Rais Samia, nasikitishwa na mateso anayopitia Mbowe katika utawala wako

Ningetamani hoja zako hizi zikitane na mtu anaejitambua ili aweze kufanya upembuzi yakinifu.
Lakini kwa bahati mbaya unaelekeza hoja kwa mtu ambae hapo alipo ni kwa kudra tu za Mungu hajui lolote kuhusu hiyo nafasi aliyoipata kwa kudra.

Analoambiwa yeye ndio huliamini maana cha kupambanulia sioni kama anacho.

Kina sirro waliomlisha mbigiri za kwamba Mbowe ni gaidi wanamjua fika.

Hadi hapo watakapo fikiri vinginevyo na wamjulishe kwamba uchunguzi wetu wa kina umebaini tofauti na mawazo yetu ya nyuma. Mbowe siyo gaidi ndio hapo na mama nae utamsikia akisema Mbowe sii gaidi.

Sii gaidi kwa maana amejiridhisha bali tu kwamba ni kauli aliyolishwa.

Sarakasi za sirro ni kutaka kuficha uhuru wa haki ya kuhoji akijishtukia kama ikiwepo basi yeye ni mhanga wa mauaji yote yaliyofanywa kipindi cha Magu.

Hivyo ameamua kutotoa nafasi ya maridhiano lisijewepo suala la jopo la kimahakama kuchunguza madhila ya awamu iliyopita.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Huo ni ujinga namba Moja ulioandika mbowe anapitia mateso kama malipo ya aliyoyafanya Tena ni madogo sana hayo aeleze alikowaficha kina saanane...
Yani Mbowe anaua watu wote hao bado jamhuri inamtazama tu!!!? Nadhani chuki imekuongoza kusema hayo.
 
Binafsi mimi ni kijana mdogo sana. Naomba nisema Mh. Rais Samia shikamoo.

Mh. Rais nasikitishwa na mateso anayopitia mzee Mbowe kwa baraka za utawala wako,,,sikudhani wewe Mama ungukuja kuongeza mikanganyiko ya kisiasa nchini...
Madaraka matamu sana
 
Malipo ni hapa hapa duniani waache wanaotesa wenzao kwa kes za kusingiziwa Mungu atalipa
 
YALIYOPO MAHAKAMANI TUJIFUNZE KUYAHESHIMU
Kesi itachakatwa kwa Shahid za upande zote,hatimaye HAKI itapatikana.
Mama alivyotamka aliyoyatamka kwenye mahojiano na mwandishi wa BBC hakujua kuwa suala Hilo liko Mahakamani??? Alivyotamka kuwa Polisi waachie kuwabambikia watu kesi alikuwa anamaanisha nn???
 
Binafsi mimi ni kijana mdogo sana. Naomba nisema Mh. Rais Samia shikamoo.

Mh. Rais nasikitishwa na mateso anayopitia mzee Mbowe kwa baraka za utawala wako,,,sikudhani wewe Mama ungukuja kuongeza mikanganyiko ya kisiasa nchini...
Sirro na wenzako hakuna dhambi halali kwa kigezo cha siasa. Mtafariki kwa mateso ya stroke ya mda mrefu mkono moja, mguu moja na mdomo utashuka kuelekea upande mmoja.

Mateso yenu yatadumu kwa miaka mkishuhudia hiyo mihela na migari, mijumba Wana wenu wakiifuja. Mnajisahau muda mchache
 
Usijifanye unazijua sana siasa kijana.

Watu wanaovamia siasa kwa mihemko ndio wanaishia kama kina Ben Saanane, Alphonce Mawazo, Lissu...
Brother ebu tupe ushahidi wa hayo uliyaandika.

Na kingine jamaa alichokiandika hapa ni swala la Mbowe kunyimwa haki yake na sio maswala ya ruzuku.
Na hata km anafungua mabiashara kupitia hizo ruzuku kwani TAKUKURU si ipo.

JESHI LA POLISI si lipo.
MAMLAKA ZINAZOSHUGHULIKIA si zipo....?

M ninaimani km utapewa ukiendeshe chama ndani ya miezi 6 tu, basi utauza kila kitu
 
Nakushauri hivi; Unapo ongelea jambo la kisheria jaribu kupata muongozo kidogo kwa wenye uelewa wa sheria japo kidogo na ukikosa wa kukuelekeza; Unaweza kuandika hapa kwenye jukwaa kuomba uelekezwe
 
Nakushauri hivi; Unapo ongelea jambo la kisheria jaribu kupata muongozo kidogo kwa wenye uelewa wa sheria japo kidogo na ukikosa wa kukuelekeza; Unaweza kuandika hapa kwenye jukwaa kuomba uelekezwe
Asante ila bado napinga Mbowe kuonewa!! Hata wewe ukionewa ntakataa
 
Hao jamaa wamekusudia kumfunga Mbowe sio Samia pekee yake ni Sirro na genge lake akiwemo waziri mkuu na waziri wa utumishi na utawala.
Wanaona Mbowe ni kikwazo kwa Samia kutawala ...ili atawale vema wamfunge Mbowe.
Kuna uwezekano kuwa Mshtakiwa Khalfan Bwire akawa pia upande wa Jamhuri kwa vitisho walivyompatia huko gerezani.
 
CCM tunasema hivi, mnamchapa mchungaji wenu ili kondoo wake watawanyike...

Lakini tangu tuanze zoezi hili ndiyo kwanzaa wanajikusanya.
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom