Rais Samia Mteue Ubunge Prof. Mussa Assad Kisha mteue awe waziri wa Fedha na Mipango

Mwenzio alisema Mwigulu ananukia mahela ikawa ndo base ya kumteua teh teh teh teh
Mama akitaka kufanikiwa afanye kaz na watu wa calibre ya Prof Assad,chale kime, khamis kagasheki and the like !!! Aaachane na haya manyika eti mwigulu
 
Punguzeni mihemko...mnahemkwahemkwa sana. Mtu anaelekea retirement.. Alafu usikute ww nikijana na unalia huna ajira... Eti Kimei awe waziri...? nonsense
 
Hawezi kuteuliwa kwa sababu zifuatazo
1.Katiba hairuhusu
2.sio Mchumi
3.Hana adabu juu ya Mamlaka in short ni mnafiki na mpigaji.
4 ni mdini.
 
Nakusalimu kwa jina la Tanganyika +Zanzibar

Tunapoelekea kuumaliza mwaka 2021 uliojaa kila aina ya misuko suko na maumivu..na kuukaribisha mwaka 2022..ambapo tunaamini nakutarajia yaliyo heri katika nyanja mbalimbali za kiuchumi..kijamii..kiafya na kisiasa.

Hivyo basi naombi kwako kama rais na kiongozi wetu ambaye unatamani hii nchi ipate mafanikio makubwa katika nyaja zote.

Ombi langu kwako ni kukuomba kwa nafasi yako mteue Prof Assad aliyekua CAG kuwa mbunge na kisha ikikupendeza zaidi awe waziri wa Fedha na Mipango.

Kwa maana ni mtu kwanza msomi wa ngazi kubwa ya kielimu katika masuala ya uchumi na fedha..pili ni mzalendo mwenye weredi..tatu na mtu mwenye msimamo anayesimamia principle na miongozo ya kazi...pamoja na hayo ameonyesha uwezo mkubwa sana pindi alipokua CAG kwa kutekereza majukumu yake ipasavyo..hadi baadhi ya wahuni kuanza kuchukia na kumletea figisu.

Nakuomba sana ili ufanikiwe katika kauli mbiu ya kazi iendelee fanya kazi na wanataaluma wenye uwezo..achana na wanasiasa ambao wengi wao huwazia zaidi chaguzi zianazofuata hivyo hufanya mambo sio kwa maslahi ya taifa bali kwa maslahi yao ili waweze kushinda chaguzi za mbele yao.

Nihayo tu kwa leo..naamini wazee wa vetting mtamfikishia mama hili na kumsadia katika hili ili tuweze kusonga mbele kiuchumi na kimaendeleo.

#MaendeleoHayanaChama View attachment 2063951
Kuongoza hapa Tzn sio tuu taaluma inatakiwa ni pamoja na utamaduni wa jamii.

Wasomi aina yake wengi tuu wamefeli walipotaka kutumia taaluma zaidi refer Prof wa Uchumi wa gas..

Pili huyo kwangu hafai Kwa sababu namuona anaamini kwenye sera za kubana matumizi sasa kwa Uchumi kama wetu unapobana matumizi inaleta umaskini kwa sababu Watu hawana vipato..

Anaweza tuu kuwa mshauri kwenye planning commission hasa namba ya Kuboresha government service yaani utumishi wa umma..

Of course kuna maeneo mengi ya kupunguza gharama za utawala yasiyo na tija ila sio kupunguza spending au kutegemea uchumi wa ndani tuu.
 
Huyu hafai. Hata Marope hakufaa kuwa kwenye cabinet. Na Nepa naye hawezi kuwa kwenye cabinet.
Watu wasioweza kumvumilia kiongozi mkuu wa nchi ni hatari sana.
Lakini pia kuteuliwa kwao kunaleta funzo baya hata kwa wengine. Kwamba unaweza ukatunisha misuli kwa viongozi wa juu wa nchi, na bado serikali ikakuona unafaa?
Ni sawa na mama kushabikia mtoto anayeoonyesha ukorofi wazi wazi kwa baba, hata kama wazazi wana ugomvi.
Mtu anayeweza kuonyesha unafiki na ukorofi wazi wazi kwa mkuu A wa nchi, bado anaweza akamgeuka mkuu B wa nchi.
Sio watu wa kuwaamini kwenye serikali.
Kwenye utumishi wa umma na uongozi wa umma hata kama boss ni kilaza, basi heshimu hicho kiti (cheo chake).
Watu wanaonyesha dharau ya wazi wazi kwa cheo katika public leadership hawafai hata milele kurudi kwenye public leadership position.
Mkuu
Hapo nadhani unashindwa kutofautisha mtu kuwa na "Confidence " na hali ya kuwa na "Arrogance ". Nisameheni maneno hayo sina kiswahili chake kizuri.
Prof Assad alikuwa na Confidence ya anacho kijua, kifanya. Japokuwa walionekana mkorofi hasa kwa wale miungu watu.
2. Arrogance ni pale unapokuwa jeuri, dharau na wakati mwingine kuwa mjuaji unayejiona unajua kila kitu hali hujui.
Pale unapo lewa madaraka na kuwajibu ovyo k.m " Asiyetaka aende Burundi " hiyo ni dharau na arrogance ya hali ya juu.
 
Mkuu
Hapo nadhani unashindwa kutofautisha mtu kuwa na "Confidence " na hali ya kuwa na "Arrogance ". Nisameheni maneno hayo sina kiswahili chake kizuri.
Prof Assad alikuwa na Confidence ya anacho kijua, kifanya. Japokuwa walionekana mkorofi hasa kwa wale miungu watu.
2. Arrogance ni pale unapokuwa jeuri, dharau na wakati mwingine kuwa mjuaji unayejiona unajua kila kitu hali hujui.
Pale unapo lewa madaraka na kuwajibu ovyo k.m " Asiyetaka aende Burundi " hiyo ni dharau na arrogance ya hali ya juu.
Assad ni mjuaji(arrogant).
 
Ukitaka kudharauliwa jiingize kwenye siasa zetu za bongo
Mzee Assad acha atulie zake kwa heshima kabisaa
Huu upuuzi wa siasa una watu wakee
 
Back
Top Bottom