwa hili.

Asanteni
Mpeni ushauri na kuhusu mbolea pia sio mnaangalia products tu ila raw materials mnajifanya kupiga kimya.
Ingia shamba ulime uone kama utaandika hiki unachokiandika.

Sent
 
Ukiona mtu ameweka picha ya Osama usibishane nae ..alishakata tamaa anatamani afe Anataka wa kufa nae
Katie mbele kule. Tuteseke kulima alafu mtupangie mnunuaji. Kama kuna faida zaidi nje mtulazimishe tuuze kwenye faida ndogo.
Aise nitakutukana. Heshimuni wakulima. Wamenyanyasika sana
 
Nimepata gunia 80 za mahindi kila gunia kilo 100. Nahifadhi gunia 10 kwa chakula na dharura.

Sasa anatokea mtu anataka nisiuze nnakotaka hata kama bei ni nzuri kisa kuna wengine hawana.

Hilo ni jukumu la nani? Ni vipi ukunikatisha tamaa mwakani nisilime utanilazimisha? Kwanini serikali isinunue mahindi na kuhifadhi au kuwagaia wasio nayo.

Ila mimi kwa sulubu nilizo pata ninyimwe bei nzuri. Mipango yangu ni kuhusu kaya yangu. Hizo kaya nyingine ni uratibu wa serikali lakini nisiviziwe nivune kisha niporwe kwa ngongo wa nyuma kupitia bei ndogo.

Hatukuwekeana mkataba.
Ikibidi serikali ngazi za chini watukague tunao uza kama hatujaweka akiba.

Hii habari ya kuzuia mazao yanayo zalishwa yasiuzwe nje siyo sahihi.

Yaani wakulima wafanye juhudi na bidii halafu watawala katika madawati wapitishe kuwa wakulima wasiuze watakako.

Kuna wasemao eti mahindi hayazalishwi na wanaovusha mipakani, sawa lakini wakulima wanajua kutofautisha nini Tshs 400 au 500 kwa kilo na nini Tshs 800 au 1000 kwa kilo.

Msituonee wakulima. Kulima sio shughuli ya kitoto.
Nipo pamoja nawe mkuu kuna viumbe vya allah humu wanasemaga kulima ni kazi ya masikin so wakae kwa kutulia tafuta shamba mwakn lima mahnd yako ili uweke akiba
 
Back
Top Bottom