Rais Samia: Nilitaka kuzungumza Kiswahili kwenye Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa ila sikuwa na Mkalimani kwenye msafara

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kiswahili kimekua kiasi cha kuweza kutumika kimataifa hali ambayo ilimfanya atake kuongea kiswahili alipokuwa akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa(UNGA)

Hata hivyo amesema katika msafara hawakuwa na mkalimani na hawakujiandaa kwa hilo, hivyo alilazimika kutumia kiingereza.

Amesema Kiswahili imekuwa ni lugha ya biashara kwa kanda ya Afrika Mashariki na SADC. Hata ukienda Ulaya ukimsema mtu kwa Kiswahili ujiangalie maana wanaweza kukujibu kwa kiswahili.
Kwa hiyo tangu hotuba inaandaliwa ilikuwa ya Kiswahili, ila alipofika kule na kubaini mkalimani ajaja ndio aliisoma kwa kiingereza?
 
Kurugenzi ya mawasiliano ifumuliwe yote, kweli Rais anaenda kwenye bunge la dunia bila kumuandaa kwa all possible presentation encounters?

Halafu tunasema eti tunaitangaza Tanzania kuvutia watalii kwa haya makosa madogo hivi na ya wazi kabisa.
Angembemba mkalimani watu pia wanfelaumu kuwa ameenda na watu wengi

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Aseme tu ameona noma kutumia kiswahili kuomba chanjo maana watz wangeshangaa why anaomba chanjo wakati chanjo zilizopo tz zimesuswa na wananchi.
 
UDOM inatoa degree ya tafsiri na ukalimani katika miaka karibu minne iliyopita, sijawahi kuskia serikali imechukua hata mwanafunzi mmoja (mfasiri/mkalimani msomi) badala yake wameamua kuwakumbatia wadau wenye taaluma ya kuunga unga (holela) matokeo ndio haya; raisi hana official interpreter kwenye msafara wake+mkalimani kwenye msiba wa hayati Magufuli.


Ushauri wangu, mkuu wa mawasiliano ikulu afike pale UDOM achukue wanafunzi bora kadhaa na kuwaamini katika jukumu la kufanya tafsiri na ukalimani katika shughuli za kiserikali.
Hao wakalimani wa Udom labda wakaombe kazi UN lakini kwa mfumo wa UN hawawezi kuingia huko, kwa hili la Rais naona angekuja na malalamiko ya ubaguzi wa wazungu kuwa walimkatalia mkalimani wake kuingia UN! Bila kujua wanao wakalimani wote wa lugha rasmi za wanachama, mfano Tanzamia tuna lugha nyingi ila moja ndiyo rasmi mfano kitindiga, basi hicho kitatafsiriwa.
 
Bora umepiga English Mama..Hongera sana
Wabongo wote wameufyata

Walidhani hukijui kama naniii
 
Lakini bado vyombo vyetu vya kutoa haki za watanzania havitumii Lugja ya kiswahili kutoa haki.
tunapaswa tuharakishe vyombo vyetu vitoe haki za watanzania kwa Lugha ya kiswahili sio Kiingereza.
 
Halafu yuleyule angepiga ukalimani kimya kimyaa kule na vile wageni wameweka headphone angewalisha matango pori ungeona watu wanapiga makofi hujui wanachopigia makofi...
haahaaaaha jamaa angetengeneza speech of the Karne maana walichosikia sicho kilichoandikwa kwenye hotuba baada kumaliza kikao!
😁😁😁
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kiswahili kimekua kiasi cha kuweza kutumika kimataifa hali ambayo ilimfanya atake kuongea kiswahili alipokuwa akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa(UNGA)

Hata hivyo amesema katika msafara hawakuwa na mkalimani na hawakujiandaa kwa hilo, hivyo alilazimika kutumia kiingereza.

Amesema Kiswahili imekuwa ni lugha ya biashara kwa kanda ya Afrika Mashariki na SADC. Hata ukienda Ulaya ukimsema mtu kwa Kiswahili ujiangalie maana wanaweza kukujibu kwa kiswahili.
Hakujiandaa kwa hilo? Hivi hawa watu wako sawa kichwani kweli?!
 
Au ndo tuamini Rais aliandaliwa na katiba? Mpaka safari nayo ni kwa kudra za Mungu,haikuandaliwa.
Haya tusiseme sana,tutakulaumu katiba kwa kutuandalia safari vibaya to USA
Hizi tunaita porojo za wanasiasa. Alikuwa anafurahisha genge. Wakalimali wapo wengi sana hata angetaka kutafuta siku moja kabla ya safari angepata.
 
Ahsante kwa taarifa...

Wakaliamani siyo lazima uende nao, pale pale unaweza kuwapata...
 
Back
Top Bottom