Rais Samia, sasa ni wakati wa kuunganisha Tanzania Bara na Visiwani kwa kujenga daraja

Lady Mwali

Senior Member
Nov 15, 2018
147
332
Mh.Rais,
Kwa kuwa kisiwa cha Zanzibar ni chanzo kikuu cha vivutio vya kitalii, ukizingatia wewe ni mzaliwa wa Zanzibar basi fanya kila unaloweza kabla hujamaliza kipindi chako cha urais wa JMT ujenge daraja kubwa linalopita juu ya bahari kutoka Bagamoyo mpaka Zanzibar ili hata wenye magari waende ZNZ kirahisi.

Ninahakika hili liko ndani ya uwezo wako kupata pesa kufanikisha mradi huu mkubwa.

Natambua jinsi ulivyokubalika kimataifa.Nchi za wahisani wanaweza kufanikisha hili pamoja na mapato ya ndani, ikibidi ongeza tozo katika huduma mbalimbali kama ununuzi wa LUKU, mafuta na hata katika miamala ya simu ili kufanikisha mradi huu utakaenda sambamba na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

Ninahakika hata ukishawishi nchi za UAE ( Umoja wa Falme za Kiarabu) pamoja na Omani wafadhili mradi huu utafanikiwa kupata ufadhili kutoka nchi hizi zenye historia kubwa katika visiwa vya Zanzibar, ukizingatia Omani ilitawala Zanzibar.

Hayati Magufuli aliwezaje kujenga Airport Chato akiwa Rais wewe utashindwaje kujenga daraja kubwa?
Mcheza kwao hushinda.

Kukamilika mradi huu utasaidia kuimarisha Muungano na utalii ktk visiwa hivi.Nina hakika 100% hili linawezekana, naomba siku ya uzinduzi wa ujenzi wa daraja hili niwepo.

Happy Mapinduzi Day.
 
unadhani hilo daraja ni kazi Rahis?litameza trillion kama 3..utazirudishaje
 
Nadhani ni wakati sahihi wa kuwa na serikali tatu🚶🚶🚶
 
Back
Top Bottom