Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 31,660
- 32,964
Kaja na uzanzibari, kule wanaita chuo cha mafunzoYaani Mtu Kaiba na Kaua au amesababisha Hatari Kubwa ama katika Jamii au Nchi halafu akihukumiwa na Mahakama kwenda Jela Kisheria asiitwe tena Mfungwa na sasa aitwe Mwanafunzi?
Kwahiyo Mbakaji awe anaitwa Mwanafunzi Mbakaji, Muuaji nae awe anaitwa Mwanafunzi Muuaji huku Jambazi nae awe anaitwa Mwanafunzi Jambazi?
Hivi ni kwanini Viongozi huwa mnapenda Kukurupuka hasa katika Fikra na Matamko? Sasa Mhalifu leo hii akiitwa Mwanafunzi nini Hadhi tena ya Mwanafunzi hapo? Yaani leo hii Rais Samia hujui kuwa neno Mwanafunzi lina Hadhi Kubwa mno Kitaaluma na kwamba leo kutaka Kwako Kushauri kuwa hata hawa Wahalifu wa Kisheria ( Wafungwa ) nao waanze Kuitwa Wanafunzi ni Kuwadhalilisha Wanafunzi na hata Wanataaluma Wote?
Na kwa jinsi Mamlaka husika za Tanzania na Watu wanavyopenda Kujipendekeza Kwako nina uhakika huu Ushauri wako wataupokea bila ya hata Kuutathmini na Kuuchambua Kimantiki ( Logically ) kisha wataweka Pamba katika Masikio yao na Kuukubali ( Kukukubalia ) ili mradi tu uone Unanyenyekewa huku Mioyoni mwao wakiwa Wanakusanifu na pengine hata Kukudharau.
Rais Samia leo ( tena mapema tu hivi ) Mimi GENTAMYCINE naukataa wazi wazi hapa huu Ushauri wako ( Pendekezo lako ) kuwa kuanzia sasa Wafungwa wawe Wanaitwa jina la Wanafunzi bali kwa dhana ya Kujenga, Kudhibiti na hata kutoa Fundisho kwa Wengine waendelee tu kuitwa Wafungwa hivyo hivyo na kama hilo Jina wakiona linawakera basi waachane na Vitendo vyao vya Uhalifu katika Jamii.
Yaani Raia ( tena Amiri Jeshi Mkuu ) kabisa badala ya kuwa Mkali na Kuchukia Vitendo vya Kiuhalifu, Kuvikemea na kuonyesha kuwa huvitaki na huvipendi Wewe bila hata haya ( aibu ) kama Rais unakuja na Hoja Nyepesi ya kutaka wasiitwe tena Wafungwa bali waitwe Wanafunzi?
Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na hata Taasisi Nyeti hebu jitahidini sana Kumjenga Mama hasa katika yale ambayo anataka Kuyasema kwani ni kama naanza kuona Rais Samia huwa anatoa Kauli zake kwa Kukurupuka na Kimihemko zaidi hali ambayo inaweza sasa Kumfanya aanze Kudharaulika na hata Kuonekana Kituko na wale Waliobarikiwa Ubongo mzuri ( Akili Kubwa ) na Mwenyezi Mungu.
Nitawadharau mno Wanasheria ( ambao nawaheshimu sana ), nitawadharau mno BAKITA na nitamdharau zaidi Jaji Mkuu wa Tanzania ( ambaye namheshimu kutokana na kuwa na Akili sana na pia Poti wangu kutoka Mkoani Mara ) na nitamdharau kuliko Maelezo Waziri na Wizara husika kama Wote hawa kwa pamoja wataukubali huu Ushauri mwepesi na hafifu wa Rais Samia kuwa kuanzia sasa Wafungwa wawe Wanaitwa Wanafunzi.
Kwa wale mnaotaka kujua zaidi juu ya Ushauri huu mwepesi na hafifu alioutoa ( alioupendekeza ) Rais Samia nendeni ITV Tanzania mtaukuta huko na Mimi huku sasa nikiendelea tu Kuwakumbuka Marais wangu makini na Werevu ( Intelligent ) kuwahi kutokea nchini Tanzania Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Hayati Benjamin William Mkapa na Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli na sishangai ndiyo maana kila mara GENTAMYCINE huwa si tu nawakumbuka bali hata huwa nawalilia huku nikiionea Huruma Tanzania yangu inakoelekea.