SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Mhe Rais Samia Suluhu Hassan hongera na pole kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya katika kufungua nchi yetu, kuhakikisha nchi yetu utawala wa sheria na uadilifu katika kila sekta nchini na wananchi kwa ujumla unashamiri huku ukihimiza utatuzi wa kero za wananchi na uwekaji wa mazingira wezeshi kwa uwekezaji nchini. Sisi tunakuelewa na tunakuombea heri ufanikiwe zaidi.
Mhe Rais Mama yetu anaitwa Hannelore Morgan Manyanga alikuwa mkuu wa kitengo cha sheria idara ya uhamiaji akitumikia cheo cha kamishna ila alihusishwa kwenye sakata la kuingiza stika feki za viza nchini zikitokea Afrika Kusini na tangu akamatwe na kuwekwa gereza la Segerea ni zaidi ya mwaka mmoja sasa huku watuhumiwa wenye mzigo wa stika hizo wakiwa waliachiwa huru na mahakama.
Kwa heshima kabisa tunaomba ofisi yako tukufu itusaidie kulitazama faili lake ili haki itendeke kwani mama yetu aliandaa kesi ya hao walengwa ambao baadae waliachiwa kwa mujibu wa sheria. Kwa heshima Mhe Rais tunaomba msaada wako utusaidie mama yetu.
Tunakutakia afya njema.
#KaziIendelee #ZegeHalilali