Rais Samia na hotuba ya matarajio kwa Watanzania

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,037
20,333
RAIS Samia Suluhu Hassan, amezidi kuonyesha ni kiongozi mwanamageuzi, mtu bora na sahihi aliyeandaliwa kuwa kiongozi madhubuti kwa namna anavyowasilisha hotuba zake, ambazo zimekuwa zikivutiwa watu na kutoa mwelekeo thabiti wa Tanzania bora, ambayo inakwenda kufanikiwa chini yake.

Hii inatokana na siku chache amekuwa mtu imara na sahihi anayekwenda kuleta na kuendeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana na kuletwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara na visiwani kwa miaka 59, na ndio amekuwa mwanamageuzi.

Ikumbukwe toka awamu ya kwanza na sasa awamu ya sita watanzania wanataka maendeleo na kwa awamu hii Rais Samia, nchi inakwenda kusonga mbele kutokana na uwepo wa kiongozi thabiti na mwenye mwelekeo bora wa kuwaletea maendeleo wananchi hasa kwa namna anavyowasilisha hotuba zenye kuakisi maisha halisi ya watanzania.

Nionavyo, Rais Samia ni mtu sahihi aliyekuja kwa wakati sahihi katika kuwatumikia wananchi na kwenye serikali hii anakwenda kuonyesha tafsiri sahihi ya kiongozi aliye bora anakuaje hasa kutokana na maono makubwa aliyokuwa nayo katika kuleta ukombozi wa Mtanzania; ambapo katika hotuba aliyoitoa bungeni ameonyesha tafsiri ya uongozi hasa kutokana na kugusia mambo mengi yenye mwelekeo wa kuwagusa wananchi.

Japokuwa amekuwa akisisitiza ataendeleza mambo yaliyoachwa na mtangulizi wake Hayati Rais Dk. John Magufuli, pia ameeleza ataendeleza mipango mbalimbali yenye kuleta utatuzi wa ajira kwa vijana, kupunguza na kuondoa umaskini kwenye kaya kwa kuja na mipango mathubuti ikiwemo kuboresha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ambazo kwa tafsiri za kawaida ni sekta zinazokwenda kugusa watanzania moja kwa moja.

Kilimo ni uti wa mgongo wa nchi, anapokuja kiongozi na kuonyesha mwelekeo wa kuinua sekta hiyo, anaonyesha kuwa ni Rais mwenye maono na mwanga wa maendeleo unaokwenda kuendeleza maendeleo yale yaliyofanywa na viongozi waliomtangulia kwenye sekta ya Kilimo na sekta mbalimbali.

Kiongozi mwenye maono ya kimageuzi ni lazima anatoa hotuba zenye kuakisi maendeleo, anayekwenda kuleta chachu kubwa ya kuijenga Tanzania kutokana na maono aliyokuwa nayo katika muda mfupi kwa kutoa hotuba zenye mwelekeo bora kwa nchi, na kuamsha utayari wa kujiletea maendeleo bora katika nchi.

Tanzania imepata kiongozi bora mwenye maono nguvu kubwa na sio 'kiongozi msakatonge ' ambaye hawezi na hana uwezo wa kusukuma gurudumu la maendeleo lililopo sasa na sio mtu mwenye agenda ya kificho ya kuleta mpasuko na mgawanyiko miongoni mwa jamii za Watanzania au anataka kujinufaisha binafsi na familia yake kama walivyo viongozi wengi wanaopata madaraka duniani.

Sifa za kiongozi bora kwa sasa anazo Rais Samia ambaye amekuwa kiongozi mwenye kujua tafsiri na maana ya uongozi. Rais Samia ni mfuatiliaji wa mambo, mtendaji kazi, mchukia rushwa kwa vitendo, mpenda maendeleo ya Watanzania(Zanzibar na Tanzania Bara) kwa ujumla na mwenye kiu ya kutaka kuleta mabadiliko ya dhati kwa watumishi na wananchi nchini kwa kuwa ana sera bora za kuwatumikia wananchi.

Siasa za Tanzania zinahitaji mtu anayepata Urais kwa kusukumwa na tamanio la kuondoa umaskini na kuleta maendeleo na sio mtu anayeutaka Urais kwa kulisaidia kundi fulani au mataifa ya nje ili aweze kupenyeza agenda zao wanazozitaka kwa. Rais Samia ni jemedari na askari mwaminifu katika kuutukuza Utanzania na kuleta maendeleo kwa wananchi wote na sio pandikizi au wakala wa wasakatonge.

Rais Samia ni ni mtu mwenye uthubutu kwa Watanzania, ambao wapo kwenye kipindi kizuri na hatua muhimu ya kidemokrasia wakati wanapoelekea kwenye kuyatafuta maendeleo yao, hivyo ni wakati wa kila mtanzania kuhakikisha wanamtizama Rais Samia kama mboni na wasikubali kumpoteza kwani ni mtu anayekwenda kulinda utu wa Mtanzania, Muungano na kuleta maendeleo ya dhati ya wananchi na si kwenda kuendeleza siasa za 'ubinafsi'.

Ubora na uimara wa Rais Samia kiuweledi na kiutumishi ndio mambo yanayomtofautisha na watu wengi, yeye ana sifa za upekee na utofauti wake wa uongozi na amestahili kupewa nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania, kutokana na sifa zake za bora, ambazo kupitia matamshi yake anayoyatoa kwenye hotuba zake anaonyesha kabisa mwelekeo thabiti kwa kujibu kero za wananchi kwa utulivu mkubwa na kutoa majawabu nini serikali itafanya katika kufikia maendeleo hayo.

Tanzania Bora ipo na itapatikana kwa uharaka chini ya Rais Samia na atazidi kutukomboa Watanzania kifalsafa, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na hayo yanatokana na upekee wa uongozi wake aliokuwa nao unasimama katika falsafa ya uweledi, utashi, misimamo na maamuzi ikiwa ni pamoja na kuiva kiitikadi na kitaaluma katika nafasi zote alizoshika ikiwemo ya Umakamu wa Rais katika utawala wa awamu ya tano ya Rais Hayati Dk. Magufuli.

Naamini Rais Samia, amekuwa kiongozi mwenye maono 'vision' ya mbali yenye tija na kuyafanyia utekelezaji, ambayo wengine (wafuasi) hawayaoni na ndio maana kila anapozungumza anaweza kugusa maeneo yote muhimu ya kijamii na ninaungana na mtaalamu wa masuala ya uongozi na mwandishi aliyebobea nchini Marekani Warren Bennin anasema; "Uongozi ni kubadilisha maono kuwa uhalisia", ambapo kwa kiasi kikubwa Rais Samia anafanya hayo na kwa kiasi kikubwa hotuba yake kwa Bunge imegusa maeneo yote muhimu kwa umma.

Pia, Rais Samia ni kiongozi bora, ambaye ameonyesha ni mtu wa kutenda kwa kufuata dhamira ambayo hutenda kwa kufuata sauti ya moyo wake, inayomfanya mtu kutofautisha jema na baya kama ambavyo mwanazuoni Stephen R. Covey anasema; "Sauti hii ya ndani ni tulivu na ya amani". Pia "inahusisha kujitoa mzima kwa jambo jema tarajiwa. Ni dhamiri inayotafsiri maono kwa huruma kwa wengine"

Tunaamini, Tanzania iko kwenye mikono salama chini ya Rais Samia, ambaye ameonyesha mwelekeo bora wa kwenda kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini ili waweze kunufaika na kusonga mbele kiuchumi kwanza kwa kuhakikisha anatatua shida na kero za Watanania ambazo kwa namna moja au nyingine zimekuwa ni kikwazo katika kufika kwenye matamanio ya maisha yao.

Hivyo, hotuba ya Rais Samia kwa wabunge na watanzania imeonyesha mwelekeo sahihi wa nchi kwa miaka minne ijayo, ambayo kwa namna moja au nyingine ni wakati kwa watendaji kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza maono makubwa yalioko kwenye hotuba hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwao katika kuwatumikia watanzania.

SIKU NJEMA
 
Ila sasa kwa hiyo wale wabunge wasio na chama Mama anaruhusu waendelee kuwepo na kunajisi muhimili?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom