Rais Samia S. Hassan akutana na Chama cha Wafanyabiashara wa China

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,263
24,140
21 April 2021

RAIS SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WA CHINA


Mhe. Samia Suluhu Hassan leo akutana na wawakilishi wa chama cha wafanyabiashara wa China wanaoendesha biashara zao Tanzania.

Mwakilishi huyo wa chamber hiyo ya wafanyabiashara amebainisha kwa sasa kuna zaidi ya makampuni 800 ya China yanayofanya shughuli zao nchini Tanzania na kuwa wanaridhishwa na mazingira mazuri ya kufanya biashara nchini Tanzania.

Akaongeza mwakilishi wa wafanyabiashara hao kuwa wana mpango wa kuanzisha eneo maalum la kibiashara nchini Tanzania ambapo viwanda vyao watazalisha bidhaa mbalimbali kama za mawasiliano kama simu, madawa n.k
Source : Global TV online

N.B
Kariakoo jijini Dar es Salaam Tanzania, kuibuka tena kama kitovu cha biashara kanda ya maziwa makuu na kusini mwa Afrika

. "Kariako is no doubt one of the biggest commercial centres in Tanzania and East Africa at large where many Chinese businesspeople operate.http://tz.china-embassy.org/eng/ddbd/t1123754.htm

Kasi hii ya kuvutia na kuwapa imani wafanyabishara inaungwa mkono tangu awamu ya Jakaya Kikwete na sasa awamu ya Mh. Samia Suluhu Hassan inazidi kuunga mkono sera hiyo kushirikiana na wadau wa maendeleo.

http://tz.china-embassy.org › ddbd
Chamber pledges to ensure high quality products
28 Jan 2014 — The Kariakoo Chinese Chamber of Commerce (KCCC) has promised to adhere to Tanzania's product standards. It says by so doing it will protect the image of the Chinese manufacturers. According to him, the chamber which has more than 200 members will operate ethically and create more jobs for Tanzanians
 
Tunakwenda vizuri ndugu zangu. Tumtieni moyo mama pamoja na kumshauri ushauri wenye kujenga, tutafika sehemu nzuri sana ndani ya muda mfupi.

Hatua hii ni muhimu kwa ajili ya kutengeneza ajira mpya za kutosha na kuchangamsha uchumi wetu ambapo nchi nyingine za kiafrika zitakuja kununulia magari, simu na vifaa vingine vya ki -electoniki hapa Tanzania badala ya kwenda china.
Maono ya Rais mama Samia kuhusu uwekezaji nchini kwenye nyuzi 360
 
Usitumie mdomo wako au vidole kufanya kazi ya mku..du. Mambo ya HOVYO unaandika, dini haina nafasi kwa Rais SSH kwa kuwa anateua watu kwa uwezo na umahiri wao. Na mimi ni Mkristu toka dhehebu Katoliki
Unakurupuka..
 
Enzi za Wafanyabiashara toka Zimbabwe, Malawi, Zambia, Dr Congo, Rwanda, Burundi, Comoro kuishia Kariakoo Dar es Salaam kununua mahitaji yao badala ya kwenda China zinarudi.

Hii itachochea uchumi wa sekta zote biashara za jumla, rejareja, mahoteli, nyumba za wageni, usafiri na starehe.

Jiji la Dar es Salaam linaanza kurudisha hadhi yake iliyopotea kwa miaka 5.
 
Mataga walituchelewesha sana miaka hii 5.

Maendeleo ni watu siyo yale Maendeleo ya Vitu kama majengo ya Dodoma makao makuu sisi watu wa Dar es Salaam hayatufaidii chochote
 

Biashara Soko la Kariakoo saa 24, Mlipaji Mkuu wa Kodi, Tegemeo kwa Wafanyabiashara​


*Taa, kamera za CCTV zaanza kufungwa mitaani
*Lengo ni kulifanya kama masoko makubwa duniani

BIASHARA katika Soko la Kariakoo, hasa kwa maduka yanayozunguka eneo hilo, sasa zitafanyika kwa saa 24 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali.

Agizo hilo lilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Februari 28, mwaka huu alipokutana na wafanyabiashara wa Kariakoo.

Majaliwa alisema kuwa Serikali imepanga mpango wa kubadilisha utaratibu wa kufanya biashara katika eneo la Kariakoo ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa saa 24 kama yalivyo masoko makubwa duniani.

Alisema lengo la mabadiliko hayo ni kukuza uchumi wa taifa na wa wafanyabiashara kwa ujumla.
“Nchi yetu ina usalama na ulinzi wa kutosha, hivyo hatuwezi kushindwa kufanya biashara wakati wote,” alisema Majaliwa.
Kutokana na agizo hilo, MTANZANIA ilitembelea eneo hilo na kuzungumza na uongozi wa soko ili kujua utekelezaji wake umefikia hatua gani.

Akizungumzia utekelezaji wa agizo hilo jana, Kaimu Meneja Mkuu wa soko hilo, Donald Sokoni, alisema kuwa katika kutekeleza agizo hilo la Serikali kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya kufunga taa zaidi ya 70 katika soko hilo ambazo zitasaidia kuongeza mwanga, hasa nyakati za usiku.

Alisema mbali na taa hizo, pia wameweza kufanya ukarabati wa vyoo na bafu katika soko dogo ili kutoa fursa ya wafanyabiashara kupata huduma za kuoga na nyinginezo.

“Tumeanza ukarabati kama ambavyo Serikali imeagiza na tuna imani ndani ya wiki hii ukifika hapa Kariakoo utakuta mabadiliko makubwa. Kwa kuwa tumejipanga kuimarisha utendaji na ulinzi pia ili agizo hili liwe endelevu,” alisema Sokoni.

Alisema kwakuwa soko hilo limeanza kufanya kazi tangu mwaka 1975, miundombinu yake imechoka, hivyo inahitajika maboresho makubwa.
“Uwezo wetu wa kifedha ni mdogo kwakuwa soko hili ni kwa ajili ya kutoa huduma tu, hatuna uwezo mkubwa wa kulifanya liwe la kisasa zaidi, hivyo tunaomba Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), iweze kutusaidia fedha za kupaka rangi jengo hili na tuweze kutoa huduma kwa saa 24,” alisema Sokoni.

Alisema wana jumla ya wafanyabiashara 1,673 ambao wanafanya biashara mbalimbali katika soko hilo.
Sokoni alisema wanakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti walionao ambayo haitoshelezi kufanya maboresho ndani ya soko hilo ambalo lina idadi kubwa ya wafanyabiashara na wateja wanaoingia na kutoka.
UFUNGAJI KAMERA ZA ULINZI
Mei 17, mwaka huu, Mtendaji wa Mtaa wa Kariakoo Magharibi, Manyala A. M, aliandika barua akiwataka wamiliki wa nyumba zote kuhakikisha wanapaka rangi majengo yao na kuweka taa kubwa mbele pamoja na kufunga kamera za CCTV.

“Kutokana na agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ili kuwezesha eneo la Kariakoo kufanya kazi kwa saa 24, wamiliki wote wa majumba mnaagizwa kupaka rangi majengo, kuweka taa kubwa mbele ya jengo na kuweka CCTV kamera. Hatua kali za kisheria utachukuliwa mmiliki atayeshindwa kuwasilisha agizo hili,” ilieleza barua hiyo ambayo ilinakilishwa kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kariakoo Magharibi.
HISTORIA SOKO LA KARIAKOO
Soko la Kariakoo ni soko kuu jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla ambalo hufanyika biashara za aina zote za mahitaji muhimu ya kila siku kwa Watanzania na raia kutoka nje ya nchi.

Wafanyabiashara kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zimbabwe, Zambia, Malawi na Visiwa vya Comoro hufika Kariakoo kununua bidhaa mbalimbali ikiwamo nguo na kupeleka katika nchi zao.

Biashara zinafanyika kwa jumla na rejareja. Soko hili linajumuisha majengo mawili makuu (soko kubwa na soko dogo) pamoja na maeneo yanayozunguka majengo hayo.

Soko la Kariakoo lipo katikati ya Jiji la Dar es Salaam na ndiyo chanzo cha eneo zima la Kariakoo kujulikana kwa jina hilo.
Jengo la Soko Kuu la Kariakoo lipo katika kiwanja namba 32, na limezungukwa na mitaa ya Nyamwezi, Mkunguni, Sikukuu na Tandamti.
Historia ya jina la Kariakoo na soko la Kariakoo inaanzia tangu enzi za ukoloni wa Mjerumani wakati Tanzania Bara ikiitwa Tanganyika.

Uamuzi wa kujenga Soko Kuu la Kariakoo ulifanywa na Serikali mwaka 1970 baada ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuagizwa kujenga soko jipya la kisasa ambalo lingechukua nafasi ya soko la zamani.
Matarajio ya Serikali ya kujenga soko hilo yalikuwa ni kuwapatia wakazi wa jiji soko kubwa la chakula ambalo lingetosheleza mahitaji yao kwa muda wa miaka 50 hadi 70. Mipango ilikamilika na ujenzi ulianza rasmi Machi 1971.

Ramani ya jengo la soko ilitayarishwa na mchoraji wa ramani za majengo, Mtanzania Beda Amuli na wajenzi wakawa Kampuni ya MECCO wakisaidiana na makandarasi wengine.
Ujenzi uligharimu Sh milioni 22.
Shughuli zote za ujenzi zilikamilika Novemba 1975, na soko lilifunguliwa rasmi kwa matumizi ya wananchi Desemba 8, mwaka 1975 na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.
TRA NA MKOA WA KODI KARIAKOO
Septemba 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kwa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, alitangaza kulifanya eneo hilo kuwa mkoa maalumu wa kodi.

Kayombo alisema eneo la Kariakoo ni kitovu cha biashara hapa nchini na kwamba litasaidia kwa kila mfanyabiashara kuwa na mashine ya kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo.

Alisema kuwa hiyo ni moja ya mkakati wa harakati za kuhakikisha kuwa mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa wakati.

Source : Biashara Soko la Kariakoo saa 24 | Mtanzania
 
Tafadhali ya corona ilichukuliwa kwenye kutaniko hilo?

Wachina wengine walienda kumwona "RIP" Magufuli.

TAHADHARI NA USALAMA KWA "MAMA" NI MUHIMU KULIKO VITU VYOTE.
 
Mungu mbariki Rais wetu kwa maono mema kwa wananchi wake...safi sana Mama Samia Suluhu Hassan
 
Mama anajitahidi kurudisha imani kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza ncbhini. Huu ni hatua nzuri ya kuelekea kufufua biashara, uwekezaji na ukuaji uchumi.

Ni matumaini yetu kuwa hili litaenda sambamba na kupunguza na koundoa kabisa kero mbalimbali zinazokwamisha ufanyaji biashara ikiwa ni pamoja na masuala ya kodi, upatikanaji vibali N.K.
 
Tatizo la hawa Wachina ni kutothamini utu wa mtu mweusi. Mshahara kwa mwezi anaweza kukwambia sh. Laki moja tu bila aibu. Na ikichelewa anakukata, isipokuwa kazini eti unaumwa hupati kitu. Ni aibu.
 
Sema wa china ubaya wao wakiingiza sehemu wana sepa na kila kitu awa zambia saizi wamekamata kila kitu.
 
Ni vyema pia tujipange kuwasimamia. La sivyo tutaendelea kuwa watumwa ndani ya ardhi yetu
Shida ya wachina ni kwamba wameweka mbele zaidi maslahi yao binafsi,pia wasipoangaliwa kwa umakini mkubwa wanachanganya biashara aina zote na ujangili hata wa mali asili kama uwindaji haramu wa Tembo na vitu kama hivyo.so tunahitajika watz kuwa smart kidogo ktk kuwasimamia na tusikubali wakatushirikisha kwenye biashara za kipumbavu za kuihujumu nchi kama watakuja waje wakiwa wamenyooka na biashara wanazokuja kufanya.
 
22 April 2021
Dodoma, Tanzania

Hotuba ya Rais Leo Bungeni 22 April 2021

Mh. Samia Suluhu Hassan akilihutubia bunge mjini Dodoma Leo amesema serikali yake itaweka mazingira mazuri zaidi kuvutia uwekezaji kwa kuondoa urasimu usio na ulazima.

Mh. Rais wa awamu ya sita wa serikali ya Muungano wa Tanzania aliambia Bunge kuwa sekta binafsi ndiyo utii wa mgongo ktk kukuza uchumi na kutengeneza nafasi za ajira nyingi na soko kwa bidhaa za kuchakata mazao ya wakulima, wafugaji na kuongeza thamani madini.

Sekta binafsi kupitia uwekezaji wa ndani na toka nje, itachochea tija na ukisasa ktk uzalishaji mashambani, ufugaji na uvuvi kwani nchi hii Tanzania imejaliwa ardhi ,mabonde, maziwa, mito na ukanda mrefu wa bahari ya Hindi. Bila kusahau madini na utalii.

Bandari maalum za uvuvi kuanzishwa na meli nane za kisasa kununuliwa ili kufanya uvuvi katika bahari kuu.

Maeneo mahususi ya viwanda kujengwa kulingana na mazao yanayozalishwa ili kuwezesha mazao kuchakatwa kuzuia upotevu au uharibifu wa mazao baada ya kuvunwa na kutengeneza ajira ktk maeneo hayo ya nchi.

Maendeleo laini kupitia TEHAMA teknolojia ya habari na Mawasiliano kukuzwa ili kuwezesha Mapinduzi ya viwanda na uwekezaji kuweza kupatikana Tanzania unasisitizwa na serikali ya awamu ya sita kuelekea mpango wake wa Maendeleo ya miaka mitano inayoishia 2025.

Serikali Itatia mkazo Nishati mchanganyiko kama kutoka vyanzo vya mwanga wa Jua, thermal, gesi kujazia pale umeme wa nguvu za maji wa Rufiji JNHPP, Mtera, Kidatu n.k ambayo inaokabiliwa na tishio la mabadiliko ya tabia-nchi ili taifa liwe na uhakika wa nguvu za nishati kuendesha uchumi wake.
 
Back
Top Bottom