Rais Samia nia yako ni njema lakini hao unaowaongoza akili zao wanazijua wenyewe

Nimekua napitia nyuzi za Watanzania tangu ujio wa Mama Samia jana hapa nchini Kenya, hamna hata uzi mmoja unaojadili au kudadavua huu ujio kitaalam, kwa minajili ya kuelewa dhamira ya mama kwenye jitihada zake za kuifanya Tanzania iamke tena. Kila Mtanzania analalamika tu, watu wameingiwa na uwoga wa ajabu, yaani yanayojadiliwa yangekua yanaandikwa na wazee wale wa kitambo enzi za ujamaa ningeelewa, ila hawa ni vijana wa kisasa waliosomea UDOM na UDSM elimu ya kisasa ambao nlitegemea watakua wameboreshwa kimtazamo kwenye masuala ya dunia ya leo hii ya utandawazi.

Mama amesema Watanzania watakuja kuwekeza kwa nguvu hapa Kenya....hehehe yaani hawa hawa Watanzania hawa au wengine wataletwa..... hebu soma nyuzi kama hizi.

Majitu ya Chato ni ya hovyo sana.
 
Wakenya ni wanafiki tu na roho mbaya waliorithishwa na mzee wao mganga wa kienyeji Jomo Kenyatta.

Jomo Kenyatta mramba miguu ya wazungu ndio chanzo kikubwa kwa Nchi za East Afrika kutoungana,alikuwa anawapelekea umbea.
 
Toka ule muungano wa east africa wa kwanza ulipovunjika,hamna jirani anayewaamini wakenya,uhuru alimjazia lundo la mambo ma yetu,ajira bila permit work,utalii,aviation,bomba la gesi,kama ni muelewa kwenye hotuba zake zote mama amekomaa kwenye ushirikiano wa biashara tu,angethubutu pale na yeye kusema wakenya na wao waje tu TZ kufanya kazi bila permit work kesho huko mipakani kusingetosha
 
Halafu Kiswahili cha huyu mama kimenyooka hadi raha, lafudhi ya Kizanzibari, kama ya ndugu zetu wa Mombasani, yaani ametukosha sana Wakenya, amesababisha niendelee kukipenda Kiswahili zaidi na zaidi.
 
Kwa hivyo mama ni Vasco Da Gama wa ziara zisizokua na tija?
Subiri miezi sita. Ihifadhi hii comment. Tanzania ipo na sera zake juu ya Kenya, hazibadiliki. Mtaanza kupiga kelele vilevile tena.
 
Mama anataka muamke na kushindana, muache kuwa waoga waoga na wazembe wa kutupwa, muache kulialia.
Kwanza viwanda vyetu vitaunga kwenye gesi yenu hiyo moja kwa moja, hadi raha, ndio tutazalisha yaani tu basi.
Watanzania wengi wamejiajiri kwenye kilimo, uvuvi,ufugaji, utalii, misitu, biashara nk

Zaidi ya 60% ya malighafi za viwanda vya Kenya zinatoka Tanzania

Kenya ni jangwa ni barren country ndio maana wakenya diaspora ndio wanaongoza kuingizia Kenya forex through remittance kuliko utalii, export business na kitu chochote

Hii pekee ni indicator kwamba Kenya haina mazingira na haifai kwa uwekezaji

Unategemea mtanzania aje kufanya nini huko zaidi ya kuleta mazao na ready made products? Cha muhimu fungueni mipaka wa Tanzania tulete mazao yetu ya kila aina msiendelee kufa njaa.
 
Sijawahi kuwaamini wakenya hata siku moja, vijamaa vijanja janja sana halafu full uzalendo usitegemee ukafungue biashara kenya halafu mkenya aache biashara za mkenya mwenzie akuungishe mtz! nehi
Sio uzalendo

ukabila
 
I like this lady so far.... she's seems to be pragmatic. Let's see how things pan out from here

Hapo pa kuunga viwanda vyetu kwenye gesi yao pamenipa raha sana, mama amefungua biashara, ameaumua aidha Watanzania waendelee na uwoga uwoga wao au waone majirani wakinufaika na raslimali zao.
 
Sijawahi kuwaamini wakenya hata siku moja, vijamaa vijanja janja sana halafu full uzalendo usitegemee ukafungue biashara kenya halafu mkenya aache biashara za mkenya mwenzie akuungishe mtz! nehi

Siyo uzalendo tu bro. Ukabila, wenyewe hata mambo ya kipuuzi ni ukabila tu. Mjaluo akiingia bar ya wakikuyu, wale wahudumu wakigundua ni jaluo, wanaanza kum'beza au hata kuto muhudumia ipasavyo. Au hata mkikuyu akipita karibu na bar ya wajaluo, utakuta hiyo bar ya jaluo hiyo, twende zetu huku.
Hata kuoa hivyo hivyo, yaani kijana akimzikia binti mpaka mwisho, unaishia kutamani tu. Maana siku ukimleta kwenu, utakoma wazazi wako watakavyokuzodoa. Umetulea nini hapa, utafikiri wenyewe ndiyo wanaishi naye, wakati wewe ndiyo unaenda kukaa naye.
 
Back
Top Bottom