Rais Samia: nataka itumike "Single Source." Je, "Force Account" za JPM na "Zabuni Shindanishi" za JK zimeishia wapi? Sheria ya manunuzi imefutwa?

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,463
2,289
Leo wakati Rais akizindua mpango wa maendeleo (tafsiri "matumizi") ya pesa ya Covid kutoka IMF, amesema anaagiza watumie "single source" kwenye manunuzi na kandarasi. Kasema zabuni za kawaida zinatuchelewesha, hataki kuzisikia.

Swali langu lina sehemu mbili tatu:

hivi taratibu za matumizi ya zabuni shindanishi haziko kisheria ?

the biggest political upheaval ever in this country, ukiondoa Nyerere kufukuzwa Ikulu na jeshi kwa masaa 48, ni pale Prime Minister Lowassa na Principle Secretary Msabaha na wengine walipotimuliwa na shinikizo la tume ya Mwakyembe kwa kushindwa kuzingatia taratibu za manunuzi na zabuni, procurement and tendering.

likaja wimbi kubwa la kutilia mkazo mambo ya procurement, watu mpaka mameneja kwenye mashirika na mawizara wakapelekwa vyuoni na kwenye ma semina kusomea kozi za procurement, sheria ikawa amended ikapewa meno, ikaundwa regulatory body inayoshughulikia procurement tu.... tunakumbuka ?????

haya, akaja Marehemu, akawa anauliza maafisa manunuzi na wakurugenzi wa Halmashauri majukwaaani, mnatumia "force account" ? Force account ikawa force account.

sasa leo Rais Samia katangaza anaagiza watumie "single source."

Single source ni nini?

Force account ni nini?

Na zabuni shindanishi zimefutwa lini?

na kwa nini zilikuwa haliteti tija ?

toka single source and force account zije na Magufuli tumeacha kupigwa? Kwa ripoti gani?

Na Rais anawezaje kufuta sheria ya bunge thabiti jukwaani ?????
 
Hapo Sasa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Kaleta Mchanyato, Mseto Kuna Mamlaka Zitashindwa Kufanya Kazi Zake

Hii Sasa Hivi Imewaibua Watu Kwenda BRELA Haraka Kusajiri Kampuni Tayari Kwenda Kupiga
Acha Tuone Japo Mupe....Muruke.....
 
Kila Rais anayekuja anajiamulia anachotaka, ndio maana taifa linazidi kudumaa kimaendeleo kwasababu hakuna succession plan, halafu wakiambiwa kuhusu Katiba Mpya wanajibu hawaihitaji kwasasa ili wazidi kutuvuruga tu, na wale wajinga wengine wanasema Katiba Mpya haina maana itakuwa ya Chadema.
 
Leo wakati Rais akizindua mpango wa maendeleo (tafsiri "matumizi") ya pesa ya Covid kutoka IMF, amesema anaagiza watumie "single source" kwenye manunuzi na kwenye kandarasi. Kasema zabuni za kawaida zinatuchelewesha, hataki kuzisikia.

Swali langu lina sehemu mbili tatu:

hivi taratibu za matumizi ya zabuni shindanishi haziko kisheria ?

the biggest political upheaval ever in this country, ukiondoa Nyerere kufukuzwa Ikulu na jeshi kwa masaa 48, ni pale Prime Minister Lowassa na Principle Secretary Msabaha na wengine walipotimuliwa na shinikizo la tume ya Mwakyembe kwa kushindwa kuzingatia taratibu za manunuzi na zabuni, procurement and tendering.

likaja wimbi kubwa la kutilia mkazo mambo ya procurement, watu mpaka mameneja kwenye mashirika na mawizara wakapelekwa vyuoni na kwenye ma semina kusomea kozi za procurement, sheria ikawa amended ikapewa meno, ikaundwa regulatory body inayoshughulikia procurement tu.... tunakumbuka ?????

haya, akaja Marehemu, akawa anauliza maafisa majukwaaani, mnatumia "force account" ? Force account ikawa habari ya mjini.

sasa leo Rais Samia katangaza anaagiza watumie "single source."

Single source ni nini?

Force account ni nini?

Na zabuni shindanishi zimefutwa lini?

na kwa nini zilikuwa haliteti tija ?

na ni wapi wameona single source au force account ni bora zaidi? Kwa ripoti gani?

tumeacha kupigwa kwenye makandarasi toka single source and force account zije ?

Na Rais anawezaje kufuta sheria ya bunge thabiti jukwaani ?????
Mkuu mbona alifafanua vizuri kabisa,kwamba hizi pesa tulizopewa inabidi tuzitumie kwa muda wa miezi Tisa kukamilisha hiyo mipango yetu...

Sasa tukisema tufuate taratibu za manunuzi ya serikali au kugawa tenda basi miezi Tisa itafika na tutakua hatujafanya jambo lolote maana taratibu za ugawaji tenda au manunuzi za serikalin zinatumia muda mrefu.

Kwaio akapendekeza itumike njia ya single source ili kukimbizana na muda ...shughuli nyingine za kwenye miradi mingine wataendelea kama kawaida na force account.
 
Single source ni pale anapatikana mkandarasi bila kumshindanisha na wengine. Mnamteua kwa vigezo vyenu, mna bargain bei, mnaingia nae mkataba. Nadhani athari zake kila mmoja anaziona. Mojawapo ni makampuni yanayofahamika tu ndio yatapata tenda. Yale yanayochipuka ndio basi. Nyingine ni katika hiyo hatua ya kuelewana.

Amandla...
 
Force account ni bomu. Single source ni bomu. Walichotakiwa ni kuchagua miradi inayotekelezeka katika muda husika. Kwa mfano, kuwanunulia vifaa vya kujikinga madaktari na wauguzi, kuweka vifaa vya kupima katika kila kitongoji n.k. Kutaka kujenga madarasa ndani ya miezi mitatu ni kujitafutia matatizo.

Amandla...
 
Kwaio akapendekeza
Hajapendekeza. Katamka "naagiza" itumike single source.

Kuna watu walifungwa jela kwa kutofata sheria ya manunuzi. Samia aende bungeni kufuta sheria kwanza.

Viongozi wamejifunza nini kwa DC Sabaya ?

Leo Samia akiitwa na Mungu ghafla utetezi wa "niliagizwa na mamlaka ya uteuzi" hautakuwa na mashiko mahakamani kama mamlaka ya uteuzi mwenyewe keshakufa.
 
🚣..habari za jioni
Sisi wengine tutakusaidia kupiga Kasia tuu🤸🚣🏊.washiriki mliopewa upendeleo msituangushe tafatali tusio na hii fursa tunawasikilizeni Kwa hamu kubwa na utulivu. Tunatanguliza shukrani, sisi wakosa hii fursa.
 
Hajapendekeza. Katamka "naagiza" itumike single source.

Kuna watu walifungwa jela kwa kutofata sheria ya manunuzi. Samia aende bungeni kufuta sheria kwanza.

Viongozi wamejifunza nini kwa DC Sabaya ?

Leo Samia akiitwa na Mungu ghafla utetezi wa "niliagizwa na mamlaka ya uteuzi" hautakuwa na mashiko mahakamani kama mamlaka ya uteuzi mwenyewe keshakufa.
Mbona huwa mnapenda kupotosha mambo bila sababu?

Utaratibu wa single sourcing upo kisheria,na umekuwa ukitumika mara nyingi katika manunuzi ya serikali pale inapohitaji huduma za dharura.

Iko hivi, angalau watoa huduma watu wanaombwa kutoa bei zao,halafu mwenye bei ya kuridhisha anapewa kazi.
 
Single source ni pale anapatikana mkandarasi bila kumshindanisha na wengine. Mnamteua kwa vigezo vyenu, mna bargain bei, mnaingia nae mkataba. Nadhani athari zake kila mmoja anaziona. Mojawapo ni makampuni yanayofahamika tu ndio yatapata tenda. Yale yanayochipuka ndio basi. Nyingine ni katika hiyo hatua ya kuelewana.

Amandla...
Kwa mtindo huu rushwa itatamalaki na vikampuni vya mifukoni vingi vitaanzishwa, mwendazake alilaumiwa kwa Mayanga Construction huyu nae anajitengenezea mazingira.
 
Leo wakati Rais akizindua mpango wa maendeleo (tafsiri "matumizi") ya pesa ya Covid kutoka IMF, amesema anaagiza watumie "single source" kwenye manunuzi na kandarasi. Kasema zabuni za kawaida zinatuchelewesha, hataki kuzisikia.

Swali langu lina sehemu mbili tatu:

hivi taratibu za matumizi ya zabuni shindanishi haziko kisheria ?

the biggest political upheaval ever in this country, ukiondoa Nyerere kufukuzwa Ikulu na jeshi kwa masaa 48, ni pale Prime Minister Lowassa na Principle Secretary Msabaha na wengine walipotimuliwa na shinikizo la tume ya Mwakyembe kwa kushindwa kuzingatia taratibu za manunuzi na zabuni, procurement and tendering.

likaja wimbi kubwa la kutilia mkazo mambo ya procurement, watu mpaka mameneja kwenye mashirika na mawizara wakapelekwa vyuoni na kwenye ma semina kusomea kozi za procurement, sheria ikawa amended ikapewa meno, ikaundwa regulatory body inayoshughulikia procurement tu.... tunakumbuka ?????

haya, akaja Marehemu, akawa anauliza maafisa majukwaaani, mnatumia "force account" ? Force account ikawa habari ya mjini.

sasa leo Rais Samia katangaza anaagiza watumie "single source."

Single source ni nini?

Force account ni nini?

Na zabuni shindanishi zimefutwa lini?

na kwa nini zilikuwa haliteti tija ?

na ni wapi wameona single source au force account ni bora zaidi? Kwa ripoti gani?

tumeacha kupigwa kwenye makandarasi toka single source and force account zije ?

Na Rais anawezaje kufuta sheria ya bunge thabiti jukwaani ?????
Mkuu single source hutumika kwa case ya miradi ya dharura( uharaka) au miradi yenye unyeti( confidential) hivyo mh. Rais ameona time tuliyonayo ni ndogo kwa mpango husika kwa hiyo miradi mingine itaendelea kufuata utaratibu wa kawaida either forced account au competitive tendering.
 
Sifa za miradi kuitwa "nyeti" au ya "dharura" zimeainishwa wapi? au itategemeana na mawazo ya muhusika? anaweza kuuita mradi wowote aupendao "nyeti" au wa "dharura" ili kuhalalisha hiyo single source.
 
Single source ni pale anapatikana mkandarasi bila kumshindanisha na wengine. Mnamteua kwa vigezo vyenu, mna bargain bei, mnaingia nae mkataba. Nadhani athari zake kila mmoja anaziona. Mojawapo ni makampuni yanayofahamika tu ndio yatapata tenda. Yale yanayochipuka ndio basi. Nyingine ni katika hiyo hatua ya kuelewana.

Amandla...
Bora force account
 
Mkuu single source hutumika kwa case ya miradi ya dharura( uharaka) au miradi yenye unyeti( confidential) hivyo mh. Rais ameona time tuliyonayo ni ndogo kwa mpango husika kwa hiyo miradi mingine itaendelea kufuata utaratibu wa kawaida either forced account au competitive tendering.
Miradi hiyo ni kama vile ujenzi wa uwanja wa ndege chato na ununuzi wa ndege kwa cash money
 
Back
Top Bottom