Rais Samia, Mwanza: Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya utatoka hivi karibuni, wote ni vijana. Mkipata fursa hizi mkafanye kama ilivyotarajiwa

Afadhali nimeambiwa jina langu nalo liko kwenye ile bahasha nyeupe na karatasi nyeupeeeee. iliyosainiwa kwa wino mwekundu hahaaaaaaaa just jokng.....naona Waganga wakipata pesa sana watu wanazindika , wanafanya shirki,wanatumia talasimu na hirizi ili wasing'olewe just to remind and let you know Rais halogeki...poleni.kazi njema ndio itawalinda.
 
  • Thanks
Reactions: vvm
Rais amesema Leo kuwa Ma-DC wote wapya watakuwa vijana maana karibuni anataka kufanya mabadiliko makubwa na wote watakaochukua nafasi ni vijana.

Kama ni kweli hii basi Natoa pongezi kwake.
Hapo atakuwa ameshindwa kazi uamuzi wa kuamini vijana wengi katika teuzi ndio uliotia doa utawala wa mwendazake.
 
kwa hilo siungi mkono tutashuhudia vituko balaa, Hapi. Makonda, Jerry Muro, Sabaya, Chalamila, DC Iringa hao wote vijana
 
Mkwewe Waziri,

Mwanae Mbunge,

Ndugu ya Waziri wa Mambo ya nje, Balozi,

Sasa wewe mnyonge Nani anakujua ??
Yeye kazi yake ni kuongeza vichwa kwenye mikutano ya wanasiasa, kuimba nyimbo na kufanya vurugu🤣
 
Rais amesema Leo kuwa Ma-DC wote wapya watakuwa vijana maana karibuni anataka kufanya mabadiliko makubwa na wote watakaochukua nafasi ni vijana.

Kama ni kweli hii basi Natoa pongezi kwake.
Pongezi za nini kama siyo upeo finyu wa kuona mbali? Tatizo la vijana ni kubwa ni zaidi ya kupewa u-DC. Hizi ndizo zinazoitwa siasa uchwara za kufunika real problem na ku-deal na petty issues.
 
Pongezi za nini kama siyo upeo finyu wa kuona mbali? Tatizo la vijana ni kubwa ni zaidi ya kupewa u-DC. Hizi ndizo zinazoitwa siasa uchwara za kufunika real problem na ku-deal na petty issues.
Isitoshe hili ni dili la UVCCM tu. Nashangaa watu wamefurahi kweli kweli. UVCCM wenyewe hawa wengi pasua kichwa tu!
 
Tatizo hao vijana ni wale wanaojuana na Rais na wasaidizi wake.

Utaratibu wa sasa hautoi fursa sawa kwa waTZ wote kuweza kupata nafasi na kutumikia Taifa hili.

Upendeleo ni mkubwa sana kwa wanaojuana na Rais na wasaidizi wake.

Hapo kuna kundi kubwa la watanzania wananyimwa haki zao.

Tunataka Katiba.
 
Mwangomango, mwanasheria msomi, mtetezi wa haki, rais mstaafu Law School of Tanzania, mgombea ubunge jimbo la Rungwe uko wapi/? Kijana mchapa kazi.
Nauliza mimi kama mtumishi wa Bwana, yuko wapi?
Hahahaaha vijana wa kitanzania mmeona ahadi ya mama? mmeambiwa vijana tu ndo watapata teuzi za UDC , Daa kwa pembeni namuona kijina anakenua meno na kupiga makofi nakusema Madam katukumbuka, Huku hajulikani hata UVCCM na hajui kuwa hizo nafasi ni za vijana wa vigogo serkalini na si za watoto wakulima. Maneno matamu ila.... matokeo....Vijana hakuna atakaye leta suluhu ya changamoto zetu tujitahidi kufanya kazi na kutochagua kazi ukiamka asubuhi buni chechote cha kufanya ili hata ukipata elfu 5 kesho utapata elfu 7 na kuendelea wanasiasa tutawalaumu tu bure maana wao watakuja kwetu wakitupa maneno mataumu maana walishajua kuwa tunapenda kusikia maneno matamu ila hatupendi kusikia maneno machungu yenye ukweli yatakayo tufanya kila mtu achukue hatua ya kujipambania kwake yeye na kizazi chake.
 
Back
Top Bottom