Rais Samia, "nakuamuru" uwajengee Kivuko Wananchi wa Ipatikana na Nzoka Mkoa wa Songwe

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Salaam Wakuu.

Kwa mjibu wa Katiba, rais ameajiriwa na Wananchi kuwatumikia. Hivyo kama Mwajiri, namtaka au namuamuru rais Samia awajengee kivuko hawa Wananchi. Ziara yake moja inatosha kuwawekea kuvuko hawa wananchi.

Nimefika Nzoka Momba, Wananchi wanavuka kama Makomandoo unaweza hisi ni mafield marshal.

Pamoja na kwamba wanalipa kodi na Tozo, bado Wananchi wa Momba Mkoani Songwe wanaendelea kuiomba Serikali kuwajengea kivuko kinachounganisha Kata mbili za Nzoka na Ipatikana kutokana na kuvunjika kwa kivuko cha awali kwa zaidi ya miaka minne sasa. Kata zote zina Viongozi wa CCM.

Wanafunzi, wajawazito na Wazee, wanapita kwa kubembea kama Kima.

Mkuu wa Mkoa na Wilaya wafukuzwe kwani hawakusaidii. Utakosaje hela ya kujenga sehemu hii kwa miaka minne?

Pia namtaka Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG akakague hela za Ujenzi zilizotumika na bado hili daraja halikujengwa. Wilaya ya Momba, Mkoani Songwe, ilitumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.507,936,715.62 kwa ajili ya ujenzi lakini hili daraja halijajengwa.

Pia Milioni 100 zilizobaki kwenye Ujenzi wa madarasa(Mkopo wa Covid-19 wa Tril 1.3 au Pesa za Samia), zipelekwe kujenga hili daraja sio kurudishwa Hazina.

Natoa Amri.

Nakala kwa:

Mkuu wa Mkoa: Omary Mgumba

Mkuu wa Wilaya Momba: Fakii Lulandala

Mkurugenzi wa Wilaya ya Momba Regina Bieda
 
Hiyo sio kazi ya Samia bali Tarura,Tanroads,na mawaziri wanaohusika na wizara za ujenzi.

Wenzenu wamejengewa kwa kufuata huo ushauri nyie vipi

Screenshot_20220117-203734.png
 
Waajiri mnaombaje tena....!? Si mmeanza na amri?
===
Tumieni lugha rafiki mtasikilizwa.
Ipo siku na haiko mbali sana watu wataanza kudemand mambo mengi tu....muda unabadilika. Sisi wengi hatubadiliki wala kutambua dalili za mabadiliko yanayoendelea huko nje. Tumezoea kula na kuvimbiwa na kuona kama hiyo ni haki yetu ya msingi.
I hope hekima itatuongoza vema
 
sasa kuwajengea katemporary bridge tu hapo RC, DC, RAS, DAS, RPC, nk yaani wameshindwa kabisa kupitia hata akili zao kujenga temporary and safe bridge kwa ajili ya hao Watanganyika...

RPC akiamuru vijana wake waingie road wiki moja tu hapo Songwe hela inapatikana chap....Kuna wakati Ugalu tunaokula inawezekana ukawa sumu..

Hapo kuna mapoli kibao na miti ya magogo tele imejaa mapolini, Wameshindwa kumobilize nguvu kazi na likajengwa daraja la Magogo chapu hapo wakati inasubiriwa permanent solution...

RC na MaDc's wako mmeshindwa hata kuandaa harambee au matamasha hapo Songwe mkialika akina Daimond, Harmonize nk au hata kuziomba Simba na Yanga kucheza friend match hapo Songwe na Songwe UTD ikapatikana hata 200M ikajengwa temporary steel structure hapo chapu.
 
Ningekubaliana na wewe kama ungemshirikisha mkuu wa Magereza mkoa ili atoe nguvukazi ya wafungwa, ila sio RPC aamuru faini za road?,

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom