BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
RAIS SAMIA SIKIA SAUTI YA ASKOFU!
Kuna Waraka unasambaa katika mitandao ya kijamii unaosadikiwa kuandikwa na Bishop Ikongo. Waraka huo unadai kuwa Waraka wa Wizara wenye kichwa: "Mabadiliko ya Hadhi ya Vyeti vya Usajili wa Taasisi za Kidini" sio maelekezo ya Serikali ya CCM bali ni wa Msajili mwenyewe na baadhi ya viongozi wachache wasio na mapenzi mema na Serikali ya CCM.
Kama kweli Waraka huo unaosambaa mitandaoni ni wa Bishop Ikongo, basi tuna mambo machache muhimu ya kuangazia! Mosi, Bishop Ikongo ni miongoni mwa Maaskofu wachache sana waliojitangaza hadharani kuwa yeye ni kada wa CCM, na kwa sababu hiyo, Waraka wake unaweza kuwa na umuhimu mkubwa sio tu kwa sababu yeye ni Kiongozi wa Dini bali kwa kuwa pia yeye ni kada wa CCM.
Pili, Msajili huteuliwa na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM na katika mazingira ya miaka ya hivi karibuni, hakuna mteule wa Rais asiyekuwa kada wa CCM! Kwa mantiki hiyo, Msajili na yeye ni kada wa CCM! Tatu, hao 'viongozi wengine' wanaoshirikiana na Msajili kutaka kuihujumu Serikali ya CCM hawawezi kuwa Wajumbe wa Nyumba Kumi au Makatibu Kata! Ni lazima watakuwa na hadhi kuzidi ya Msajili kwa maana ya kuwa wenye ngazi kuanzia Makatibu Wakuu wa Wizara, Mawaziri na hata watu wazito ndani ya CCM!
Sisi Askofu Mwamakula tumeonya mara nyingi kuwa kuna mnyukano mkubwa wa makundi ndani ya CCM na ndani ya Serikali yake. Tumeangaliza kuwa kuna kundi lina vazi la utiifu lakini linatoa ushauri wa kupotosha Taasisi ya Urais kwa ili kuihujumu Taasisi hiyo. Ni dhahiri kuwa kundi hili liko ndani ya CCM, ndani ya Serikali na ndani ya TISS pia.
Wajibu wetu sisi ni kushauri, kukemea, kuonya na kuangaliza. Huko nyuma tulitoa kauli za kukemea minyukano hiyo na wale wanaotoa ushauri wa kupotosha Taasisi ya Urais. Siku chache zilizopita, tulimshauri Rais avunje Baraza la Mawaziri ili aliunde upya sambamba na kupangua safu katika vyombo vyote vya dola. Tunarudia tena kusisitiza kuwa Rais hana njia nyingine zaidi ya kufanya hivyo. Kufanya hivyo haitakuwa ni kwa manufaa yake na CCM tu, bali itakuwa ni kwa manufaa ya Taifa zima.
Tunajua kuwa watu wenye hila wataanza kutusagia meno kwa sababu ya msimamo wetu na ushauri huu ambao unaweka kikwazo katika kufanikisha hila zao. Na sisi tunafahamu kuwa tunatimiza wajibu wetu katika mazingira magumu sana katika zamani hizi ambazo kusimamia ukweli ni sawa na kuabiri meli inayokwenda kuzama Baharini. Lakini hatuna budi kutimiza wajibu huu (Ezekieli 33:1-20).
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula