Rais Samia S. Hassan, hili la kuwa nalo makini

Baba jayaron

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
4,007
5,446
Kwako Mheshimiwa,

Pole kwa majukumu magumu uliyonayo katika kuhakikisha tunapiga hatua.

Pia nikupongeze kwakuonesha kwamba wewe ni msikivu hasa kwa uteuzi na utenguzi wa kiongozi wa TPDC.

Lengo la ujumbe huu nikukuongozea technique au ushauri katika awamu yako,
Mheshimiwa Rais, nadhani unafahamu kabisa kwamba mpaka sasa unakambi mbili au zaidi zinazovutana wapate nafasi kukushawishi wapate teuzi si kwa maslai ya taifa au kukusaidia bali kwa maslai yao binafsi au kukuangusha.

Mama kwenye suala la teuzi kama kuna watu wanakushauri pokea kwa jicho la tatu ushauri wao, lakini maamuzi makubwa yatokane na dhamira yako ya dhati ya kuisaidia nchi yetu.

Kama Rais mwanamama tunatamani uache alama dhabiti katika uongozi ili wanamama (wanawake) wapate kujivunia hata sisi kama taifa tutembee kifua mbele kua na rais aliyehudumu vipindi vyote kwa mafanikio.

Mtangulizi wako pamoja na changamoto zilizoonekana lakini alijitahidi saana kutokufungwa na uchama akitafuta watu pottential katika nafasi nyeti, hivo kwakua hili ni jema si mbaya ukaliiga ilikuleta tija kwenye uongozi wako.

Tunaimani hakuna hata mmoja aliyekupa hio nafasi zaidi ya Mwenyezi Mungu (Allah) hivyo hauwiwi kumlipa mtu fadhila hapo zaidi ya kufanya HAKI na ADILI kama shukrani kwake.

Asalaam Aleykum.
Tumsifu Yesu kristo.
 
Mungu akubaliki sana Ushauri ni Mzuri sana

Ajaribu kutafuta watu wenye potential sehemu mbali mbali na sio kuangalia tuu wale anaoletewa au wa karibu
yaani ukiangalia ni kama kuna watu hana imani nao ila kama anawafanyia ugwana flani hivi nadhani hio haitakua na afya kwetu nadhani angejipa nafasi zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom