Mpinzire
JF-Expert Member
- Jan 18, 2013
- 7,219
- 12,933
Rais Samia ameyasema hayo akiwa Jijini Arusha huku akisema atajemga stendi kubwa na za kisasa kama ilivyokuwa awamu ya 5.
---
AIS Samia Suluhu Hassan amesema serikali yake inaandaa mradi mahususi wa kuomba fedha ili kufanikisha ujenzi wa stendi mpya za kisasa katika miji na majiji.
“Tutakapo zipata tunania maeneo mengi ya majiji na miji kuwe na stendi za kisasa kama tulivyo anza katika awamu ya tano,” amesema Rais Samia wakati akitolea ufafanuzi hoja zilizojitokeza katika mkutano wake na Wananchi wa Arusha akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Rais Samia ametolea mfano stendi ya mabasi ya Arusha akisema ni jukumu la halmashauri kukamilisha kila kitu ukiwemo mchoro ili serikali ipitishe fedha kupitia TAMISEMI. Stendi kuu ya Mabasi ya Magufuli iliyopo Mbezi Dar es Salaam ni moja ya stendi za kisasa zilizojengwa kipindi cha utawala wa awamu ya tano. Stendi nyingine ni Dodoma na Morogoro.