Rais Samia: Nilitaka kuzungumza Kiswahili kwenye Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa ila sikuwa na Mkalimani kwenye msafara

Naam ALIKURUPUKA huo ndiyo ukweli. Inaonyesha jinsi alivyokosa umakini yeye na wapambe wake.

Tuseme alikurupuka, hiyo ziara haikuandaliwa, hivyo vya kuvaa masikioni nilisikia vinasetiwa lugha unayotaka kuisikia wewe,

Tanzania tunafeli wapi? Au ndo huo mpango wa kumdondosha samia.

Vile yule alitamka sululu sikusikia hata editing.

Wabongo mlitoa jina la rais kimakosa au ndo mpango mkakati,

Naongea na nyie kurugenzi ya mawasiliano.
 
Kurugenzi ya mawasiliano ifumuliwe yote, kweli Rais anaenda kwenye bunge la dunia bila kumuandaa kwa all possible presentation encounters?

Halafu tunasema eti tunaitangaza Tanzania kuvutia watalii kwa haya makosa madogo hivi na ya wazi kabisa.
Neo the one. kwann umejiitaa ivo?
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kiswahili kimekua kiasi cha kuweza kutumika kimataifa hali ambayo ilimfanya atake kuongea kiswahili alipokuwa akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa(UNGA)

Hata hivyo amesema katika msafara hawakuwa na mkalimani na hawakujiandaa kwa hilo, hivyo alilazimika kutumia kiingereza.

Amesema Kiswahili imekuwa ni lugha ya biashara kwa kanda ya Afrika Mashariki na SADC. Hata ukienda Ulaya ukimsema mtu kwa Kiswahili ujiangalie maana wanaweza kukujibu kwa kiswahili.
Serikali ya Tanzania chini ya chama cha mapinduzi itabaki kuwa ya kimzamzaa na kihadaa hadaa daima kwa watanzania. Yaani Kurugenzi ya mawasiliano ikulu ilishindwa kuandaa mkalimani kama lengo kubwa lilikuwa ni kukipromote kiswahili kwenye bunge la dunia?! Kauli ya SSH haijengi hoja yoyote ya msingi juu ya ukuwaji wa kiswahili kama alishindwa kukitumia kwenye mkutano ule.
 
Katika heka heka zangu za kuzurura duniani nikiwa kringsjå siku moja tumeingia kwenye lift sisi wabongo 2 na mzungu mmoja. Basi yule mzungu aliingia na masanduku mengi kiasi tukawa tumebanana. Nikamwambia yule mbongo kwa kiswahili hapa bora tungemuachia atangulie then tupande ikishuka tena.
Heeeeh yule mzungu si akatusalimia kwa kiswahili na akaendeleza mazungumzo kwa kiswahili fasaha kabisaa. Kumbe kwana aliwahi kuishi hapo chuoni makumira kwa program mbalimbali za kubadilishana uzoefu kwa wanafunzi.
Kweli usimseme mtu kwa kiswahili ukiwa nordic countries, Scandinavian states, Canada, UK, USA, German, France, Holland, na nchi zingine ambazo uhusiano wake na tanzania for the previous decades (i mean dating from 2015 kurudi nyuma) umekuwa mzuri.
2015 - 2021 ilikuwa wakati wa kujenga nchi..sio kupambana.
 
Kurugenzi ya mawasiliano ifumuliwe yote, kweli Rais anaenda kwenye bunge la dunia bila kumuandaa kwa all possible presentation encounters?

Halafu tunasema eti tunaitangaza Tanzania kuvutia watalii kwa haya makosa madogo hivi na ya wazi kabisa.
Nawe unaamini alichokisema,aseme tu aliogopa kuongea kiswahili asije akaonekana wa kuja
 
Tuseme alikurupuka, hiyo ziara haikuandaliwa, hivyo vya kuvaa masikioni nilisikia vinasetiwa lugha unayotaka kuisikia wewe,

Tanzania tunafeli wapi? Au ndo huo mpango wa kumdondosha samia.

Vile yule alitamka sululu sikusikia hata editing.

Wabongo mlitoa jina la rais kimakosa au ndo mpango mkakati,

Naongea na nyie kurugenzi ya mawasiliano.
Kwanza tunaomba radhi kwa kilichotokea na tunaahidi hakitojirudia..

Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
 
Hahahahaha kwii kwii kwii
Mzungu:My is Livingston

Mkalimani:Anaitwa jiwe linaloishi

Mzungu:I come from Johannesburg

Mkalimani:Anatokea Kwenye begi la yohana

Mzungu:I feel happy to see all of you here

Mkalimani:

Mzungu:

Mkalimani:

Watu:

Mkalimani:

Watu:
Mzungu : thank you and goodbye

Mkalimani: asante na ununuzi mwema


Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
 
...Mama ameiangalia kwa makini filamu inayohusi Wakalimani wa Umoja wa Mataifa ya 'Interpretaor'??
 
Mama Samia bado hujapoteza. Lile yai ulilovunja ni tosha.. Kiingereza Ni lugha ya Dunia. Na kule ulienda duniani.
U N inao wakalimani wa lugha zote wanachama, kila mjumbe huchagua lugha anayotaka kusikiliza, Ulaya ni uingereza tu ndiyo inatumia kiingereza na huko Marekani ni USA na Kanada, Marekani Kusini hakuna kiingereza, Bara la Asia ni India tu na nje ya hapo ni Austraria na Newzeland.
Yeye angeongea kwa kiswahili tu na UN wangetafsiri.
 
Mama siyo kabisa, pamoja na kuwa ni rais bado exposure yake ni ndogo sana, mpaka sasa hata hajui vikao vya UNGA (United Nation General Assembly) huwa vinaendeshwaje. Hata watu wanaomzunguka Rais wetu huenda upeo wao ni mdogo.

USAHIHI
Ukienda UN kwenye vikao vyao, huhitaji kwenda na mkalimani wako, kule kuna karibu kila mkalimani wa lugha inayotambulika kimataifa na hata baadhi ya lugha zisizotambulika kimataifa, hivyo kama Rais Samia angeongea Kiswahili basi kiswahili kingetafsiriwa automatically kwa lugha nyingine yoyote inayokubalika kimataifa (hata kama ni zaidi ya lugha 30), na hilo sio jukumu la muongeaji kusaka wakalimani au kuja nao bali huwa ni jukumu la UN kufanya hivyo na hufanya hivyo siku zote.

Pili, Mama Samia hata angekuja na mkalimani wake bado angeishia hotelini (asingeruhusiwa kuingia UN au kutafisiri hotuba hiyo rasmi kwa niaba ya UN) na bado asingetosha kutafsiri kiswahili kuja lugha zingine zote zinazohitajika kwenye vikao vya UN.

Tatu, kukua kwa technologia na ujio wa sasa wa Covid duniani umefanya shughuli nyingi za UN kufanyika kimtandao (virtual) na wakalimani wengi huwa hawapo pale pale ukumbini, huweza kuwepo popote pale duniani na wakatafsiri kwa ufasaha hotuba yoyote muda huo huo.

Nne, hotuba ya lugha ya kiingereza aliyoitoa Mama Samia kule UN ilitafsiriwa kwa lugha zote za kimataifa zinazotambulika na UN pamoja na lugha zingine kadhaa zisizotambulika kimataifa, kwa sauti na maandishi siku ile ile muda ule ule kwa faida ya wahudhuriaji, wasio hudhuria na watu wote duniani na zitabakia kuwa kumbukumbu ya kudumu (rejea) ya UN.

Mwisho, Mama Samia huenda amekaririshwa kuwa kila mtu duniani anajua kiingereza, ama anadhani UN ni mkutano wa wazungu na wazungu wote wanajua au kuhusudu kiingereza, Rais wetu bado mswahili swahili sana!!.
 
UDOM inatoa degree ya tafsiri na ukalimani katika miaka karibu minne iliyopita, sijawahi kuskia serikali imechukua hata mwanafunzi mmoja (mfasiri/mkalimani msomi) badala yake wameamua kuwakumbatia wadau wenye taaluma ya kuunga unga (holela) matokeo ndio haya; raisi hana official interpreter kwenye msafara wake+mkalimani kwenye msiba wa hayati Magufuli.


Ushauri wangu, mkuu wa mawasiliano ikulu afike pale UDOM achukue wanafunzi bora kadhaa na kuwaamini katika jukumu la kufanya tafsiri na ukalimani katika shughuli za kiserikali.
 
Nafikiri mama anadanganya kwamba kulikuwa na haja ya mkalimani wakati vipo vifaa vya kutafsiri lugha.
 
Nawe unaamini alichokisema,aseme tu aliogopa kuongea kiswahili asije akaonekana wa kuja
Huo ndio ukweli, watanzania wengi tumekuwa na hio tabia na yeye ana huo mtazamo sana.
Ili kutaka kutupooza kuonyesha kwamba anajali sana vya kwetu ndipo amekuja na swaga kwamba hakuwa na mkalimani.
 
Back
Top Bottom