Rais Samia; Si wote wakuitao Mama Mama wanakutakia heri

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
14,906
2,000
Mama Samia wewe ni jemedari wetu mkuu. Mwenye shaka na uwezo wako kuliongoza taifa hili atakuwa hajitambui tu.

Hata hivyo nisiache kunukuu tokea katika msahafu wa kikristo pasemapo "si kila aitae bwana bwana atauona ufalme wa mbinguni."

Sawia na hii si kila wakuitao Mama Mama wana mapenzi mema na wewe kama rais. Wengi wao ni chui katika ngozi za kondoo. Wenye kukaanga mbuyu na kuwaachia wenye meno watafune. Hawana furaha kuliona taifa likija pamoja. Kwao mifarakano ndiyo furaha yao kamwe si suluhu.

Wapo wanaoshindwa kutambua kuwa wewe zaidi sana ya kuwa mwenyekiti wa CCM, pia ni rais wa JMT. Kofia inayokutaka wewe kuiheshimu na kuilinda katiba.

Kwa mujibu wa katiba, Serikali ni ya wananchi. Kunakokupa wewe wajibu wa kuwasikiliza wananchi wote. Vipi upande wowote kukutatiza wewe kumsikiliza yeyote?

IMG_20210704_051559_619.jpg


Tunaamini chochoko za mifarakano tokea kwa wanaokuchagiza kutumia nguvu dhidi wengine hazitakuyumbisha wala kukufanya wewe kutokuuona mustakabala ulio mwema zaidi wa nchi yetu uko wapi.

Waswahili wanasema kataa neno usikatae wito. Waliokuomba kukuona waone, ukapate kuwasikiliza.

Penye wengi hapaharibiki neno.

Ninawasilisha.
 

Lorenzo Samike

JF-Expert Member
Jun 18, 2021
772
1,000
Haswa hawa wafuasi wa chama cha Demoghasia na maandamano.

Kila kitu MAMA MAMA MAMA. sijui ni madeko au ni kitu gani? Bado sijaelewa.

Kama mnafikiri katiba mpya inakuja kimasihara kwa kumuita Rais "MAMA" na kumlamba lamba, basi mtafurahishwa punde.

She is not just a MAMA, yuko na kundi lenye nguvu nyuma yake ambalo linachukua nafasi kubwa ya maamuzi anayoyafanya.

Msimchukulie poa nyie wafuasi wa mbowe.... shauri yenu!
 

billgate

JF-Expert Member
May 6, 2021
272
500
kumuita mama kunakera yani wabongo mnaweza hata kuibiwa kwa ajili ya mambo ya kijinga,kila mtu ana mama yake huyo samia ni rais tu

hili jina la mama mama tuachane nalo afanye kazi asije akalewa umama akasahau majukumu mazito ya nchi
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
14,906
2,000
kumuita mama kunakera yani wabongo mnaweza hata kuibiwa kwa ajili ya mambo ya kijinga,kila mtu ana mama yake huyo samia ni rais tu

hili jina la mama mama tuachane nalo afanye kazi asije akalewa umama akasahau majukumu mazito ya nchi

Zaidi sana kuna waliojikita kumwita Mama Mama malengo mazima yakiwa kumfarakanisha na yeyote na kwa lolote hata kama ni la kijinga:

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom