Rais Samia, Polisi wanadanganya kuhusu mauaji ya Hifadhi ya Ruaha, usikubali hili

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,983
2,000
Moderators, naomba msiunganishe uzi huu kwa kuwa una mambo ya msingi makubwa ya ukosefu wa haki za binadamu. Ni thread ya msingi sana katika kututoa katika karaha za utawala uliopita.

Nilikuwa nimeacha kutoa thread JamiiForums, lakini kwa hili la Polisi kudanganya umma kuhusu mauaji ya wananchi ndani ya hifadhi ya Ruaha limenifanya nirudi. Nimeshindwa kukaa kimya, nikiona jinsi Polisi wanavyodanganya waziwazi kama vile tuko enzi za awamu iliyopita.

Ni kwa jinsi hiyo basi, nimeona nitoe wito na appeal kwa Raisi Samia kwamba zile enzi za Polisi kudanganya umma askari wanapoua raia linapaswa kukomeshwa mara moja. Linaudhi sana, na Polisi wanapofanya hivyo wanatufanya wananchi hatuna akili. Na pia ni dharau kwa Raisi aliyewapa Polisi dhamana ya kulinda raia.

Kamanda wa Polisi Mbeya, Ulrich Mateia, billa aibu wala kupepesa macho,kawaida ya wauaji makatili, amedai kwamba raia waliouwawa Hifadhi ya Ruaha waliuwawa na wanyama wakali. Na bila kujua, akadokeza kwamba watu hawa wakiwa katika kuvua samaki, waliuwawa na mamba.

Sasa Bwana Ulrich Matei, hapa kuna jambo moja, eidha wewe huna uwezo wa kufikiri kama polisi, au sisi umetuona hatuna uwezo wa kufikiri kama wanadamu. Unatukana akili za Watanzania na Raisi wetu.

Umedai kwamba William Estoberi (38), Sandu Masanja (28) na Ngusa Salawa (14) waliuwawa na mamba wakivua samaki. Na ajabu ni kwamba miili yao imekutwa haijaliwa na mamba!

Matei, unachotaka kumwambia Raisi Samia na Watanzania kwa ujumla ni kwamba, wakati hawa watu wakivua samaki; kuna haya yalitokea (scenarios);
  1. Mtu wa kwanza alikamatwa na mamba na wengine wawili wakaendelea kuvua samaki
  2. Mtu wa pili akakamatwa na mamba na bado aliyebaki mmoja akaendelea kuvua samaki
  3. Mtu wa tatu akakamatwa na mamba wakawa wameisha
  4. Wote watatu walivamia na mamba mmoja kwa wakati mmoja
  5. Wote watatu walivamia na mamba tofauti watatu kwa wakati mmoja
  6. Mamba waliwaua lakini walikuwa wameshiba samaki kwa hiyo hawakuwala hawa wavuvi haramu
Je, haya ndio unayaotaka kumwambia Raisi Samia na Watanzania?

Ni wazi sana kwamba wewe Matei na askari wa aina yako mlizoea sana kutoa uongo wa kitoto katika matukio kama haya wakati wa awamu iliyopita, na bado mnadhani mko kwenye zile zama, bado mnadhani kuna mtu juu atawatetea hata mkiongea utumbo wa namna gani.

Tunakubali kwamba wananchi kuvamia maeneo ya hifadhi na kufanya ujangiri ni kosa kubwa, lakini hakuna sehemu sheria zetu zinasema askari wakiwakuta wananchi wamefanya hivyo wawaue na kuwasingizia mamba.

Kwako Raisi Samia, haya ndio mambo yatautofautisha utawala wako na ule uliopita. Umetupa faraja kwamba tunaanza upya, lakini tukianza upya na watu wasiotaka kubadilika kama hawa kina Matei hatutafika popote. Kama tunataka kuanza upya basi tuondoe takataka na makombo ya watu wenye tabia za kama Matei. Kifo cha Mtanzania yeyote, awe jangiri au raia mwema, hakikubaliki ikiwa kitatokea katika mazingira yenye kukiuka haki za binadamu.

Kwa hiyo basi, ushauri wangu ni uchunguzi wa kweli ufanyike juu ya suala hili. Ni wazi hata taarifa za madaktari waliofanyia uchunguzi maiti za wahanga wa tukio hili zina walakini. Miili ya wahanga ifanyiwe uchunguzi upya ili wale wote waliohusika na tukio hili wachukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa watu wenye kutumia vibaya dhamana walizopewa na serikali. Enzi za kuua raia na kuleta maelezo yasiyo na pua wala mdomo zimepita

Reference: RPC: Uchunguzi wa awali waliouawa Ruaha wameshambuliwa na wanyama
 

Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
3,618
2,000
nakuunga mkono asilimia mia. wanalindana sana hao jamaa utafikiri sisi raia siyo watanzania wenzao
Kuna mtu alikikamatwa na polisi kijijini kwetu hapa tarime usiku mida kama saa 3 hivi
Kesho yake wakatangaza ameuawa kwenye tukio la kuvamia hardware na amepigwa risasi akijaribu kukimbia
 

Bigawas

Senior Member
Feb 19, 2021
125
225
nakuunga mkono asilimia mia. wanalindana sana hao jamaa utafikiri sisi raia siyo watanzania wenzao
Kuna mtu alikikamatwa na polisi kijijini kwetu hapa tarime usiku mida kama saa 3 hivi
Kesho yake wakatangaza ameuawa kwenye tukio la kuvamia hardware na amepigwa risasi akijaribu kukimbia
Sio vibaya mkuu ungefafanua kama alituhumiwa kufanya nini ili hata mtu avute hisia kama alistahili au alionewa. Kuna baadhi ya matukio, mtu anatuhumiwa na watu tofautitofauti na taarifa za huyo mtu unakutwa zimeripotiwa zaidi ya mara 7 police.Kama ni wa namna hiyo ni halali yake wala usilalamike.
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,983
2,000
nakuunga mkono asilimia mia. wanalindana sana hao jamaa utafikiri sisi raia siyo watanzania wenzao
Kuna mtu alikikamatwa na polisi kijijini kwetu hapa tarime usiku mida kama saa 3 hivi
Kesho yake wakatangaza ameuawa kwenye tukio la kuvamia hardware na amepigwa risasi akijaribu kukimbia
Kuna watu hawana kabisa utu ni wauaji wabaya zaidi ya wanyama, na wapo watu wa aina hiyo ndani ya jeshi la polisi. Lakini utakuta ndio wa kwanza kwenda makanisani na misikitini wakiamini kuwa wakitubu angalau mara moja kwa wiki basi sio tatizo kuendelea na tabia zao za kinyama
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom