Rais Samia muulize Bilionea Alhaj Aliko Dangote alitaka umpe nini ambacho hajapewa?

Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
2,371
2,000
Mpendwa Rais wangu umejitahidi sana kututoa hofu wa Tanzania kuwa unaweza na jinsia yako sio kitu cha kushindwa kuongoza jahazi na tumekubali na kukupokea kwa mikono miwili yawekana kabisa ukaja kuwa mkombozi wetu kwa nchi yetu.

Naamini kwa muda mrefu taifa lilikosa mtu kama wewe na moderating factor katika Governance.

Kuna tahadhali tunayo sisi wananchi wako hasa kuhusu wawekezaji wanaokuja kukuona na kutoa maomba mbali mbali. Na mfano mzuri ni Dangote, hatujui aliomba nini zaidi mbali ya aliyotunukiwa mpaka muda huu.

D1.jpg

DOCUMENTS NDIYO ZITASEMA UKWELI KAMA HAYA YAFUATAYO ALIZAWADIWA DANGOTE BURE.

1) @ &#%*^/#%_=÷×+
2) Mliimpa ardhi bure bila kulipia senti tano.
3) Mliimpa eneo la kuchimba lime bure bila kulipia senti tano.
4) Milimpa bure eneo la kuchimba gypsum bila kulipia senti tano.
5) Mlimmpa uhuru wa kuingia wafanyakazi anavyoona na wengi hawakupata na vibali.
6) Mlimsaidia kuingia magari ya kusambaza sementi bure bila kulipia ushuru mbali ya mntambo.
7) Alipo lalamika kuhusu coal makaa ya mawe mliimpa bure ili achimbe mwenyewe bila kujali sheria ya madini inasameje.
8) Alipata tax holiday ya miaka mitano, afanye biashara yake bila kulipa kodi.
9) Mlimpelekea bomba lá gesi mpaka kiwandani kwake wakati wawekezaji wengine hugharamia wenyewe.
10) Kiwanda bado ni kidogo kuliko Twiga Cement (wazo) ambao yote hayo walilipia kuwapata na hata kodi ya ardhi wao wanalipa.
11) Je, hii ya kuzoea bure kuna fanya malipo ya statuary contributions kama NHIF, NSSF, WORKERS COMPENSATION FUNDS, na michango mingine pamoja na Corporate social responsibility aone atapata bure?

Mkidai kodi halisi anasema anapata hasara yaani mumempa kila kitu bure na sasa anapata hasara na wazalishaji wengine kodi na kulipia huduma zote na kodi kama Twiga Cement, Simba Cement, Mbeya ya cement na viwanda vingine 19 vya kuzalisha cement. Viwanda vyote vingine vinapata faida na kulipa kodi. Haya tutafika.

Marais waliopita ama walikuwa too soft ama extremists lakini mama kuingia kwako tunaamini kuna mazuri yanakuja. Kwa uchache tuu tunaomba ujielekeza kwenye mambo machache muhimu lakini ndio yatakuwa game changer kwa nchi yetu.
 
Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
2,371
2,000
Magembe hivi vitu umesema alipewa bure una ushahidi?
Haya ni maoni tuyapokea na hapa ndipo pá kuuliza, na kuondoa kiwingu. Nimeandika na saidi a kusema kwa sauti wengine wanasema kimya kimya kama ni uwongo unasambaa kumbe sio kweli.
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,321
2,000
Haya ni maoni tuyapokea na hapa ndipo pá kuuliza, na kuondoa kiwingu. Nimeandika na saidi a kusema kwa sauti wengine wanasema kimya kimya kama ni uwongo unasambaa kumbe sio kweli.
Kwahio ni Allegations AKA Inasemekana ?

Ili wasikuite muongo labda ongezea hapo neno kabla ya hizo shutuma kwamba inasemekana...

Anyway kuondoa huu mzizi wa fitina hii mikataba iwe inawekwa kwenye public eye kila mwenye macho aone na kabla haijasainiwa ipelekwe Bungeni ichambuliwe
 
ikigijo

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
1,220
2,000
Mkuu mengii uneandika Ika Sijaona Uliposema pia Ameajiri Management yooote ni Wahindi.

Si ni Bora nikauza Ndizi kuliko kusimamiwa na Muhindi!Yaani Kazi ambazo Watanzania wanaweza kuzisimamia Yeye Kaweka Muhindi,Kenya hii kitu Haipoooo,Hata Kwao Nigeria haipooo.

Watanzania wakilata Nafasi za Management hapo watalipa Kodi,Watalipa Nssf,Kutakuwa na Multplier effect kwa Jamii nk nk!
 
Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
1,258
2,000
Kama kweli halipi hata kodi sababu ya hasara kwa nini yeye aonekane kama kaleta neema kuliko hao uliosema wanalipa kodi yaani Twiga cement na wengine? Au huna uhakika?

Japo kwa uzoefu wa kukaa mgodoni miaka kadhaa,wawekezaji hawapendi kulipa kodi sahahi huwa wanajazia operating costs kubwa ili tu faida isiwepo au iwe kidogo sana.

Jamaa wale wa mgodini wamekuwa wakichimba usiku na mchana ila wanatuambia hawaja wahi pata faida.Swali tukauliza kwanini wasifunge mgodi maana ni zaidi ya miaka 10 sasa wanachimba ,majibu ni chenga mtupu.
 
fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,874
2,000
Hivi kwann kila siku Dangote ni yeye tu Ikulu kwa kila Rais anayeingia?
Je hata viwanda vingine vya cement wako hivyo?

Mi napata mashaka na Huyu bilionea wa Africa,huenda utajiri wake umegubikwa na favor nyingi ambazo kuna watu chini kwa chini wananufaika nate.
Daily Ikulu??????
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,953
2,000
Kwahio ni Allegations AKA Inasemekana ?

