Rais Samia sikia sauti ya Askofu Ikongo

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
RAIS SAMIA SIKIA SAUTI YA ASKOFU!

Kuna Waraka unasambaa katika mitandao ya kijamii unaosadikiwa kuandikwa na Bishop Ikongo. Waraka huo unadai kuwa Waraka wa Wizara wenye kichwa: "Mabadiliko ya Hadhi ya Vyeti vya Usajili wa Taasisi za Kidini" sio maelekezo ya Serikali ya CCM bali ni wa Msajili mwenyewe na baadhi ya viongozi wachache wasio na mapenzi mema na Serikali ya CCM.

Kama kweli Waraka huo unaosambaa mitandaoni ni wa Bishop Ikongo, basi tuna mambo machache muhimu ya kuangazia! Mosi, Bishop Ikongo ni miongoni mwa Maaskofu wachache sana waliojitangaza hadharani kuwa yeye ni kada wa CCM, na kwa sababu hiyo, Waraka wake unaweza kuwa na umuhimu mkubwa sio tu kwa sababu yeye ni Kiongozi wa Dini bali kwa kuwa pia yeye ni kada wa CCM.

Pili, Msajili huteuliwa na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM na katika mazingira ya miaka ya hivi karibuni, hakuna mteule wa Rais asiyekuwa kada wa CCM! Kwa mantiki hiyo, Msajili na yeye ni kada wa CCM! Tatu, hao 'viongozi wengine' wanaoshirikiana na Msajili kutaka kuihujumu Serikali ya CCM hawawezi kuwa Wajumbe wa Nyumba Kumi au Makatibu Kata! Ni lazima watakuwa na hadhi kuzidi ya Msajili kwa maana ya kuwa wenye ngazi kuanzia Makatibu Wakuu wa Wizara, Mawaziri na hata watu wazito ndani ya CCM!

Sisi Askofu Mwamakula tumeonya mara nyingi kuwa kuna mnyukano mkubwa wa makundi ndani ya CCM na ndani ya Serikali yake. Tumeangaliza kuwa kuna kundi lina vazi la utiifu lakini linatoa ushauri wa kupotosha Taasisi ya Urais kwa ili kuihujumu Taasisi hiyo. Ni dhahiri kuwa kundi hili liko ndani ya CCM, ndani ya Serikali na ndani ya TISS pia.

Wajibu wetu sisi ni kushauri, kukemea, kuonya na kuangaliza. Huko nyuma tulitoa kauli za kukemea minyukano hiyo na wale wanaotoa ushauri wa kupotosha Taasisi ya Urais. Siku chache zilizopita, tulimshauri Rais avunje Baraza la Mawaziri ili aliunde upya sambamba na kupangua safu katika vyombo vyote vya dola. Tunarudia tena kusisitiza kuwa Rais hana njia nyingine zaidi ya kufanya hivyo. Kufanya hivyo haitakuwa ni kwa manufaa yake na CCM tu, bali itakuwa ni kwa manufaa ya Taifa zima.

Tunajua kuwa watu wenye hila wataanza kutusagia meno kwa sababu ya msimamo wetu na ushauri huu ambao unaweka kikwazo katika kufanikisha hila zao. Na sisi tunafahamu kuwa tunatimiza wajibu wetu katika mazingira magumu sana katika zamani hizi ambazo kusimamia ukweli ni sawa na kuabiri meli inayokwenda kuzama Baharini. Lakini hatuna budi kutimiza wajibu huu (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Wanajamii wote na watanzania kwa ujumla msiisikie sauti ya askofu kwa sababu askofu huyo ni mhuni, ni bange ya mhuni kwa sababu wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015-2020 alikuwa ni shabiki wa CHADEMA kimpigia debe Lowasa kwenye ufunguzi wa kampeni pale viwanja vya jangwani aliomba kwenye ufunguzi.

Aliomba sana mgombea wa CCM apate tezi dume, lakini kwenye uchaguzi watanzania walimpuuza hawakumchagua mgombea wake, Leo hii tena Askofu kawa msema kweli wa kumsikiliza eti. Askofu ni mpotoshaji, mpotoshaji mpotoshaji Rais Samia usimsikiliza.
 
Hujasema huo waraka umeandika kitu gani, japo unaonekana utakuwa umeziweka taasisi za dini kwenye wakati mgumu zitakapohitaji kusajiliwa, hili litakuwa limekuja ili kumfunga mdomo Gwajima kama huo waraka utakuwa ni wa kweli toka ofisi ya msajili.

Hili sio sawa, nionavyo Gwajima kwasababu ni wa kwao walitakiwa kumshughulikia ndani ya vikao vyao, sio makosa ya Gwajima yasababishe kuwaumiza wasiohusika.

Kuhusu makundi ndani ya CCM na minyukano naona yanasababishwa na udhaifu wa mtawala, ana uwezo na mamlaka wa kuyamaliza, lakini ameamua kwa makusudi kuyaacha yaendelee kuwepo bila kujua hiyo minyukano ya makundi inaleta athari kwenye serikali anayoiongoza na kusababisha atupiwe mizigo ya lawama.

Athari hizo ni pamoja na ushauri mbovu anaopata toka kwa wasaidizi wake unaomletea lawama toka kwa wananchi kuwa serikali yake haiwajali wananchi.

Vitu kama tozo za miamala ya simu mpaka leo kimya, licha ya kuambiwa tume iliyoundwa ilishamaliza kazi yake, mapungufu kwenye baadhi ya teuzi anazofanya ambazo humlazimisha kutengua baada ya siku chache n.k
 
Hii si bahati mbaya, bali ni mkakati na matayarisho ya awali tu, kabla ya kuunganishwa kwa dini zote kuwa chini ya mtawala mmoja. Ni lazima madhehebu (taasisi za kidini) yaliyotawanyika yaunganishwe kuwa chini ya utawala mmoja.

Kwa madhehebu ya Kikristo kuungana na kuwa chini ya dhehebu mama maandiko matakatifu huita kama "sanamu ya mnyama kupewa pumzi ya kuishi tena ili kuendesha vita na watakatifu".
 
Naona Rais ameshajikatia tamaa ya kuwania Urais 2025 ndiyo maana ameamua kuacha bora liende. Kilichoandikwa na gazeti la uhuru hadi kufungiwa kwake kinadhihirisha nadharia hii. Na huu ndiyo mwanzo wa mwisho wa CCM.
 
Mkuu BAK why tukubali kucheza hizi sarakasi za CCM ambazo zinalenga kututoa kwenye wazo msingi(katiba mpya)
 
Mama hatari sana huyu halafu amekuwa muongo kupindukia.
Alianza kutudanganya akiwa msata kuwa mjomba wetu haumwi na yuko vizuri baada ya siku tatu akajakututangazia msiba kuwa mjomba kafariki.

Huyu mama si msema kweli kabisa, juzi anasema Watanzania wamekubali Tozo za miamala lakini hawataki katiba mpya.
 
Back
Top Bottom