Rais Samia: Nilitaka kuzungumza Kiswahili kwenye Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa ila sikuwa na Mkalimani kwenye msafara

Umefanya nimecheka, siyo kwa ukalimani ule maana ingekuwa balaa angeweza kutafsiri kwamba Magufuli hajafa.
Hahahahaha kwii kwii kwii
Mzungu:My is Livingston

Mkalimani:Anaitwa jiwe linaloishi

Mzungu:I come from Johannesburg

Mkalimani:Anatokea Kwenye begi la yohana

Mzungu:I feel happy to see all of you here

Mkalimani:🤔🤔🤔🤔

Mzungu:🙄🙄🙄🙄

Mkalimani:😳😳😳😳

Watu:😁😁😁😁😁

Mkalimani:🤫🤫🤫🤫🤫

Watu:😂😂😂😂😂
 
Kurugenzi ya mawasiliano ifumuliwe yote, kweli Rais anaenda kwenye bunge la dunia bila kumuandaa kwa all possible presentation encounters?

Halafu tunasema eti tunaitangaza Tanzania kuvutia watalii kwa haya makosa madogo hivi na ya wazi kabisa.
Mama anatakiwa kuonywa yasije ya JPM yakajitokeza. Yeye ni Rais na jambo kama hilo ni masuala ya ndani si ya kuueleza Umma! Ni aibu sana kwa wasaidizi wake
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kiswahili kimekua kiasi cha kuweza kutumika kimataifa hali ambayo ilimfanya atake kuongea kiswahili alipokuwa akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa(UNGA)

Hata hivyo amesema katika msafara hawakuwa na mkalimani na hawakujiandaa kwa hilo, hivyo alilazimika kutumia kiingereza.

Amesema Kiswahili imekuwa ni lugha ya biashara kwa kanda ya Afrika Mashariki na SADC. Hata ukienda Ulaya ukimsema mtu kwa Kiswahili ujiangalie maana wanaweza kukujibu kwa kiswahili.
Mmmh sijuhi!
 
Alisahau kwenda naye au nafasi zilikuwa zimejaa ?

Unataka kuniambia UN hawana facilities za kuweka Mkalimali wa Kiswahili na kila mmoja anakwenda na wake...., Na kama Africa Kusini wametoa Hutoba kwa Zoom kwanini malimali asingefanya kazi kwa Zoom ?

Kwangu mimi hii haikuwa an issue..., kwa wengi aliokuwa anaongea nao wanajua Kingereza na kuongea directly ni kuepuka makosa katika translations..., lakini hii excuse ni ya ajabu sana bora angekaa kimya....
 
Tuseme alikurupuka, hiyo ziara haikuandaliwa, hivyo vya kuvaa masikioni nilisikia vinasetiwa lugha unayotaka kuisikia wewe,
Issue iko hapo, kwenye hizo mashine za kutafsiri, hakuna Kiswahili? Au wanatuona wote zumbukuku?

Kwanza hakuhitaji kuongea hicho kiswahili, hakuzungumzia mambo yanayotuhusu waswahili, CORONA ndo kitu pekee alichozungumza na kwakweli hakituhusu sisi, labda kwa ile safu ya wachache waliopangwa kupiga za mikopo na misaada ya corona, Mwezi wa kwanza and the like.
 
Mama Samia bado hujapoteza. Lile yai ulilovunja ni tosha.. Kiingereza Ni lugha ya Dunia. Na kule ulienda duniani.
We wasema ajapotea wakati yeye anaona kapotea hadi haelewi afanye nn?

Kwamba hakuwa amejipanga ataongea nini Kule ama atatumia lugha gani alikurupuka tu
 
Bora ibaki hivyo maana uongo aliozungumza mle unatia hasira ingekuwa Kiswahili sijui ingekuwaje,
Eti vibrant democracy in Tanzania?!!
 
Miaka ile tuliambiwa kuna vifaa vinatafsiri lugha zote duniani nani ameuhujumu huo ukumbi wa mikutano
 
Hii inaonyesha kuwa tumerudi enzi za Vasco da Gama kwenda kila safari wakati wowote hata bila kujali kama Kuna ulazima wa kusafiria. Mkutano wa UNGA upo kila mwaka na inajulikana kuwa ni mkutano wa kuuza sura kwa viongozi wa kitaifa Duniani.

Haiingii akilini kuwa mtu aliyekubali kushiriki mradi wa Royal tour kwa lengo la kuitangaza Tanzania aache kusafiri na usafiri wa kitaifa kwa maana ya Air Tanzania hata kama gharama ingekuwa kubwa kiasi gani. Air Tanzania ingelitangaza taifa vizuri zaidi.

Haiingii akilini pia chifu Hangaya mswahili ambaye analinadi taifa letu akaacha kukinadi kiswahili kwa kukitumia kwenye jukwaa la Dunia. Hii ilikuwa nafasi nzuri na adimu ya kuonyesha uongozi huko UNGA kuwa taifa letu lina Rais wa jamhuri na watu wake wana lugha yao ya mawasiliano inayotambulika kimataifa.

Yaliyopita si ndwele, Tugange yajayo.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kiswahili kimekua kiasi cha kuweza kutumika kimataifa hali ambayo ilimfanya atake kuongea kiswahili alipokuwa akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa(UNGA)

Hata hivyo amesema katika msafara hawakuwa na mkalimani na hawakujiandaa kwa hilo, hivyo alilazimika kutumia kiingereza.

Amesema Kiswahili imekuwa ni lugha ya biashara kwa kanda ya Afrika Mashariki na SADC. Hata ukienda Ulaya ukimsema mtu kwa Kiswahili ujiangalie maana wanaweza kukujibu kwa kiswahili.
Basi angehutubia kwa kiswahili mapokezi yangekuwa mpaka vijijini ndani kabisa
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Back
Top Bottom