Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Ni kweli kupanda gari la juu kwa hawa wazee wetu ni changamoto.
Ni vizuri wakaliona pia kwa Mama Maria Nyerere.
Ni kweli kabisa uzee hiyo ngumu sana vitu vingine.
Malkia kafa mda wake ulipofika ila hakuna alichokosa mpk anafariki labda mume tu.
 
Inachezewa sana kivipi we jamaa.. Mbona unakuwa na roho ya kimaskini sana?

Zawadi ya Ml 450 kwa mtu alie simamia ustawi wa taifa letu.. tena ukiangalia hata kwenye baadhi ya sarafu kuna sura yake hiyo tsh ml 450 bado ni ndogo sana Ndugu yangu
Kumbuka Tshs 450m = 15 Tractors
 
Baada ya kuzindua kitabu chake Jioni ya leo Rais Samia amesema anamshukuru Mungu kwa kumpa Mwinyi miaka 96 na sasa anamwombea afike 100

Pia amesema anaona Mzee Mwinyi akipata shida ya kupanda gari alilonalo na ameamua kumpa zawadi ya benzi la chinichini.

USSR

=====

“Nakushukuru sana Mzee wangu Rais Mstaafu Mwinyi kwa kunikaribisha kuzindua kitabu cha simulizi ya maisha yako, nampongeza Mzee Mwinyi kwa kuamua kuandika kitabu ambacho sio tu kitawasaidia Watanzania na Dunia kumfahamu pia kina historia ya Tanzania” Rais Samia

kwenye uzinduzi kwa kitabu cha Mzee Mwinyi Dar es salaam leo

“Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi inaenda sambamba na kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa, tunamtakia kila la kheri wakati anatimiza miaka 96, tunamuomba Mungu akutunze ufike miaka 100 na zaidi ili tuzidi kuvuna hekima na busara zako” Rais Samia
View attachment 1778144
“Nimemuandalia zawadi Mzee Mwinyi, kwa kutimiza umri wa miaka 96 leo, nimekuwa nikiona usumbufu anaoupata akiwa anapanda na kushuka kwenye Gari lake, kwa niaba ya Serikali Mzee wetu leo tutampatia Benz la chini ambalo litampa raha kwenye Safari zake” Rais Samia
View attachment 1777949
View attachment 1777889
Mzee wa Ruksa
 
Back
Top Bottom