Ili wasikuite muongo labda ongezea hapo neno kabla ya hizo shutuma kwamba inasemekana...

Anyway kuondoa huu mzizi wa fitina hii mikataba iwe inawekwa kwenye public eye kila mwenye macho aone na kabla haijasainiwa ipelekwe Bungeni ichambuliwe
Hivi kwenye hili Bunge la akina Ndugai, kuna mwenye uwezo wa kuchbua mikataba?
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,953
2,000
Kama kweli halipi hata kodi sababu ya hasara kwa nini yeye aonekane kama kaleta neema kuliko hao uliosema wanalipa kodi yaani Twiga cement na wengine? Au huna uhakika?
Japo kwa uzoefu wa kukaa mgodoni miaka kadhaa,wawekezaji hawapendi kulipa kodi sahahi huwa wanajazia operating costs kubwa ili tu faida isiwepo au iwe kidogo sana.
Jamaa wale wa mgodini wamekuwa wakichimba usiku na mchana ila wanatuambia hawaja wahi pata faida.Swali tukauliza kwanini wasifunge mgodi maana ni zaidi ya miaka 10 sasa wanachimba ,majibu ni chenga mtupu.
Tatizo mlikuwa mnasikiliza sana porojo za marehemu.

Ni mgodi gani walisema kuwa wamekuwa hawapati faida? Hakuna mgodi uliowahi kutoa hiyo kauli.

Walchoeleza ni kuwa hawajarudisha hela waliyowekeza. Na kwa vile bado hawajarudisha, hawawezi kulipa corporate tax, amvayo huwa ni 30%. Lakini kodi nyingine zote pamoja na tozo mbalimbali wamekuwa wakilipa.

Kwa bahati mbaya, wajinga wasioelewa mambo haya, walishindiliwa ujinga, mpaka wengine baadaye wakaondoka kwenye ujinga na kuhamia kwenye uwendawazimu.
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,953
2,000
Hivi kwann kila siku Dangote ni yeye tu Ikulu kwa kila Rais anayeingia?
Je hata viwanda vingine vya cement wako hivyo?

Mi napata mashaka na Huyu bilionea wa Africa,huenda utajiri wake umegubikwa na favor nyingi ambazo kuna watu chini kwa chini wananufaika nate.
Daily Ikulu??????
Hujui mambo ya uwekezaji. Ungekaa kimya, jitahidi ujielimishe kwanza. Dangote mara zote amekuwa anaalikwa, siyo yeye anayeomba kukutana na Rais.

Marehemu alimwalika, kulipokuwa na taarifa kuwa anahamishia kiwanda chake Kenya.

JK alimwalika kumwomba awekeze nchini.

Mama amemwomba ili uwekezaji wake wa sasa uwe ja tija, na ikiwezekana awekeze zaidi. Huyu ni tajiri na mwekezaji mkubwa kwa kiwango cha kimataifa. Kila nchi inataka uwekezaji wake.
 
zithromax

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
2,156
2,000
Mkuu mengii uneandika Ika Sijaona Uliposema pia Ameajiri Management yooote ni Wahindi...
Si ni Bora nikauza Ndizi kuliko kusimamiwa na Muhindi!Yaani Kazi ambazo Watanzania wanaweza kuzisimamia Yeye Kaweka Muhindi,Kenya hii kitu Haipoooo,Hata Kwao Nigeria haipooo!
Watanzania wakilata Nafasi za Management hapo watalipa Kodi,Watalipa Nssf,Kutakuwa na Multplier effect kwa Jamii nk nk!
Mama alisema tusimpagia mwezkezaji aweke watu gani ,mwekezaji atamwajiri yotote anayemwamini Kuwa akiwa shilingi moja baada ya mwezi zitakuwa shilingi mbili
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
8,642
2,000
Wazo sio kubwa kuliko dangote..
kwa sasa Dangote ndio kiwanda kikubwa interms of production tonnage per day..

Dangote aliomba auziwe gas kwa bei ya Mtwara sio ya Dar es salaam..., gas pipeline limepita upande wa pili wa kiwanda ukivuka barabara...mweye jukumu la kusupply ni TPDC, Dangote yeye amejenga gas plant kwa gharama zake...

Ugomvi wa Dangote ni kugeukwa na awamu ya tano nje ya makubaliano ya awamu ya nne....complain yake ni yeye kuja kuwekeza based taratibu na makubaliano yake na awamu ya nne....awamu ya tano ghafla bin vuu inabadili taratibu na kuleta taratibu mpya na hawataki mazungumzo....wewe ungefanyaje?...

Dangote ananunua gas, Dangote ananunua maji, Dangote ametoa ajira kwa watu zaidi ya 2000, PAYE za watu zaidi ya 2000, NSSF zaidi ya watu 2000...Dangote anasupplier wakibongo wanaolipa kodi....unajua faida ya watu 2000 wakiwa na ajira kwenye mji?... Dangote ameleta cement sokoni kwa 10K cheaper than all...road toll ya magari zaidi ya 500....nk nk nk..

La msingi ni Serikali kumshinikiza Dangote alipe vizuri watu wetu, Aajiri wazawa wengi na kuwapa training, Dangote amentain price ya cement 10k au kushuka chini...nk nk
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,042

Nimependa, hasa mstari wako wa mwisho.

Na kama mama atahakikisha maslahi haya ya taifa hayachezewi kwa vyovyote tupo naye; lakini asijisahau na kudhani hao wawekezaji ndio kila kitu kwa manufaa ya taifa letu.
Sisi wenyewe ndiyo kila kitu, kwa hiyo asisahau wajibu huo kwetu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom