Rais Samia: Mikopo ya Wahisani ina Riba kubwa

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,864
2,000
Kama mikopo ya wahisani nina riba kubwa kubwa na ule wizi unaofanyika kkwenye fedha za umma wahisani pia wanahusika?
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,924
2,000
WaTanzania tuache tabia ya kupenda kuwa Tegemezi. Hakuna mtu anayemthamini masikini, hasa masikini asiyekuwa na ndoto ya kujikomboa katika hali yake. Wenyewe mmesikia mahela yaliyokusanywa kipindi hiki kifupi cha tozo za miamala ya simu. Tukijipanga tunaweza sio kusubiri hela za wafadhili tu, ambazo zinatolewa na masharti mengi - kama vile haki za mashoga nakadhalika. Marehemu JPM alisema mara nyingi - nchi hii siyo maskini. Serikali ikijipanga vizuri , matumizi mazuri ya pesa za serikali na kila mtanzania kulipa kodi- tutafika mbali. Nchi kama Denmark- wananchi wao wanalipa kodi kwa asilimia kubwa sana. Hapa kwetu ni asilimia ndogo sana ambao wanalipa kodi stahiki.
Uchumi unapokuwa mzuri, ndipo mapato ya serikali nayo yanaongezeka. Kwani si ndiyo tulishawahi kuwa na kodi ya kichwa kabisa? Pesa zilienda wapi? Wananchi wanalalamikia matumizi makubwa ya viongozi kuanzia mishahara na maviete. Lakini badala yake hao viongozi ndiyo wanabuni mbinu kandamizi kabisa za kuzidi kumfukarisha mwananchi wa kawaida.

Pesa zitoke kwa wananchi au zitoke kwa wahisani, ufujaji ni ule ule. Kama tungekuwa serious, tungeanza na matumizi pamoja na mishahara ya viongozi. Hayo yote yanawezekana. Especially kwa kutumia katiba mpya. Zaidi ya hapo, ni unyonyaji tu kwa watanzania ambao wengi ni masikini.
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,055
2,000
Hayo ndo madhara ya uchumi wa Kati.
Sema nini Rais na Serikali iwaeleze watu uwazi kwamba nchi ikishakuwa uchumi wa kati ni kama mtoto ameshakua lazima kujitegemea.

Sasa hapo ukienda kwenye mikopo ni riba juu sio kama ile ya awali tukiwa LDC na pia lazima tutumie rasilimali na mapato yetu full stop.

Zile mind set za misaada watu wazifute rasmi vichwani.Watu wanawacheka Kenya,Zambia na Ghana kwa sababu zimelemewa na mikopo,sababu kubwa watu wanataka raha na rushwa na hawataki wakatwe kodi sasa Serikali haina options zikachukua mikopo ya Kibiashara na haya ndio madhara yake sasa.
 

kingkongtz

JF-Expert Member
Dec 28, 2019
735
1,000
WaTanzania tuache tabia ya kupenda kuwa Tegemezi. Hakuna mtu anayemthamini masikini, hasa masikini asiyekuwa na ndoto ya kujikomboa katika hali yake. Wenyewe mmesikia mahela yaliyokusanywa kipindi hiki kifupi cha tozo za miamala ya simu. Tukijipanga tunaweza sio kusubiri hela za wafadhili tu, ambazo zinatolewa na masharti mengi - kama vile haki za mashoga nakadhalika. Marehemu JPM alisema mara nyingi - nchi hii siyo maskini. Serikali ikijipanga vizuri , matumizi mazuri ya pesa za serikali na kila mtanzania kulipa kodi- tutafika mbali. Nchi kama Denmark- wananchi wao wanalipa kodi kwa asilimia kubwa sana. Hapa kwetu ni asilimia ndogo sana ambao wanalipa kodi stahiki.
"WATANZANIA TUACHE TABIA YA KUPENDA KUWA TEGEMEZI"

mkuu suala la kuwa tegemezi halitaisha kwa tanzania ,tukubali tu kuwa wazungu wametuzidi mbali tena sana hatuna ujanja.

unaposema tuache kuwa tegemezi maana yake tujitegemee (sawa na ile kijana anapoamua kutoka home na kwenda kupanga kila kitu inakuwa juu yake )

so unataka kunambia tutaweza kweli ???,

hiyo haina tofaut na yule mtu anayeandika kwamba anawachukia wazungu hatamani hata kuwaona wakati muda huo huo anatumia simu,miwani,saa na mengine mengi aliyotengeneza mzungu.


MFANO:wazungu wangesema jamani tunaijia vitu vyetu na nyie njooni mchukue vyakwenu kila mmoja abaki na vyakwake.nadhani hata raisi atatembea kwa mguu .

asilimia kubwa ya watanzania tunaishi chini ya $ ,hapo hapo uungezewe kodi kila kukicha et tunajenga uchumi wa kwetu wenyewe huku maisha yetu ya kuunga unga.

siku hizi unashangaa mtu amefungua biashara baada ya miez anafunga (mifumo ya kibiashara imevurugika hela mtaani amna)
 

KING KIGODA

JF-Expert Member
Dec 28, 2018
1,504
2,000
Kuna 2.3 trillion ya world Bank na 1.3 trillion ya imf kwa ajili ya corona mpo hapo ?
Hivi JPM alikua anatoa wapi hela za ujenzi wa madarasa ?

Nimeuliza tu jamani
Majibu wanayo wahanga wa NSSF,watumishi miaka 5 no kupanda daraja,wafanya biashara wakubwa kufanyiwa unyang'anyi na serika ikiwa ni pamoja na serikali kuikopa mifuko karibu yote ya jamii.
Kifupi Yule alifanya ujenzi kwa kunyonga haki za watu.
 

Ngamanda

JF-Expert Member
Jan 9, 2019
306
500
Kwani wale wa Danish ambao ni wahisani wakubwa kabisa wanaofunga ubalozi wao nchini walitoa sababu gani? Sidhani kama hii kauli ina ukweli. Waseme tu hawawezi kufuata demokrasia. Wahisani wana masharti ambayo wanahofia yatawapoka madaraka na hivyo kunyang’anywa tonge mdomoni.

Wanaona ni bora kuendelea kukamua ng’ombe aliyekonda na wao waendelee na ma viete yao wakitafuna keki ya Taifa kwa kupokezana.
Wewe unatakaje? Elezea kwa hoja watakusikia na kujirekebisha! Lawama tu si jibu.
 

wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
8,742
2,000
Shujaa aliwafundisha sana staff wake kua sio wakweli.Legacy yake kwa kweli inaishi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom