Rais Samia sasa unaturudisha kwenye tawala za machifu kweli, au ndo njia ya umaarufu wa kisiasa?

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,698
4,693
Anachokifanya Rais Samia ni kuharibu amani ya nchi hii. Tumeishi bila ukabila lakini polepole tunarudishwa kwenye mtafaruku bila sababu. Tunalazimisha kutambua machifu bila sababu.

Yaani viongozi wa kiukoo, kikabila Watu hawa wanastahili kuachiwa kabisa nje ya mfumo kama ambavyo imekuwa miaka yote ya uhuru. Kuna nini hadi Rais anawatafute kwa nguvu zote hizo?

Museveni aliwadekeza Baganda, matokeo yake hadi leo ndani ya Kampala anaonekana ni mpangaji asiyetakiwa. Kule Kasese mwaka 2016 hadi mauaji yalitokea kwa sababu ya kudekezwa. Hatuhitaji tawala za kichifu/kikoo ktk nchi hii.

Hangaya.jpg
 
ni fursa nzuri ya kuona nguvu ya BUNGE CCM-99%!

NB: Rais Samia anatangaza nchi kiutalii tu, ... na machifu wapo japo hawana meno!
 
Mama wasiende kumzindika wasukuma akazidisha tozo maana hawa kwa ndumba ndio wenyewe. Wamemvisha ngozi kabisa kiimani hili si sawa sana labda kwa waislamu.
 
Namibia machifu wa kila kabila wanalipwa na serikali na wanatembelea gari za serikali lakini Namibia ndio nchi yenye amani zaidi ya nchi nyingine Africa. Ni mipango mizuri tu.
 
Kuwatambua rasmi machifu kwa Tanzani linaweza kuwa Janga. Tujiulize kwanza kwa nini Nyerere aliwafutilia mbali? Naona Rais Samia hajiulizi watangulizi wake walikuwa wanakwama wapi katika mambo aliyokuta yamekwama. Kwa mfano haya ya machifu, Ya Zanzibar na bahari kuu, ya Bandari ya Bagamoyo nk.
 
Anachokifanya Rais Samia ni kuharibu amani ya nchi hii. Tumeishi bila ukabila lakini polepole tunarudishwa kwenye mtafaruku bila sababu. Tunalazimisha kutambua machifu bila sababu.

Yaani viongozi wa kiukoo, kikabila Watu hawa wanastahili kuachiwa kabisa nje ya mfumo kama ambavyo imekuwa miaka yote ya uhuru. Kuna nini hadi Rais anawatafuta kwa nguvu zote hizo?

Museveni aliwadekeza Baganda, matokeo yake hadi leo ndani ya Kampala anaonekana ni mpangaji asiyetakiwa. Kule Kasese mwaka 2016 hadi mauaji yalitokea kwa sababu ya kudekezwa. Hatuhitaji tawala za kichifu/kikoo ktk nchi hii.

Acha wivu.

Mbona Hayati Magufuli alikuwa anaentertain hizi shughuli za machifu tena kwa kiwango kikubwa lakini hukusema haya unayosema?
Hivi watu wengine mlizaliwa na roho za namna gani? Ni full unafiki na nongwa. Acheni hizo double standard!
 
Back
Top Bottom