Rais Samia na CCM wenzangu, ni utamaduni wa siku nyingi kila Rais kuwa na Waziri Mkuu wake, tunaomba utamaduni huo uendelee!

Kubadili Waziri Mkuu bila ya sababu zisizoepukika ni gharama sana, kwani tunakuwa na msururu wa mawaziri wakuu wastaafu wanaohudumiwa na serikali.

Sasa hivi tuna Salim, Warioba, Malecela, Msuya, Sumaye, Lowassa, Pinda. Wote ni mawaziri wakuu wqnaohudumiwa kwa stahiki za wastaafu.

Unataka kuongeza Majaliwa naye?

Kwa sababu hii, hutaona Waziri Mkuu akibadilishwa.
Kama sababu ipo hili sio tatizo. Kukiwa na tatizo kiutendaji ni hasara zaidi. Lakini kama hakuna shida ni vizuri kuendelea na aliyepo.
 
Ni kawaida kwa Rais, mara tu anapoanza awamu yake ya uongozi, kuteua Waziri Mkuu wake,mtu anayemwamini,atakayeenda na falsafa yake, bila kumuwekea makundi.

Marais huwa wanaachana na Mawaziri wakuu wa watangulizi wao kuashiria zama mpya, pia kuvunja kundi la kisiasa la aliyemteua.

Ni wazi, lile kundi lililokuwa na imani na ndugu yule likiangalia katika safu ya uongozi, linaweza kujaribu kumtikisa mama kupitia kwa huyo. Maana safu nzima imebadilika. Na sasa wananchi wanamuelewa sana mama kuliko wakati mwingine.

Ni vyema wasimamizi wakuu wa Sera za mwendazake, sasa wampishe mama atusukie nchi ya kisasa ya kisomi na ya kitaasisi

#matege
Code-SSH-2025
Uzandiki mtupu. Mmezoea serikali za majizi sasa kikwazo chenu mmeona ni Majaliwa, mmeshashindwa tayari. Wengi watageuka mawe ya Chumvi ila sio huyo mwamba.
 
Alikuwa njia panda, hawezi kukemea, hawezi kujitoa.
Hii inathibitishwa na hatua anazochukua.
Basi hana uzalendo wowote, ni unafiki tu. Kama angekuwa na uchungu kwa yale asiyoyapenda kwanini asijitoe?.
 
Watu wanaanza kumchimba Majaliwa

Majaliwa anaingia kwny record ya Cleopa David Msuya kuwa Waziri Mkuu wa Marais Wawili tofauti hapa nchini
 
Ni kawaida kwa Rais, mara tu anapoanza awamu yake ya uongozi, kuteua Waziri Mkuu wake,mtu anayemwamini,atakayeenda na falsafa yake, bila kumuwekea makundi.

Marais huwa wanaachana na Mawaziri wakuu wa watangulizi wao kuashiria zama mpya, pia kuvunja kundi la kisiasa la aliyemteua.

Ni wazi, lile kundi lililokuwa na imani na ndugu yule likiangalia katika safu ya uongozi, linaweza kujaribu kumtikisa mama kupitia kwa huyo. Maana safu nzima imebadilika. Na sasa wananchi wanamuelewa sana mama kuliko wakati mwingine.

Ni vyema wasimamizi wakuu wa Sera za mwendazake, sasa wampishe mama atusukie nchi ya kisasa ya kisomi na ya kitaasisi

#matege
Code-SSH-2025
2025 atateua mwingine baada ya uchaguzi mkuu
 
Nakwambia hivi, mtapiga soga sana hapa JF, lakini Waziri Mkuu habadilishwi.

Haya ni mambo ambayo uongozi wa CCM ulishayapitisha, si maneno ninayosema mimi tu.

Kama unataka kuchangamsha baraza, endeleza soga.

Kama unataka kuelewa nini kitatokea na sababu zake, nishakueleza.

Wakati jaji Warioba na tume yake wanakusanya maoni juu ya katiba mpya, nilipendekeza kusiwe na kiongozi analipwa maisha yake yote. Nilipendekeza kiongozi akistaafu apewe nyumba sehemu atakayopendekeza, kisha malipo yaanze 200m-2b kulingana na nafasi husika kisha akapambane na hali yake. Huu mchezo wa kulipa mstaafu mpaka afe sio kabisa. Unamlipa mstaafu halafu unakuta alipokuwa madarakani alikuwa mwizi, katili na kuingiza nchi kwenye mikataba michafu, hii haikubaliki.
 
Majaliwa ni mchapakazi wa hali ya juu.

Kumbuka kuwa awamu ya tano JPM alimkwaza sana Majaliwa, watu kama Makonda na Kakoko hawakumheshimu.

Kaka wa bandari ikafikia hatua anamsema wazi kabisa akiwa amekaa na ndugu zake kwenye meza za waalikwa wa harusi, akisahau kuwa pembeni yake wamekaa watu wa TISS.

Makonda aliwadharau mawaziri ikafikia hatua Dr Mpango akaamua liwalo na liwe akajibu mapigo.

Majaliwa unaweza kumuweka kundi la Hayati lakini alikumbana na mikwaruzo ambayo Rais Samia anaijua vizuri.

Awamu hii anafanya kazi bila ya uwepo wa wambea na ma-snitch wa mkuu kabisa.
Majaliwa yupo vizuri, utawala wa mwendazake bashite alikuwa na nguvu kuliko hata Prime minister.

Li-makonda halifai kupewa nafasi yoyote serikalini ,Wala kupewa favor yoyote huko kwenye biashara zake
 
Naunga Mkono. Rais Samia teua Waziri Mkuu wako huyu alisimamia serikali iliyofanya uonevu mwingi sana kwa raia zaidi iliyowahi kuwepo hapa Tanzania hapo kabla. Mpumzishe kama ulivyofanya kwa Bashiru
Katika hiyo serikali samia hakuwepo?
 
Ungesimamia kwenye ile hoja ya kuongopea Taifa wakati ule hoja yako ingekuwa na uzito zaidi kuliko hiyo ya kusema kila rais na PM wake .

Kitendo cha kusema uongo ulokuja kuthibitika kwa jamaa kufa kingetosha kumshinikiza kujiuzuru hata kama kwa hiyari yake angekuwa hayuko tayari.

Kwamba ataaminikaje tena na wananchi?

Je inatakuwa na maana gani kuwa na kiongozi mkubwa ambaye hataaminika tena kwa wale anaowaongoza?

Kwamba kila atakachokisema au kukifanya wananchi watamchukuliaje baada ya kitendo kile?

Kwanini afanya vile?

Nini kilimsukuma kufanya vile?

Kwa manufaa au maslahi gani na ya nani?

Tunataka majibu.

Hapo mleta mada yamkini ungeeleweka vizuri na kuufanya mjadala wako kuwa na radha.
 
Wakati jaji Warioba na tume yake wanakusanya maoni juu ya katiba mpya, nilipendekeza kusiwe na kiongozi analipwa maisha yake yote. Nilipendekeza kiongozi akistaafu apewe nyumba sehemu atakayopendekeza, kisha malipo yaanze 200m-2b kulingana na nafasi husika kisha akapambane na hali yake. Huu mchezo wa kulipa mstaafu mpaka afe sio kabisa. Unamlipa mstaafu halafu unakuta alipokuwa madarakani alikuwa mwizi, katili na kuingiza nchi kwenye mikataba michafu, hii haikubaliki.
Tulisema tunapiga marufuku uchifu, tuwe na jamii ya watu walio sawa. Wasio na madaraja tofauti.

Lakini kiukweli bado tunaendeleza uchifu.

Watu wengine wanalipwa maisha yao yote hata baada ya kustaafu, wengine wanaachwa wapambane na hali zao.

Hii si jamii ya watu sawa wasio na madaraja. Hii ni jamii ya watu wenye madaraja tofauti.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom