kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,233
- 12,508
Rais wetu mama, Tanzania ni ya watanzania wote, na kila RAIA ni muhimu sana kwa nchi yake. Watanzania hawana kwao kwingine ila Tanzania.
Kilichompata Tundu Lissu ni vigumu kuamini kwamba yuko hai hadi Leo.
Tundu Lisu amepata maumivu makubwa sana ya kimwili, kisaikolojia, kijamii na kiuchumi. Anahitaji MTU muhimu wa kumwambia pole. Kama mfariji mkuu tafadhali mfariji huyu RAIA wako mwenye weledi mkubwa wa sheria.
Tumuite nyumbani aungane na watanzania wengine kwenye ujenzi wa nchi yao, kufanya hivyo dunia itatutukuza kama taifa.
Tumlipe anachostahili kama kipo, tumhakikishie usalama wake kama anayo hofu, tumrudishe nyumbani kama hawezi.
Vyama vingi ni mfumo ambao uko kwenye katiba yetu, usiwe uhasama bali tuendeshe kwa staha kwakuwa ulibuniwa na wazungu bila ya sisi kujitayarisha ili tuvurugane wenyewe kwa wenyewe.
Nadhani Tanzania yetu ni kubwa kuliko vyama vya siasa. Vyama vinakufa lakini taifa halifi.