Well said.Mpendwa Mama Samia,
Nchi hii haiwezi kujengwa kwa kuomba omba. Nchi inajengwa kwa kazi, bidii, na nidhamu ya utumishi wa umma.
Nchi yetu imebarikiwa kila aina ya rasilimali: Maji, Mito, Mabwawa makubwa, maziwa, madini ya kila aina, gesi, mafuta, chakula, nishati, ardhi kubwa yenye rutuba, nguvu kazi watu, mbuga, misitu, na kila aina ya rasilimali.
Kwa mambo hayo yote, hatuwezi kubabaikia wawekezaji. Wao ndio wanapaswa kutubabaikia sisi.
Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza. Kama tunavyo vitu vizuri, lazima waje wenyewe. Hizi ni basic principles za uchumi.
The Higher they demand, the better the price we get.
Unapojitembeza hovyo kwa wazungu kila kukicha wewe uko angani unaonekana Rais wa bei nafuu tu... Hamna watakachokupa zaidi ya kukutwika dozi za machanjo ya corona.
Halafu pia huko kuzunguka kwenda Ulaya mimi sijaona lolote la maana zaidi ya kunywa JUISI na wazungu tu na kuongea nao VIINGEREZA VISIVYOELEWEKA unabaki kuitikia tu YES YES YES YES YES... huku unatikisa kichwa kana kwamba unawaelewa kumbe hamna lolote!
Ukimaliza kunywa JUISI Ulaya unarudi unatuambia umetoka kutafuta wawekezaji!!!!!!
Hatuwezi kuendelea kama nchi kwa kuabudu wazungu. Lazima tutambue thamani tuliyo nayo na tujifunze kujitegemea. Itatuongezea potential.
Hii dependency syndrome inaua nchi. Ndio maana mnakabidhi wachina bandari kwa miaka hamsini na kwa bei chee ya kitapeli. Ati wahisani!!
Hatuwezi kuwa maomba omba milele. Jenga nchi! Tuache kuzurura hovyo!
Umegongelea pale penyewe.
Anatakiwa ajifunze kwa jiraani yake
Paul KAGAME. Hata Uhuru yuko powa na maendeleo wanayo.
Sisi kulilia wakati kila kitu iko!
Shida kubwa ni watendaji nao wahovyo! Hata wabunge hawajui kazi zao wakiongozwa na Rundungai wao!!