Rais Samia ni bora angesubiri kwanza achaguliwe Mwenyekiti wa CCM Taifa ndio ahutubie Bunge?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Katika hali ya kawaida, Rais Samia atapaswa kuwa mnyenyekevu na mpole kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM unaotaraijiwa kufanyika April 30 mwaka huu(nimesoma mahala), mkutano utakaokuwa na jukumu la kumchagua mwenyekiti wa CCM Taifa huku mama Samia akitarajiwa kuwa ni mgombea pekee.

Kwa mantiki hiyo, sioni uwezekano wa Rais Samia kuwa huru na kufunguka mbele ya wabunge wa CCM atapohotubia Bunge hiyo kesho zaidi ya kulazimika kuwa mpole mbele ya wapiga kura wake iwapo ni kweli haridhishwi na mwenendo wa wabunge licha ya kuwa hapaswi kuingilia Bunge kama mhimili unaojitegemea.

Hata hivyo, hali inaweza kuwa tofauti iwapo Mama Samia anataka kutumia sehemu ya hotuba yake Bungeni kujiipigia kampeni na hili tutaligundua kutokana na aina ya hotuba atayoitoa hiyo kesho.

Uwezekano wa Rais Samia kuchaguliwa upo na ni mkubwa tu, ila pia upo uwezekano wa yeye kuweka rekodi ya kupata ushindi mdogo kulinganisha na watangulizi wake. Hii inatokana na hali iivyo hivi sasa ndani ya CCM na kama inavyojidhihirisha hata ndani ya Bunge.

Hivyo, kama Mama Rais Samia anataka kufunguka ndani ya Bunge, ni bora asubiri uchaguzi upite, ila kama yuko kwenye kampeni, basi ameona mbali na itabidi awe mpole tu mbele ya wabunge wa CCM (wajumbe wa mkutano mkuu).

Nawasilisha.
 
Ushindi ni ushindi tu bora tu uwe wa haki bila dhulma wala ulaghai! Unachopendekeza kwa mama ni kuwa awe mnafiki aongee mambo ya kuwafurahisha wabunge ili achaguliwe kwa kura nyingi baada ya hapo aongee ukweli anaouamini.

Huo kwa kiswahili unaitwa ULAGHAI au UNAFIKI. Kama na wewe ni muumini wa huo utamaduni basi una matatizo ya kimsingi na huna msaada kwa Mama.
 
🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Samia Suluhu Hassan ndio Rais halali wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Aanze na kikao chochote hakuna kinachomtisha wala kumpa hofu

Mungu ibariki Tanzania
 
Rais nchi hii ana nguvu kubwa sana. Sioni hata mtu mmoja anayeweza kuzuia Samia kuwa chairperson
Kuna watu wana akili za kenge. Kuumia mpaka waone damu.

Hivi kama Speaker wa bunge anasimama mbele ya Rais utafikiri kapigwa mvua ya mawe, wewe kama mbunge wa kawaida au mwanaCCM wa kawaida utafanyaje?

Yaani ukitaka kujua hakuna mwanaCCM mwenye ubavu wa kupiga kura ya hapana, kura ziwe za wazi🤣🤣🤣🤣
 

Samia Suluhu Hassan ndio Rais halali wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Aanze na kikao chochote hakuna kinachomtisha wala kumpa hofu

Mungu ibariki Tanzania
*****, hata wewe umeanza kumuunga mkono mama Samia???

Ama kweli njaa haina adabu.

List ya wasaliti inazidi kuongezeka!
IMG_20210411_210346_368.JPG
 
Aisee! Kwamba mama ashindwe kutoa hotuba ya kueleweka bungeni akiogopa wabunge hawatamchagua kuwa mwenyekiti wa chama!!
Tunaweza kuwa na rais wa dizaini hiyo kweli mkuu?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom