Rais Samia, nasikitishwa na mateso anayopitia Mbowe katika utawala wako

Kishenge

Member
Oct 20, 2021
53
139
Binafsi mimi ni kijana mdogo sana. Naomba nisema Mh. Rais Samia shikamoo.

Mh. Rais nasikitishwa na mateso anayopitia mzee Mbowe kwa baraka za utawala wako, sikudhani wewe ungekuja kuongeza mikanganyiko ya kisiasa nchini.

Naomba ujiulize maswali yafuatayo kisha ufanye yakupendezayo mama angu.

1. Unadhani kikombe/mateso anayopitia mzee Mbowe unaweza kuyapitia wewe binafsi?

2. Unadhani kumsingizia mtu kutaiponya nafsi yako mama angu mpendwa?

3. Unadhani familia ya mzee Mbowe haimuhitaji kama ambavyo ya kwako inakuhitaji?

4. Kama kweli wewe mzalendo kwanini unaogopa katiba mpya?

5. Kama kweli mbingu ipo unahisi utairithi kwa kufumbia macho mateso ya wenzio?

6. Je, Wewe nafsi yako inakwambiaje kuhusu kesi ya mzee mbowe?

Hili nalo lichukue mama.

Hivi unajua kinachoendelea kwenye vifaa vya ujenzi? kama unajua, je, Unadhani maisha ya Watanzania umeyaboresha ili kuweza kumudu mfumuko wa bei ambao haujawahi kutokea kwa miaka 20?

Hii si yako.

IGP sirro kila nikitaka kuandika juu yako nashindwa mzee wangu, hivi Mzee Mbowe alikula nini chako umma ujue? Mbona chuki yako dhidi yake inakuwa kubwa sana?

Mbona ulivyopewa maelekezo kumkamata Gwajima uligoma? Nahisi ulisimamia taaluma yako, lakini inapokuja swala la Mbowe hujiulizi mara mbili bali unamshushia kikombe cha mateso haraka sana kuna nini kati yako na Mbowe? Mungu asikupungukie Mzee wangu Sirro ila unachokitenda sidhani kama kitakupa faraja.
 
YALIYOPO MAHAKAMANI TUJIFUNZE KUYAHESHIMU
Kesi itachakatwa kwa Shahid za upande zote,hatimaye HAKI itapatikana.
 
Usijifanye unazijua sana siasa kijana.

Watu wanaovamia siasa kwa mihemko ndio wanaishia kama kina Ben Saanane, Alphonce Mawazo, Lissu.

Vijana mihemko wa CHADEMA mnamwonaga Mbowe kama mungu, eti ni mkombozi, anajitolea, anapambania wanyonge sijui nini ???

CHADEMA mwaka 2010-15 ilikuwa inapata ruzuku zaidi ya Tsh 300M kwa miaka mitano.

Na baada ya 2015-20 baada ya wimbi la Mamvi, ikaanza kupata ruzuku ya Tsh 400M kila mwezi kwa miaka mitano.

Wabunge wote wa CHADEMA ni lazima kukichangia chama.

CHADEMA ekuwa ikipokea misaada kutoka chama rafiki kutoka Ujerumani cha CDU.

Lakini sasa hivi CHADEMA ina nini?

Ukitoa vile vigali vya PR?

Ndani ya hii miaka 10 tulichoshuhudia ni Mbowe kufungua mabiashara mapya DUBAI.

Hivi ninyi vijana mihemko mnadhani watu wote ni wajinga?
 
Binafsi mimi ni kijana mdogo sana. Naomba nisema Mh. Rais Samia shikamoo.

Mh. Rais nasikitishwa na mateso anayopitia mzee Mbowe kwa baraka za utawala wako,,,sikudhani wewe Mama ungukuja kuongeza mikanganyiko ya kisiasa nchin...
Ataachiliwa kesho kutwa sikukuu ya mashujaa kuna msamaha wa wafungwa utatolewa nae ataachiliwa japo alukuwa sio mfungwa
 
Back
Top Bottom