Rais Samia: Msiseme Mama anazunguka tu, sitozunguka bila sababu

Sina uhakika kamaSamia ana mkono katika kesi ya kumbambikia Mbowe, lakini mambo katika mengine mengi, I support Madam president.

Katika yote mazuri yenye dhamira njema, Mungu akubariki Samia, na akujalia hekima zaidi. Mapato yanapoongezeka kwa kiwango cha kuridhisha, punguza au ondoa baadhi ya kodi na tozo. Hiyo itapunguza ukali wa maisha, itaongeza uwekezaji na hatimaye kuongeza ajira.

Kesi ya kubambikiza kwa Mbowe, ndiyo doa pekee kubwa.
Sasa ya mboye yanaiigiaje hapa??
 
Kama mahindi yananunuliwa Kenya,mbona hayapandi bei toka tumevuna mpaka Sasahivi gunia la mahindi alizidi elfu 35000/ na ilikuwa hivo hata mwaka Jana
Mkuu ni kweli kbsa hata hii biashara ya mahindi kati ya kenya na tanzania mnufaika mkubwa ni kenya na si tanzania mahindi yetu yanaenda mpaka somalia na sehemu nying tu za kenya, Lakini bado kwenye kuuza hayo mahindi kenya ndo anapanga bei ya kununua na anaweza sema leo bei imepanda au kushuka ilimradi tu yeye apate faida kwako
 
mahoteli mengi yalikufa kwa kujifanya ati mikutano isifanyikie kwenye mahoteli, tena ya watanzania, mnataka hizo hela za serikali wale wazungu tu? kufanyia mikutano kwenye hotel za kibongo/lodges etc inakuza uchumi pia kwasababu mahoteli yatajiimarisha,yataajiri wafanyakazi ndio ajira hiyo na watalipa kodi. mitindo ya kuua biashara kama awamu iliyopita hatuihitaji kwasasa.
 
muacheni azunguke si ndio anachokiweza jombaa kwani unafikiri kuna kitu mule?
Usijitie upofu, kwani hamuoni kazi anayo fanya au wewe ni muathirika wa utawala wa kiimla ulio pita.
Au tuambie ulitaka afanye Nini ambacho haja fanya toka aingie madarakani, ili tukujibu.
Kutwa uko kijiweni huku unalalamika, fanya kazi uliletee Taifa maendeleo kwa kulipa Kodi na huwenda hata hujawahi kulipa Kodi ya aina yoyote umebaki kulinyonya Taifa na kulalamika tu.
Au kufufua viwanda vilivyo kuwa vimekufa ili wananchi watapata ajira kwako wewe ni ujinga.? Fika mahali uwe hata na mshipa wa aibu.
 
Bi mkubwa bwana.. inaonekana hana kitu cha kufanya ofisini, mipango hakuna
Unajifanya kujua mipango ya ofisi ,haya tuambie Kama kazi gani ambayo ulitaka afanye Kama sio kutoka na some kwa macho yake kero zinazo wakera wananchi.
Na ndivyo kiongozi bora anavyo takiwa kuwa.
 
Kama sio kutoka na some kwa macho yake kero zinazo wakera wananchi
Sipingi ziara lakini napinga utetezi wako hapa. Mwaka jana kwenye kampeni alitembea karibu nchi nzima. Nina imani kero aliziona na uzipata. Ashughulike na zile za mwaka jana alizoziona kwanza.
 
Mleta Uzi ulianza vizuri Lakini nilipoanza kusoma points zako nikagundua wewe ni pure"SukumaGang".
 
Hangaya hicho ndio anaweza pekee
Na Kuweka Shada la Maua Nyerere Day kwa Hayati Magufuli badala ya Mhusika wa Siku na Tukio Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Imenikera mno tu mpaka leo na nimeshaanza Kumpunguzia 'Marks' zake kadhaa kwani ameanza Kuonyesha Mapungufu na Kunikatisha Tamaa ya Kumkubali na Kumuamini mapema sana tu.

Na Kitendo chake cha kupenda Kusikiliza Ushauri wa Mstaafu ambaye GENTAMYCINE simkubali na sikumkubali ambaye ni 'Mswahili' na ameliharibu mno Taifa hili ndiyo kunazidi tu kunifanya nisimkubali.
 
Wazalendo fake hao wasikusumbue, wakiambiwa watoe tozo hawataki, mother akienda nje kutafuta vijisenti hawataki! Scars alizoacha magu kwenye bongo za waTZ wengi ni tatizo kubwa, natamani watu wote tumuunge mkono Mama kipindi hiki anajaribu kuwabadili hawa watu waliojengewa ujinga kwa miaka 5, Eti MABEBERU, si ndiyo hao alikuwa anaenda kuwakopa mikopo ya mariba makubwa makubwa?
Kujitegemea ni vizur tusiombe Bora tukope pesa, mbona ma Raisi wa nchi nyingine hawa zururi hovyo mfano Botswana, Namibia, Ghana, Vietnam, Thailand, Iran, kwanin viongoz wetu wana amini maendeleo yana kuja Kwa kuomba pesa wazungu
 
CCM watakuwa na kazi kubwa sana kwenye kampeni aisee, Magufuri alisema hasafiri sababu nchi yetu ni tajiri wenye shida ndio wanakuja, huyu tena naona kama anageuza hiyo kauli.

sasa sielewi hawa watu huwa wanapewa Ilani au Ilani ndio inajichanganya namna hii
Hakuna ilani isipokuwa matamko
 
Mkuu ni kweli kbsa hata hii biashara ya mahindi kati ya kenya na tanzania mnufaika mkubwa ni kenya na si tanzania mahindi yetu yanaenda mpaka somalia na sehemu nying tu za kenya, Lakini bado kwenye kuuza hayo mahindi kenya ndo anapanga bei ya kununua na anaweza sema leo bei imepanda au kushuka ilimradi tu yeye apate faida kwako
Kwanini tusiwe na viwanda vya kutengeneza unga?
 
Kwanini tusiwe na viwanda vya kutengeneza unga?
Kama utakuwa unafuatilia biashara nyingi za wakulima wa tanzania lazima utakuta kwamba kuna tatizo la masoko hata huo unga unahitaji mitaji na package nzuri then masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi ndo tunaweza fanikisha mkuu, Ukivuka tu boda ya sirari unakuta mahindi yetu yako kwenye unga yaani wamesaga na kupack na kupiga chapa yao ya kenya wakati mahindi ni ya tanzania kabisa
 
Kama utakuwa unafuatilia biashara nyingi za wakulima wa tanzania lazima utakuta kwamba kuna tatizo la masoko hata huo unga unahitaji mitaji na package nzuri then masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi ndo tunaweza fanikisha mkuu, Ukivuka tu boda ya sirari unakuta mahindi yetu yako kwenye unga yaani wamesaga na kupack na kupiga chapa yao ya kenya wakati mahindi ni ya tanzania kabisa
Ndege moja ingetengeneza viwanda vingapi vya unga na ajira? tatizo ni vipaumbele vya kijinga ndiyo vinatusumbua, kwani sisi hatuna mabalozi nje wa kutafuta masoko huko Sudan sijui wapi?
 
Kiukweli hapo ndo tatzo lipo ila kenya anatafuta masoko mpaka nje ya nchi ndo maana unaona hata matunda anauza ulaya ila ukija kwa watanzania maneno yanakuwa mengi sana, linapokuja suala la biashara kati ya kenya na Tanzania jua kenya yuko mbele sana zaidi yetu
 
Hatutaki kufanya biashara tu,

Ila tunataka kufanya biashara kwa usawa.

Kenya inaifanyia tanzania ujasusi wa kiuchumi kwa kila njia sisi tunakaa kimya tu.
 
"Tukizunguka msiseme Mama anazunguka tu, sitozunguka bila sababu, nilishacheza vya kutosha kwenye Nchi nyingi Duniani sasa hivi kazi ni moja tu kuzunguka kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania" ——— Rais Samia akiwa Arusha leo
FB6KTUcUcAQkiwY
 
Kimsingi wanaomsifia Samia ni wale wanaofaidika moja Kwa moja na utawala wake , na wale waliomsifia Maghufuli ni wale waliofaidika moja Kwa moja na utawala wake ...Sisi wanyonge tuendelee kucheza na beat mana kitaa pagumu siyo mchezo
 
"Safari nilizokuwa nafanya Nchi Jirani zilikuwa na lengo la kuondosha vikwazo, tumeondosha vikwazo na Kenya na biashara imekuwa mara sita zaidi ya ilivyokuwa, kwahiyo tukizunguka msiseme Mama anazunguka tu, sitozunguka bila sababu, nilishacheza vya kutosha kwenye nchi nyingi duniani, sasa hivi kazi ni moja tu kuzunguka kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania" -Rais Samia akiwa Arusha leo
Unafanya kazi vya kutosha mama Samia, huzunguki bure, unatutafutia kila mahali. unafanya kazi nzuri, asiyeona hana macho hata kidogo.
 
Back
Top Bottom