Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,888
22,644
Baada ya kuzindua kitabu chake Jioni ya leo Rais Samia amesema anamshukuru Mungu kwa kumpa Mwinyi miaka 96 na sasa anamwombea afike 100

Pia amesema anaona Mzee Mwinyi akipata shida ya kupanda gari alilonalo na ameamua kumpa zawadi ya benzi la chinichini.

USSR

=====

“Nakushukuru sana Mzee wangu Rais Mstaafu Mwinyi kwa kunikaribisha kuzindua kitabu cha simulizi ya maisha yako, nampongeza Mzee Mwinyi kwa kuamua kuandika kitabu ambacho sio tu kitawasaidia Watanzania na Dunia kumfahamu pia kina historia ya Tanzania” Rais Samia

kwenye uzinduzi kwa kitabu cha Mzee Mwinyi Dar es salaam leo

“Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi inaenda sambamba na kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa, tunamtakia kila la kheri wakati anatimiza miaka 96, tunamuomba Mungu akutunze ufike miaka 100 na zaidi ili tuzidi kuvuna hekima na busara zako” Rais Samia
2767605_Mwinyi.jpg

“Nimemuandalia zawadi Mzee Mwinyi, kwa kutimiza umri wa miaka 96 leo, nimekuwa nikiona usumbufu anaoupata akiwa anapanda na kushuka kwenye Gari lake, kwa niaba ya Serikali Mzee wetu leo tutampatia Benz la chini ambalo litampa raha kwenye Safari zake” Rais Samia

IMG_20210508_210843_208.jpg
 
Inachezewa sana kivipi we jamaa.. Mbona unakuwa na roho ya kimaskini sana?

Zawadi ya Ml 450 kwa mtu alie simamia ustawi wa taifa letu.. tena ukiangalia hata kwenye baadhi ya sarafu kuna sura yake hiyo tsh ml 450 bado ni ndogo sana Ndugu yangu
 
Baada ya kuzindua kitabu chake Jioni ya leo mama samia amesema anamshukuru Mungu kwa kumpa mwinyi miaka 96 na sasa anamwombea afike 100

Pia amesema anaona mzee mwinyi akipata shida ya kupanda gari alilonalo na ameamua kumpa zawadi ya benzi la chinichini ambalo thamani yake ni milioni 450 tsh ,hii nchi inachezewa sana


USSR
Wa kuwalaumu ni CCM
 
Ameshaanza na yeye kulewa madaraka. Kuna ulazima gani wa kumnunulia mzee mstaafu gari la mamilioni yote hayo ya shilingi na huku kuna changamoto lukuki kwa Watanzania maskini?

Yaani milioni 450 kirahisi tu!! Kuna ulazima wa kuiondoa ccm madarakani. Haya mambo ya kuchezea kodi zetu miaka nenda, yanachosha.
CCM ni kirusi cha Corona kilichopo India kwa sasa!
 
..as long as sio MUUAJI mimi nimeridhika.

..mabadiliko hayaji kwa mara moja.

..huwezi kutoka kwenye utawala wa KIKATILI halafu ghafla ukaingia kwenye moja kwa moja kwenye demokrasia, rule of law, na utawala bora.
 
Back
Top Bottom