Mama Samia wewe ni jemedari wetu mkuu. Mwenye shaka na uwezo wako kuliongoza taifa hili atakuwa hajitambui tu.
Hata hivyo nisiache kunukuu tokea katika msahafu wa kikristo pasemapo "si kila aitae bwana bwana atauona ufalme wa mbinguni."
Sawia na hii si kila wakuitao Mama Mama wana mapenzi mema na wewe kama rais. Wengi wao ni chui katika ngozi za kondoo. Wenye kukaanga mbuyu na kuwaachia wenye meno watafune. Hawana furaha kuliona taifa likija pamoja. Kwao mifarakano ndiyo furaha yao kamwe si suluhu.
Wapo wanaoshindwa kutambua kuwa wewe zaidi sana ya kuwa mwenyekiti wa CCM, pia ni rais wa JMT. Kofia inayokutaka wewe kuiheshimu na kuilinda katiba.
Kwa mujibu wa katiba, Serikali ni ya wananchi. Kunakokupa wewe wajibu wa kuwasikiliza wananchi wote. Vipi upande wowote kukutatiza wewe kumsikiliza yeyote?
Tunaamini chochoko za mifarakano tokea kwa wanaokuchagiza kutumia nguvu dhidi wengine hazitakuyumbisha wala kukufanya wewe kutokuuona mustakabala ulio mwema zaidi wa nchi yetu uko wapi.
Waswahili wanasema kataa neno usikatae wito. Waliokuomba kukuona waone, ukapate kuwasikiliza.
Penye wengi hapaharibiki neno.
Ninawasilisha.