Rais Samia ni Mwanamikakati, anasafiri kimkakati

Chee4

Member
May 17, 2021
35
125
Nimekuwa natafakari sana kauli aliyosema Rais Samia Hassan wakati akihutubia wazee wa Dar es salaam siku chache zilizopita kuwa ataanza safari za kujitambulisha kwa majirani zetu bila kupata jibu.

Sasa jibu nimelipata, kumbe Rais Samia ni mwanamikakati na mchumi mzuri sana anasafiri kimkakati.

Mpaka sasa Rais Samia ametembelea nchi za Uganda, Burundi, Msumbiji, Kenya na Rwanda.

Ukiangalia safari za Rais Samia katika nchi nchi ndo utajua kuwa ni mwanamkakati mzuri sana, ambaye vijana wa zamani wangesema anacheza cha Pele.

Tukianza na uganda ambapo Rais Samia ameenda mara mbili utagundua kuwa uganda na Tanzania tunafanya biashara kubwa sana kupitia mipaka yetu, majini na angani. Sio hilo tu Tanzania na uganda sasa inatekeleza mradi mkubwa wa bomba lefu kuliko yote la Mafuta barani Afrika ambapo asilimia kubwa linapita katika nchi ya Tanzania.

Ukiangalia mambo haya na suala zima la ushirikiano mzuri kati ya Uganda na Tanzania unaona kuwa Rais Samia anahitaji kuimarisha uhusiano huu wa kiuchumi, kidiplomasia na kisiasa kwa manufaa ya Tanzania na watanzania kwa ujumla.

Kwa upande wa Kenya ambapo Rais Samia alikuwa huko siku za karibuni utagundua kuwa Kenya na Tanzania ni mabwana wawili wa uchumi mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo takwimu zinasema muda si mrefu Tanzania itaipiku Kenya kiuchumi sababu ya miradi ya kimkati ya Reli ya Kisasa ( SGR), bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda, Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 likikamilika, mabarabara na mambo mengine ya mazingira mazuri ya uwekezaji.

Miradi yote Kenya ni mshirika mzuri tegemewa kwa mfano kupitia Bwawa la Mwalimu Nyerere Tanzania tutaiuzia Kenya umeme wa bei Rais.

Kupitia Reli ya Kisasa Tanzania itaungana na Kenya kwa upande wa kisumu. Na kama hiyo haitoshi ziara ya Rais Samia Kenya ilikuja na suala la ujenzi wa bomba la gesi kutoka bandari ya Dar es salaam hadi Nairobi ili Kenya ipate gesi ya bei nafuu kutoka Tanzania.

Kama hiyo haitoshi Kenya inanunua mazao mengi ya chakula kutoka Tanzania na kufanya biashara nyingi na Tanzania katika mipaka ya Tanzania. Bila Rais Samia kuimarisha uhusiano huu wa kiuchumi na Kenya Tanzania haiwezi kuendelea fedha za kigeni.

Rais Samia baada ya kutoka Kenya ameenda Burundi. Hii nchi ya Burundi ukiachilia uhusiano na Tanzania wa kisiasa na kidiplomasia ni mbia mkubwa kibiashara na Tanzania.

Ikumbukwe Burundi haina Bandari mizigo yao yote inapita Tanzania. Na katika mipaka yake na Tanzania kama kigoma kuna biashara kubwa na nyingi zinaendelea kati ya nchi hizi mbili.

Wanasema biashara ni matangazo bila Rais Samia kwenda Burundi na kuimarisha uhusiano huu wenye bandari katika ukanda wa Afrika Mashariki ni wengi wanaweza kutupiku.

Kuanzia leo hadi kesho Rais Samia ana ziara ya siku mbili nchini Rwanda.

Rwanda ni nchi ndogo sana lakini ni muhimu sana katika uchumi wa Tanzania.

Ikumbukwe Rwanda ni nchi isiyokuwa na bandari na mizigo yao yote inapita hapa Tanzania.

Pili, Rwanda na Tanzania wanashirikiana kujenga mradi mkubwa wa umeme huko Rusomo kwa ajili ya chumi za hizi nchi mbili.

Tatu, Tanzania kupitia mradi wake wa reli ya kisasa inaungana na Rwanda kupitia Isaka. Kwa hiyo mizigo toka Tanzania kwenda Rwanda itakuwa inapita isaka na kipande hiki kimeishazinduliwa cha reli.

Nne, Tanzania na Rwanda zinashirikiana katika suala la TEHAMA. Ikumbukwe Tanzania imesambaza mkongo wa mawasiliano katika nchi za Afrika Mashariki na inataka na Rwanda ipewe huduma hiyo. Haya yote yanahitaji ushawishi mkubwa na wakaribu kutoka kwa Rais Samia.

Hongera sana Mwanamkakati wa nyakati za sasa najua utaenda Zambia, DRC na nchi nyingine za maziwa makuu kwani zinakusubiri nasi Tanzania tunazihitaji kiuchumi kwani tuna deni la kuingia katika nchi za uchumi mkubwa.

Unachofanya unaendeleza mazuri ya watangulizi wako ili kufikia uchumi wa juu na kuongeza kipato cha watanzania cha kila siku.
 
Ameenda kupewa mbinu za kuwazingua kiistaraabu wenzake wakati akiwania kiti mwaka 2025!!kumbuka kagame na kikwete ni maadui!!sasa anaomba msaada wa kimbinu ili akichukua fomu tu asizinguliwe!!!!
 
Nimekuwa natafakari sana kauli aliyosema Rais Samia Hassan wakati akihutubia wazee wa Dar es salaam siku chache zilizopita kuwa ataanza safari za kujitambulisha kwa majirani zetu bila kupata jibu...
Aondoe kodi haramu ya miamala ya simu.
 
Hayo yote uliyoandika ni ya kusadikika.

Alipoenda Kenya mkasema Sasa mtaenda Kenya kufungua sijui biashara sijui nini, mmefikia wapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom